Umeme uliokuwa unapelekwa mikoa ya kaskazini utapelekwa wapi baada ya kununua mwingine kutoka ETHIOPIA?

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
Mkulima analima mahindi. Baada ya kuvuna, anapata uvivu wa kupeleka mashineni yasagwe na kupata unga wa kula kwa kuona kwamba ni gharama kuyaosha na kuyaanika juani na baadae kuyasaga.

Anaamua kuyauza na kisha kwenda dukani kwa mangi kununua sembe.

Nauliza, umeme uliokuwa unapelekwa mikoa ya kaskazini, baada ya serikali kuamua kununua mwingine kutoka nje..

Umeme huo utapelekwa wapi?
Au ndio utakao uzwa nje na serikali hiihii?
Au tutalazimika kuzima mitambo kwakuwa tutakuwa na ziada ambayo haitumiki kokote?

Swali la mwisho. Kuna umeme wa ziada kwanini watanzania bado wanagharimikia umeme huo kwa bei ambayo uwezekano wa kupungua ungekuwepo lakini bado hamtaki kupunguza gharama?
ChoiceVariable
FRANCIS DA DON
Lord denning
 
Wazee wa data mtusaidie ni MW ngapi zilikuwa zinapelekwa mikoa hiyo na sasa kwakuwa serikali itanunua kutoka nje hizo megawatts zitaelekezwa wapi?
TANESCO leo usikimbie na kujikausha ulete majibu.

Kwakuwa january makamba umesamehewa na raisi n umewahi kuwa waziri wa nishati tunaomba uje ulete ufafanuzi. Maana ule alio utoa msigwa bado unaacha maswali memgi
 
Moderators swali.hili halijajibika kwemye ufafanuzi ulio tolewacna serikali. Msiunge mada.
 
Ndio tatizo la kuongozwa kisiasa zaidi kuliko kiweledi.
 
Hii mada inahitaji majibu ya kikubwa sio ya kichawa
 
Umeme huo utapelekwa wapi?
Kawavuruga watu huku Waziri anasema hivi kisha yeye anakuja anasema hivi Geson Msigwa anakuja anasema hivi VPM anakuja anasema hivi yaan kila mtu anaongea la kwake, ila yeye ndio kaongea ukweli kwamba hatuna umeme huo maana walishagonga saini siku ile wenyewe wanaita Summit nini sijui wakatia saini umeme hautuhusu tena akaona isiwe tabu tutanunua hata hapo Ethiopia na nyinyi mpate maana huku hatuna chetu tena kwa hio jiandaeni kisaikolojia
 
Kwenye hili serikali irudi mezani. Wazo la bwawa la nyerere ilikuwa kuongeza megawatts zitakaondoa tatizo la uzalishaji mdogo wa umeme nchini na kukidhi mahitaji ya nchi.

Leo tunazalisha umeme mwingi ambao nchi inataka kuuza nchi zingine lakini wakati huohuo inataka kununua tena. Haya ni maajabu.

Waswahili walisema kimfaacho mtu chake. Umeme kutoka Ethiopia hauwezi kuwa kutegemeka ninachoona bado tunapenda kuwa watumwa. Ethiopia wakipata crisis yoyote ikaathiri nishati ya umeme mikoa ya kaskazini yote itakuwa gizani. Kama wanataka umeme wa upepo toka Ethiopia kwa nini usizalishwe Singida, Dodoma na baadhi ya maeneo ya Manyara ukaenda huko kaskazini?

Huko kwingine mkitibuana tu wanawakatia umeme kuwakomoa hata kama kuna mikataba mliingia kudhibiti hali hizo
 
Kuna somo linaitwa Magazijuto kwa vile watanzania ni mazuzu kuelekea 2025 kesho mtasikia umeme mnanunua visiwa vya comoro
Na watapiga makofi kusherehekea na shangwe km zote, wala hawahoji kwanini wao ni kushangilia tu kila kitu wanachoambiwa hata km ni cha kipuuzi na cha kijinga makofi na shangwee km mazombi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…