Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

chukua huo umri wako, jumlisha na miaka 40, nambie ungekuwa wewe ungefika misri ukiwa na miaka mingapi kama sio kikongwe? sasa kulikua na haja gani ya kuwatoa misri mpaka israel angali watu wangefika huko vikongwe havina hata uwezo wa kujenga vibanda vyao? unapoteza miaka yako ukiwa unarandaranda jangwani we umekuwa vumbi?

ujinga kwangu no.
haaaaa....nalipenda ""sana hili jukwaa
 
kulikua hamna haja ya kukagua wakati kila alipomaliza uumbaji alisema "akaona kuwa ni vyema, ikawa usiku, ikawa asubuhi" manake kila uumbaji ulimpendeza.
kusema Mungu alifanya ukaguzi siku ya 7 aone kama kila kitu kipo sawa ni kumkosoa Mungu kwamba anakosea. so Mungu wenu hajiamini mpaka afanye ukaguzi? kwanza huo mstari wa ukaguzi umeupata wapi wakati biblia inasema siku ya 7 ye alikua anakula bata tu?
hahaaaa mungu muweza wa yote mjuzi wa yote ...anafnya ukaguzi wa kazi yake tena.!? inamaana hata yeye hajiamini"" ? wakati huo huo kwwnye imani ya kiislam inasema kuwa mungu akitaka kufnya jambo anasema kuwa na lina kuwa "" sasa akishakuwa na uwezo huo anahaja ipi tena yakufanya ukaguzi wa kazi yake ""!?...mapya haya "" kwanza kwanini alipumzika" ? mantiki ya kupumzika "" nikumfanya kiumbe kuupumzisha mwili na akili yake baada ya kuchoka kufanya kazi Fulani""ama mwendo wa muda mrefu "" sasa Mungu muweza wa yote alifnya kazi kiasi kwamba akachoka akili na mwili" ikafikia hatua akaona nibora apumzike "" maana akili Yke na mwili vilikuwa vimeshachoka "" sasa hapa uweza na ujuzi wake wa vyote uko wapi""
kama hata yeye nae huwa anachoka""?? maana mnasema alipumzika ati

naamini uwepo wa Mungu "" lakini narejea kusema tena "" hivi vitabu vilivyotuletea hizi imani vinauwongo mwingi mnooo sana
 
Waliokuwa wakitoka misri kwenda Nchi Ahadi sio watu au kikundi ni taifa..

I mean ni kama nchi ya Tz yote inahama,so ni lazima ujue hata mwendo wa kutembea uwe mdogo.
Na ujue walikuwa watoto,watu wazima, wazee,mifugo n.k

So lazima waende slow sana.
Pia njia ilikuwa na vita na Mapingamizi mengi.

Japo miaka 40 ni mingi sana,ingefaa ata iwe 10 au 5
 
Hahha haimake sense sio?
Hizi dini zina stori za abunuasi sana ni sawa na waislam wanaambiwa wakijitoa muhanga wakifika peponi wanapewa mabikra 43
 
Kimsingi safari toka misri mpaka israeli ilipaswa kuchukua siku 19 tu ila mungu aliwazungusha njia ndefu ili awafundishe waissraeli namna ya kumcha Mungu.

Hakuna muisraeli aliyekuwa na miaka zaidi ya 19 wakati wa kuondoka Misri aliyeiona Isreal isipokuwa Joshua.
 
Ukisoma vizuri Biblia ni kwamba wana wa Israel baada ya kumuudhi Mungu kwa kuto kuamini kwao, Mungu akaamua kuwazungusha njia hiyo hiyo, kumbuka kuna maandiko Mungu alimwambia Musa kwamba atawaua wote kwasababu ya kuto kuamini kwao na Musa alimsihii Mungu kwamba asifanye hivyo kwasababu Wamisri watafikiri kwamba Mungu ameshindwa kuwafikisha kule aliko kua ameadhimia kuwafikisha so Mungu ilibidi afanye taratibu, yaani alisikiliza ushauri wa Musa (point to learn here, kama Mungu alimsikiliza mtumishi wake {binadamu} je viongozi wa kisiasa, kama rais au waziri) then tunasoma watu wazima pekee waliotoka Misri kuingia Kaanani/Israel ni 2 tu out of malaki yao nao ni Karebu na Yoshua; point yangu hapa ni hi, miaka hiyo yote walijikuta wanazunguka zunguka tu humo humo. Remember, watu hawa/Israel walifikaje Misri!? Walikwenda kwa miguu, kwanza was Yusufu/Joseph then miaka kadhaa baadae walikuja ndugu zake pamoja na mama zake na Masuria ya baba yake na huko ndiko waliko zaliana sana, hawakuchukua miaka mingi kufika hapo Misri. Nakumbuka hata Ibrahim (ambaye ndiye source ya hili taifa la Israel) nae aliwahi kimbilia kwenye hi nchi wakati Kaanani kuna njaa, nae hakuchukua miaka yote hiyo, kabla Yakobo na wanae hawajahamia Misri, watoto wake walifanya safari kama 2 hivi za kwenda na kurudi Misri wakitokea Kaanani, hawakuchukua muda wote huo, hapa walichukua muda mrefu kwasababu ya kuto kuamini kwao. Hope YEriko nitakua nimejibu kiasi changu
 
