Umebaini tofauti gani Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Samia unaotarajiwa kujengwa Arusha?

duuu ni juzi tu hapa nmetoka kununua mfuko wa cement kwa 17000 hiyo 23K ni kasi ya 5G.
nko mkoani
 
Ndio liwe ongezeko la bilioni mia mbili kwa nusu kazi ndugu yangu, bora tuendelee kuitwa wajinga lakini sio kuingizwa sipo aisee
 
Kwa kweli watuonee huruma hawa viongozi wetu raisi atufafanulie hizi tofauti maana haingii akilini
Hata anajua basi maskini ya Mungu. Yeye akipelekewa anatia sahihi tu huku akiambiwa ajiandae kwenda shopping ya abayah dubai kwa kisingizio cha kongamano uchwara.
 
Tuelimishane taratibu mbona ulipoachika hatukukunyanyapaa tuliishi na wewe Kwa upendo.
 
Wengi wa wachangiaji wa mada hatujawahi kujenga hata banda la kufugia kuku kwahiyo hatujui uhalisia wa gharama za ujenzi badala yake tumetanguliza ujuaji mwingi ambao hauna maana.
 
Tofauti kubwa mno, nusu ya idadi ya watu watakao kaa ongezeko la bilioni mia mbili, hata kama ilikua 200 sio hivyo isee!
Nondo, cement, mafuta, wages, urembo/nakshi, sehemu za huduma za ndani, thamani/faniture bei ya wakati huo na Sasa vinalingana?
Sikatai kuna weza kuwa na upigaji.
 
Pamoja na kwamba kuna vitu napinga kuhusu huu ujenzi ukianzia chaguo la mkoa, lakini tukumbuke pia hata uwanja wa Mkapa kulikuwa na upigaji mkubwa na kilichopangwa kujengwa hakikukamilika mpaka leo.
 
Mwaka 2007
Us dollar ilikuwa 1400
Leo ni zaidi ya 2500
Nadhani upigaji umo ila sio mkubwa kivile

Wacha tuibiwe japo kidogo
 
Angalia gharama zilizotumika kufanya marekebisho ya uwanja wa mkapa (bil 31 )
Kisha angalia gharama zilizotumika kurebisha uwanja wa Amaan Zanzibar kisha jiulize gharama za kujenga uwanja mpya zitakuwaje

Kwa kawaida kwenye mradi wowote Mkubwa wa serikali pesa lazima zipigwe. Hivyo hapo tunaweza kuwa tunaoigwa takribani 15-25% so tuwe wavumilivu
 
ni kweli gharama zimepanda, ila kiuhalisi thamani halisi ya uwanja wenye capacity ya 30k kwa standard zetu ni $60m, haizidi hapo!

kikawaida kiti kimoja kinagharimu $1000 (ndio simple calculation ya viwanja ilivyo), so at maximum uwanja wa 30k unaojengwa tanzania (nchi ambayo maeneo wazi ni mengi wala hulipi fidia) haikutakiwa kyzidi $60m
 
Hivi ni Ujenzi wa uwanja tu, ama pia itahusisha kujenga hayo majengo pembeni ya Uwanja!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…