Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Mimi niko Dar mwaka wa 8 sasa ni government employee . Sasa unataka niache kazi ya uhakika nikalime?
Nikitaka kulima huwa nalima mazao ya msimu Njombe viazi mviringo.
We unasemea njombe ya wap?ambayo viazi ni vya msimu saivi kuna kipalila au vya kumwagilia vutoka ivo mvua ina anza yani kwa mwaka unalima mara tatu.
 
Tembea uende ukajionee siyo habari za kuambiwa ni habari za kushuhudia
Hayo maeneo kama Njombe yote nimekwisha zurura, Kanda ya Ziwa yote mpaka ndani ndani kule Mpanda Mlowoka achana na hapo Buseresere au Hungumalwa.

Sio kweli kwamba Vijana wengi wametoboa.

Na kama ingekuwa rahisi unadhani kwa nini watu hukimbilia miji mikubwa?
 
Watu wenye maisha magumu wapo Dar tu acheni mawazo mgando mi nimeishi Morogoro ndani ndani maisha ni magumu nikaja kuishi Dodoma still hali ni mbaya so kuhama sehemu hakuwezi kukufanya ukawa big boss
Dar hakuna maisha magumu maana kila kitu kinapatikana. Huko mikoani maji ya 250 ndo wanauziwa 500
Ya 500 Dar mikoa yote 1000
 
Sahivi baadhi vijana wa daslam wameanzisha tabia ya kuwasifia wanaume wenzao wenye kipato tena wanawasifia kupita kiasi ili tu wapewe chochote wanajiita machawa mwisho nao wanalilia kuolewa
Kwa hiyo unaumia wakisifia?
 
Wazoefu wa kushika bomba kwenye daladala hawatakuelewa, wao kuamka saa 10 alfajiri kulala saa 6 usiku kama majinga.
Ila tukija huko mikoani tunawaona nyinyi ndio wenye maisha magumu mmechakaa kuliko sisi tulioko dar. Kwa iyo mnataka tuje huko tusote wote? Nyinyi limeni, Chomeni mikaa, vueni samaki sisi mtuache tushazoea maisha yetu.
 
Kijana wa daslam mafanikio kwake ni kumiliki samsung au iPhone, hata iwe ya laki 2 tu inatosha ilimrad isiwe tecno anaona katoboa, hapo anatafuta suruali fupi anavaa na viatu bila soksi, akipata earphone ya buku 3 na mewani nyeusi, akawa na account twitter basi ye hapo anaanza ukuda
Mbona wa mikoani mnanuka mikyundu na tumekaa kimya?
 
Mtu anakwambia eti Dar siyo kila kitu[emoji28]Binadamu[emoji119]...Haya tufanye Dar siyo kila kitu...

Ni wapi ndiyo kila kitu....

Mtu anakaa kuipondea Dar...anakuambia Dar hivi, Dar vile.... Mtu uzaliwe Mkoa huo huo kama hapa Dar, ukulie Dar,usome Dar.. utaanzaje kupapenda...Hata mimi ningeongea vya kuongea....

Mtu kama umejipata huko ulipo shukuru,na huyo aliyepo Dar muache na Dar yake..

Hata mimi mwenyewe siipendelei kivile[emoji28]
[emoji177][emoji177][emoji177][emoji7][emoji2935][emoji2935][emoji2935][emoji2969]
 
Back
Top Bottom