Mimi ninaona jibu lipo hapa,
Kutoka 13:17-18
17 Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri.
18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.
 
Misri ya Leo sio Misri ya enzi za Musa, pia haimaanishi kuwa walikuwa wakisafiri kwa miaka yote hiyo, Kuna process kuweza kuachiliwa kutoka mtumwa hadi kwa huru

The Bible is clear, walisafiri miaka 40. Hakuna maboresho.
Kwa nini walisafiri miaka yote hiyo? Nitakuja.
 
Ukisoma biblia tulia sana ndugu. Wana wa Israel walifika Sinai ndani ya siku tatu kutoka Misri (Imo kwenye maandiko) Pale walikaa miezi miwili hivi kujifunza kumjua Mungu pia kufanya agano na Mungu. Pia kumbuka ni mwendo wa siku 11 kutoka Kadeshi Narnea mpaka Horebu mpakani kabisa mwa Israel (imo kwenye maandiko) maana yake ni kwamba walifika Israel mapema sana.

Kilichowakwamisha kufika mapema ni sababu zifuatazo

Moja kumbuka walipotoka mlima Sinai waliambiwa watakuwa wanafuata wingu. Likitua mahala iwe siku mbili iwe mwezi iwe miaka wataendelea kuaka hapo mpaka siku likiinuka. (Soma kitabu cha hesabu) jinsi wana wa Israel walivyoondoka kwa majeshi yao kwa kufuata wingu.

Maana yake ni kwamba wakati mwingine wingu linaweza kutua sehemu ya maadui na ina bidi mpambane na maadui zenu mpaka siku wingu likinyanyuka, ama linaweza kutua sehemu yenye neema na kukaa siku mbili tu likaondoka.

Walifika mpakani mwa nchi za pembezeno mwa Israel ndani ya muda mfupi sana ila walifanya kitu kinaitwa fundamental Error. Wazee walimwambia Musa bila kumuuliza Mungu alituma atume mashujaa kadhaa kwenda kupeleleza nchi yaani Kaanani. Walipoenda wakakuta nchi kweli ni nzuri ardhi ina rutuba na ina matunda na wakakata baadhi ya matunda wakaleta kwa wazee matunnda. Pia katika upelelezi huo walikuta wana wa Anaki. Majitu makubwa sana yaliyopanda. Wakaogopa sana wakaleta kilio kambini watu wakavunjika moyo wakamsahau Mungu YAHWE aliewatoa katika nyumba ya utumwa kwa mkono ulionyooshwa. Basi neon la unabii likatoka kwa knywa cha Musa Kwamba kwa kuwa waeshindwa kumwamini Mungu wao, basi hawataingia katika nchi ya ahadi ispokuwa watoto wao na wale waliomuamini Mungu.

Walipopata habari hiyo wakaamua kwenda kupigana ili wapite kwa nguvu maana wananchi wa maeneo yale waliwazuia kupita.

Musa akawaambia wasipigane kwa maana Mungu hayupo pamoja nao. Waliopokwenda jaribu kupigana wakapigwa wakakimbizwa mpaka mbali.

Basi Mungu alipowafukuza aliwarudisha jangwani akawa anawapitisha sehemu zenye maadui na hatari nyingi ikiwa ni pamoja na sehemu zenye nyoka wa moto japo hakuwatupa kabisa ili kuepusha jina lake lisitukanwe.

Lakini pia jambo lingine Mungu aliwazungusha sehemu moja miaka na miaka. Mfano milima ya safu zamilima seiri waliizunguka kwa miaka mingi (mind you wao kazi yao ni kufuata wingu linapo elekea tu basi.)

