Ukisoma vizuri Biblia ni kwamba wana wa Israel baada ya kumuudhi Mungu kwa kuto kuamini kwao, Mungu akaamua kuwazungusha njia hiyo hiyo, kumbuka kuna maandiko Mungu alimwambia Musa kwamba atawaua wote kwasababu ya kuto kuamini kwao na Musa alimsihii Mungu kwamba asifanye hivyo kwasababu Wamisri watafikiri kwamba Mungu ameshindwa kuwafikisha kule aliko kua ameadhimia kuwafikisha so Mungu ilibidi afanye taratibu, yaani alisikiliza ushauri wa Musa (point to learn here, kama Mungu alimsikiliza mtumishi wake {binadamu} je viongozi wa kisiasa, kama rais au waziri) then tunasoma watu wazima pekee waliotoka Misri kuingia Kaanani/Israel ni 2 tu out of malaki yao nao ni Karebu na Yoshua; point yangu hapa ni hi, miaka hiyo yote walijikuta wanazunguka zunguka tu humo humo. Remember, watu hawa/Israel walifikaje Misri!? Walikwenda kwa miguu, kwanza was Yusufu/Joseph then miaka kadhaa baadae walikuja ndugu zake pamoja na mama zake na Masuria ya baba yake na huko ndiko waliko zaliana sana, hawakuchukua miaka mingi kufika hapo Misri. Nakumbuka hata Ibrahim (ambaye ndiye source ya hili taifa la Israel) nae aliwahi kimbilia kwenye hi nchi wakati Kaanani kuna njaa, nae hakuchukua miaka yote hiyo, kabla Yakobo na wanae hawajahamia Misri, watoto wake walifanya safari kama 2 hivi za kwenda na kurudi Misri wakitokea Kaanani, hawakuchukua muda wote huo, hapa walichukua muda mrefu kwasababu ya kuto kuamini kwao. Hope YEriko nitakua nimejibu kiasi changu