Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Wazoefu wa kushika bomba kwenye daladala hawatakuelewa, wao kuamka saa 10 alfajiri kulala saa 6 usiku kama majinga.
#kataadaladala

Daladala ni kero

Daladala ni mateso

Daladala ni unyanyasaji

Daladala ni umaskini

Daladala ni usafiri wa makapuku na watu wa hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unalala store (jiko, meza, sofa, feni, kitanda, pasi, bag la nguo na vitu vingine vyote ukifungua macho tu hivi hapa.
HII NI 99% ya wanaoanza kupambana tanzania haipigwi hatuna tofauti na vifaa vilivyopo stoo.
 
Mbeya ni Likijiji likubwa linalowaka taa usiku. Kuliko uishi mbeya bora uende Tabora
Hahaha acha utani bhana! Kuna sehemu kibao watu wametoba kuzidi hata Dar! Nenda Arusha na Mwanza hapo ndo utajua Dar ni kukariri maisha tu!
 
Upewe maua yako.
 
Huu ni ukweli mchungu sana, ardhi kwa ajili ya kilimo bado inapatikana kwa bei rahisi sana maeneo mengi ya nchi hii, naona maeneo mengine wakenya wanakuja kuchukua kwa njia ya uwekezaji sisi vijana tumejazana Dar,Arusha, na Mwanza tunashangilia na kubishana kuhusu Simba na Yanga.

Siku tukija kushtuka ardhi yote imeenda kwa wageni au inamilikiwa na wachache kisha vizazi vyetu vinaenda vibarua vya kupalilia dengu.
 
Kijana,

Kwa upande mwngne umenena vyema,

Kimsingi dar hapana utulivu kabisa,na uspokua mwangalifu unaweza kujikuta kipato chote kinishia kwenye matumiz na muda unazd kwenda .

Tuwe waangalifu mujini,yapo maisha mengne nje ya dar…yasiyo na mahangaiko mengi
 
INASIKITISHA SANA

Vijana wanahangaika na kuomba kazi zisizo na uhakika ajira portal hata buku mfukoni ni changamoto wanasubiria ajira ya 750k per month utakuta wengine huu mwaka wa tatu na zaidi yuko home anasubiri kuitwa kwenye interview nafasi 2 wanaofanyiwa interview 200

Wakati kuna kijana mwenzao sasa hivi anauza gunia moja la vitunguu 350,000 pale soko la Ilala hapo alilima heka 1 akatoa magunia 80

Tanzania ina vijana wa hovyo sana. Sekta ya kilimo na biashara ya mazao kuna fursa sana.

Tatizo vijana hawatembei, hawataki kujifunza kuhusu kilimo, wanachojua ni kwenda Kidimbwi na Kitambaa Cheupe

Kukodi shamba la ekari 1 maeneo yenye ardhi nzuri ya kilimo na baadhi unaweza kufanya hata irrigation hapa Tanzania ni 30,000 mpaka 70,000

Huwa nashangaa kijana anatoka mkoa wenye ardhi nzuri ya kilimo anakuja kuwa boda au machinga Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…