Kumbuka mara ya kwanza waliingilia upande wa mbele huku chini ndo nchi ya Edomu lakini Mungu alipowafukuza aliwazungusha kwanza kama kurudi nyuma halafu akawazungushia kwenda kuingilia upande wa juu yaani kaskazini kurudi kusini ndo Yeriko . Na wakati mwingine aliwaweka nchi ya watu waa mataifa ili kuchunguza Imani yao lakini mwishowe walizoea maeneo yale wakaishia kwenda kuoa binti zao na kufundishwa kutumikia miungu mingine.

Baada ya miaka hiyo arobaini wakaanza kuwapiga wafalme waliokuwa wamefuga njia including Ogu mfalme wa Bashani.

Hizo ndo factors zilizosababisha wana wa Israel kusota jangwani kwa miaka arobaini.
 
Safari ya Wana wa Israel toka Misri hadi nchi ya ahadi walikua wanaongozwa na Mungu mwenyewe kupitia ishara ya wingu likisimama wanasimama hivyo hivyo hata likitembea nao wanatembea, Kizazi hiki kilimkufuru Mungu na adhabu aliyowapa ni wote kuangamia njiani hata Musa mwenyewe aliishia kuiona nchi ya ahadi ila hakufika wote waliotoka Misri waliishia jangwani.

Sijakuelewa hapa mkuu, Kwamba hakuna aliefika nchi ya ahadi
 
Kuna kitu lazima watu wajue kuhusu Numerology ya Bible ndio unaweza kuongea. 40 inaposemwa haimaanishi 1 mpaka 40 lazima kujua 40 ni nini?
Namba mara nyingine zina represent attributes na sio quantity ya numba zenyewe
 
HADITHI ZA KUFIKIRIKA
National discovery channel wanadocumentary huwaga wanaionesha ya ugunduzi wa vifaa vya kale baharini mahala ambapo waisraeli walivuka na farao akamezwa na bahari, pamoja na sehemu walizopita hawa jamaa,siku ukibahatika kuiona utajitukana kwa kauli yako uliyoitoa,jamaa hawabahatishi wale walichunguza na wanapata jibu kwa ushahidi wa macho na kisayansi,safari hyo ilikuwepo
 
Ukisoma vizuri Biblia ni kwamba wana wa Israel baada ya kumuudhi Mungu kwa kuto kuamini kwao, Mungu akaamua kuwazungusha njia hiyo hiyo, kumbuka kuna maandiko Mungu alimwambia Musa kwamba atawaua wote kwasababu ya kuto kuamini kwao na Musa alimsihii Mungu kwamba asifanye hivyo kwasababu Wamisri watafikiri kwamba Mungu ameshindwa kuwafikisha kule aliko kua ameadhimia kuwafikisha so Mungu ilibidi afanye taratibu, yaani alisikiliza ushauri wa Musa (point to learn here, kama Mungu alimsikiliza mtumishi wake {binadamu} je viongozi wa kisiasa, kama rais au waziri) then tunasoma watu wazima pekee waliotoka Misri kuingia Kaanani/Israel ni 2 tu out of malaki yao nao ni Karebu na Yoshua; point yangu hapa ni hi, miaka hiyo yote walijikuta wanazunguka zunguka tu humo humo. Remember, watu hawa/Israel walifikaje Misri!? Walikwenda kwa miguu, kwanza was Yusufu/Joseph then miaka kadhaa baadae walikuja ndugu zake pamoja na mama zake na Masuria ya baba yake na huko ndiko waliko zaliana sana, hawakuchukua miaka mingi kufika hapo Misri. Nakumbuka hata Ibrahim (ambaye ndiye source ya hili taifa la Israel) nae aliwahi kimbilia kwenye hi nchi wakati Kaanani kuna njaa, nae hakuchukua miaka yote hiyo, kabla Yakobo na wanae hawajahamia Misri, watoto wake walifanya safari kama 2 hivi za kwenda na kurudi Misri wakitokea Kaanani, hawakuchukua muda wote huo, hapa walichukua muda mrefu kwasababu ya kuto kuamini kwao. Hope YEriko nitakua nimejibu kiasi changu
Mimi ninaona jibu lipo hapa,
Kutoka 13:17-18
17 Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri.
18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.
Ukisoma biblia tulia sana ndugu. Wana wa Israel walifika Sinai ndani ya siku tatu kutoka Misri (Imo kwenye maandiko) Pale walikaa miezi miwili hivi kujifunza kumjua Mungu pia kufanya agano na Mungu. Pia kumbuka ni mwendo wa siku 11 kutoka Kadeshi Narnea mpaka Horebu mpakani kabisa mwa Israel (imo kwenye maandiko) maana yake ni kwamba walifika Israel mapema sana.

