Umenunua kigari cha milioni 15 unakata bima comprehensive. Una akili sawa sawa wewe?

Watu na pesa zao ndugu
 
bora mimi niliyemkatia bima mchepuko wangu na kufunga sensors + bore gauge kwenye kitenesi chake.. naenjoy sana..
 
Mimi naona wewe ndio mwendawazimu
 
Mkuu hilo fanfa ndio likoje
 
Siku zote nabishana na wewe, nilijua wewe ni mzima
 
Bima ya nyumba haina mashtaka ila Bima ya gari ni lazima...
 
Mkuu hilo fanfa ndio likoje
We mgeni hapa mjini?
Ni sticker ya bima lakini inakuwa haipo kwenye system, zile sticker za bima zinaprintiwa na binadamu siyo malaika.

Ni kama vyeti feki tu, ukikiangalia kwa macho ni chenyewe ila ukienda kwenye mfumo hukioni.

Na wapo mabroker wamewapiga wateja wao kwa mafanfa hayahaya na umekata ofisini kabisa.
 
Bima unachokithamini.
Yaa hapa ndo mantiki ya bima ilipolala, hicho kitu umekipa thamani gani na ukikosa utapata hasara gani.......mfano kama gari imepata ajali kubwa na haifai hadi ununue gari jingine na hiyo pesa huna uwezo wa kuipata ndani ya miaka mitano, je, bora kucheza pata potea au utoe laki nne uwe na bima comprehensive.....akili kumkichwa.​
 
Namanyere [emoji1][emoji1]

Ndo upo uko Mkuu?
Namanyere ni kule mgharibi ya mbali Tanzania mkoa wa Rukwa/Katavi kama sijakosea, ni kilometres chache sana kutoka hapo una kuwa Katavi National Park. ( nimewahi kupita huko kipindi fulani katika harakati za kupambana na maisha) [emoji18][emoji120]
 
Sasa kama huna hela tukusaidieje yaani!
 
Nyie ndio ambao mkishapata ajali mnaanza kuwasumbua watu wa bima wawafanyie michongo gari zenu ziingizwe mlipwe wakat mmekata bima gar ishapata ajali
Na wanawaponza sana hao wafanyakazi
 
Wewe ndiyo mwamba Sasa. Nawashangaa Sana Hawa wenye vigari vya milioni 8, 10, 12, 15 wanahangaika kulipa comprehensive. Shubamiti!!
Labda baada ya Mwaka au miaka miwili wanavitia Moto au wanavitumbikiza mtoni,alafu wanadai bima iwalipe huwezi jua!! Mjini mipango!!
 
Ahsante. Mi sio mgeni ni vile siwezi jua kila kitu
 
Janja janja kibao yaani.

Wajanja wa mjini wanalipa comprehensive miaka 2 halafu wanasuka dili na wenye bima. Inaandaliwa ajali halafu mtu anaenda kuvuta mpunga gari mpya inanunuliwa. Wewe wa Namanyele unalipa mpaka mwisho.
Namanyele 😀😀 niliendaga 2016 pale St. Bakhita kuangalia kazi, nilikimbia bila kuaga... Aisee Tanzania ni kubwa sana inabidi tuigawanye tupate nchi kama 4 au 5,,, yaani kuna sehemu watu wanaishi utafikiri wako nchi jirani.
 
siyo kila kampuni ya bima inastahili wateja.
 
Hao mazinjathropus walikuwa hawajengi vyoo,kwa hiyo hapo unatusaidiaje,tusijenge vyoo tujisaidie vichakani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…