Umeme ushakatika maeneo mengi muda huu, ulipo upo?

Ni uhayawani wa hali ya juu na umajinuni mkubwa kukata umeme usiku.
Umeipenda mwenyewe, chaguo lako milele, na uvimbe upasuke utajijua mwenyewe 😂🤣🤣😂. Kazi iendeleee
 
Wamekata hata hapa nilipo kwenye saa kumi kamili.
 
Hidaya anazingua 🤣🤣🤣😂
 
.
 
Bila aibu Waziri mkuu anatutangazia umeme unazalishwa Hadi umezidi,shame, huo umeme unazalishwa kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara.
 
Arusha Giza kali mno toka saa 8 lasoro hivi.
 
Oya sio kila kitu mnalalamika tu.kuna upepo mkaliii
 
Oya sio kila kitu mnalalamika tu.kuna upepo mkaliii
Naona kama ID inasadifu maandishi.

Upepo mkaliii ndio nini na unazimaje gridi?

Umeshawahi kusikia mji fulani huko duniani, haukuwahi kuona umeme umekatika kwa miaka 88? Ulikatika dk 2, ikatafutwa mara ya mwisho kutokea tukio hili ilikuwa lini!

Miaka 88. Wewe huku unatoa sababu kila leo;
  • Matengenezo
  • Maji
  • Miundombinu
  • Ukame
  • Capacity
  • Hitilafu

Zote hizo ni repetitive, ipi ambayo imeshughulikiwa kikamilifu ili isijirudie?
  • Imeshughulikiwaje?
  • Zinahitaji muda gani kutatuliwa moja kwa moja?
  • Uwezo na uwezekano wa kuzitokomeza kabisa upo?
 
Mi ndio naamka hapa sioni kitu kote kweusi tii..
 
Mkuu upepo Ni mkali Sana . Tusubiri upite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…