Kilichowakwamisha kufika mapema ni sababu zifuatazo

Moja kumbuka walipotoka mlima Sinai waliambiwa watakuwa wanafuata wingu. Likitua mahala iwe siku mbili iwe mwezi iwe miaka wataendelea kuaka hapo mpaka siku likiinuka. (Soma kitabu cha hesabu) jinsi wana wa Israel walivyoondoka kwa majeshi yao kwa kufuata wingu.

Maana yake ni kwamba wakati mwingine wingu linaweza kutua sehemu ya maadui na ina bidi mpambane na maadui zenu mpaka siku wingu likinyanyuka, ama linaweza kutua sehemu yenye neema na kukaa siku mbili tu likaondoka.

Walifika mpakani mwa nchi za pembezeno mwa Israel ndani ya muda mfupi sana ila walifanya kitu kinaitwa fundamental Error. Wazee walimwambia Musa bila kumuuliza Mungu alituma atume mashujaa kadhaa kwenda kupeleleza nchi yaani Kaanani. Walipoenda wakakuta nchi kweli ni nzuri ardhi ina rutuba na ina matunda na wakakata baadhi ya matunda wakaleta kwa wazee matunnda. Pia katika upelelezi huo walikuta wana wa Anaki. Majitu makubwa sana yaliyopanda. Wakaogopa sana wakaleta kilio kambini watu wakavunjika moyo wakamsahau Mungu YAHWE aliewatoa katika nyumba ya utumwa kwa mkono ulionyooshwa. Basi neon la unabii likatoka kwa knywa cha Musa Kwamba kwa kuwa waeshindwa kumwamini Mungu wao, basi hawataingia katika nchi ya ahadi ispokuwa watoto wao na wale waliomuamini Mungu.

Walipopata habari hiyo wakaamua kwenda kupigana ili wapite kwa nguvu maana wananchi wa maeneo yale waliwazuia kupita.

Musa akawaambia wasipigane kwa maana Mungu hayupo pamoja nao. Waliopokwenda jaribu kupigana wakapigwa wakakimbizwa mpaka mbali.

Basi Mungu alipowafukuza aliwarudisha jangwani akawa anawapitisha sehemu zenye maadui na hatari nyingi ikiwa ni pamoja na sehemu zenye nyoka wa moto japo hakuwatupa kabisa ili kuepusha jina lake lisitukanwe.

Lakini pia jambo lingine Mungu aliwazungusha sehemu moja miaka na miaka. Mfano milima ya safu zamilima seiri waliizunguka kwa miaka mingi (mind you wao kazi yao ni kufuata wingu linapo elekea tu basi.)

Kumbuka mara ya kwanza waliingilia upande wa mbele huku chini ndo nchi ya Edomu lakini Mungu alipowafukuza aliwazungusha kwanza kama kurudi nyuma halafu akawazungushia kwenda kuingilia upande wa juu yaani kaskazini kurudi kusini ndo Yeriko . Na wakati mwingine aliwaweka nchi ya watu waa mataifa ili kuchunguza Imani yao lakini mwishowe walizoea maeneo yale wakaishia kwenda kuoa binti zao na kufundishwa kutumikia miungu mingine.

Baada ya miaka hiyo arobaini wakaanza kuwapiga wafalme waliokuwa wamefuga njia including Ogu mfalme wa Bashani.

Hizo ndo factors zilizosababisha wana wa Israel kusota jangwani kwa miaka arobaini.
 
National discovery channel wanadocumentary huwaga wanaionesha ya ugunduzi wa vifaa vya kale baharini mahala ambapo waisraeli walivuka na farao akamezwa na bahari, pamoja na sehemu walizopita hawa jamaa,siku ukibahatika kuiona utajitukana kwa kauli yako uliyoitoa,jamaa hawabahatishi wale walichunguza na wanapata jibu kwa ushahidi wa macho na kisayansi,safari hyo ilikuwepo
Haya hao wachunguzi no miongoni mwa waliovumbua kwamba MTU mweusi alikuwa nyani.ukiwaona wape hongera.
 
ILE ILIKUA SHULE YA MUNGU KWA WANA WA ISRAEL SIO SAFARI PEKE YAKE NA NDIO MAANA MPAKA LEO TAIFA LA ISRAEL LIPO
 
Back
Top Bottom