Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Braza alifika kijiji fulani kuuliza ardhi ya kulima huko chobingo akapewa upana wa hekari 5 urefu ajipimie mwenyewe.

Kama akilima hekari 40 na kupanda mikorosho baada ya miaka 5 atakuwa wapi?
Sasa ngoja apande hizo korosha zake baada ya kukomaa miaka 5 kisha wenyeji wamuombe hati miliki ya hiyo ardhi, ndio atajua kuwa hajui.
 
Ila watu wa dar wana roho ngumu sana mtu anaishi chumba kimoja, kuna kitanda, TV, sofa, vyombo mpaka mtungi wa gesi ndani daah! Usafiri sasa kama kwa wale wapanda daladala ndo kivumbi.. Dar kama huna hela ni pachungu sana.
Mtu anaishi mbagala, chanika, keko, manzese sasa hapo uko dar au uko uswenkeni.. Mtu anayeishi dar ni anayeishi ushuani tu ila hawa wengine ni bora waje tulime nao viazi huku kijijini
Wapi usipokuwa huna pesa ni tamu?? Maisha ya Dar yanareflect maisha ya miji mingi Tanzania tofauti ni ndogo hususani kwenye wingi wa watu ambapo ni added advantage kwa Dar maana Kampuni nyingi zinafunguliwa na fursa za biashara.
 
Ila watu wa dar wana roho ngumu sana mtu anaishi chumba kimoja, kuna kitanda, TV, sofa, vyombo mpaka mtungi wa gesi ndani daah! Usafiri sasa kama kwa wale wapanda daladala ndo kivumbi.. Dar kama huna hela ni pachungu sana.
Mtu anaishi mbagala, chanika, keko, manzese sasa hapo uko dar au uko uswenkeni.. Mtu anayeishi dar ni anayeishi ushuani tu ila hawa wengine ni bora waje tulime nao viazi huku kijijini
Kijana wa daslam mafanikio kwake ni kumiliki samsung au iPhone, hata iwe ya laki 2 tu inatosha ilimrad isiwe tecno anaona katoboa, hapo anatafuta suruali fupi anavaa na viatu bila soksi, akipata earphone ya buku 3 na mewani nyeusi, akawa na account twitter basi ye hapo anaanza ukuda
 
Kijana wa daslam mafanikio kwake ni kumiliki samsung au iPhone, hata iwe ya laki 2 tu inatosha ilimrad isiwe tecno anaona katoboa, hapo anavaa na viatu bila soksi, suruali fupi akipata earphone ya buku 3 na mewani nyeusi, akawa na account twitter basi ye hapo anaona katoboa
Watu wa dar wana magumu sana basi tu
 
Bila salamu nawapa ujumbe wenu enyi watu.

Mnaweza kusema kuwa najiinua au nawakashifu ila Mimi siko huko. Ni upendo tu.

Waarabu wanasema fikisha ujumbe hata kama ni mchungu.

Miaka 5 inatosha kabisa mtu kupima bahati ya maisha Dar es salaam au mahali popote.

Unaishi Dar miaka zaidi ya 5 huna nyumba, huna kiwanja, kula kwako ndo kule unatafuta leo ili ule leo, kila siku kwenye daladala wewe ukichomoa pesa kubwa basi buku 2.

Unalala store (jiko, meza, sofa, feni, kitanda, pasi, bag la nguo na vitu vingine vyote ukifungua macho tu hivi hapa.

Tanzania hii kuna mahali kama Liwale huko Lindi ukifika kijiji chochote ukiomba ardhi ya kujenga au kulima unapewa bure kabisa. Yet wewe uko dar hata hatua 4 za ardhi Chanika huna . Umerogwa shituka

Kijijini wenzako wenye bidii wanamiliki pikipiki, gari, guta, nyumba, duka nk.

Kijijini ni bidii zako tu. Mjini kuna pesa kuliko kijijini ila kama kila ukihangahika huzipati za kukukwamua ni vyema utafute chimbo kijijini.

Braza alifika kijiji fulani kuuliza ardhi ya kulima huko chobingo akapewa upana wa hekari 5 urefu ajipimie mwenyewe.

Kama akilima hekari 40 na kupanda mikorosho baada ya miaka 5 atakuwa wapi?

Nakuuliza wewe unayelipwa laki 2 na Mwindi.
Hili la kupewa ardhi umenikumbusha mbali, mwaka 2011 nilienda Songea nikakutana na rafiki yangu mtumishi wa Uma ananiambia anamiliki acre zaidi 1,000 nikimwangalia hali yake ya kifedha hailingani kabisa na hizo heka maana nilikuwa nafananisha na bei za ardhi mikoa ya kaskazini.

Kuja kugundua kumbe yule mshenzi alinunua kwa 25,000 tu kwa heka na zingine kama kumi alipewa bonus ya kukalibishwa kijijini.
 
Aliyekwambia Tanzania haina wenyewe ni nani ?

Muulize yule Rwegasira aliyelima Vanilla kule Bukoba sasa hivi anashangaa.., Au Yule Namungo Chemtwara unadhani alivyokuwa analalamikia bei ya Korosho ipo chini gharama zake za dawa n.k. hazijarudi unadhani anapenda malalamishi ?!!!!

Tatizo watu mmekuwa brainwashed Makosa ya watunga Sera kutunga Sera mbovu yanahamishiwa kwa wabangaizaji wanaojitahidi kila kukicha mkono uende kinywani (tena bila kulalamika) sasa hizi kejeli nadhani ndio zitawafanya waseme enough is enough....
 
Watu wa dar wana magumu sana basi tu
Huo ndo ukwel Maisha ya dar ya kwenye media na uhalisia ni vitu tofauti wanaoishi maisha mazuri ni wachache asilimia kubwa maisha ni magumu kwenda kuoga inabidi uende na shuka lako ndo utundike iwe mlango wa bafu, hao ndo wanatakiwa waondoke watafute fursa mikoani ili kupambana na umasikini.
 
Kijana wa daslam mafanikio kwake ni kumiliki samsung au iPhone, hata iwe ya laki 2 tu inatosha ilimrad isiwe tecno anaona katoboa, hapo anatafuta suruali fupi anavaa na viatu bila soksi, akipata earphone ya buku 3 na mewani nyeusi, akawa na account twitter basi ye hapo anaanza ukuda
Samsung na iphone zinamilikiwa na vijana wa dar tu? Mbona Tecno, infinix na Itel zinatumiwa na vijana wengi Dar es salaam..

Sasa kama wachumi wameligrade jiji la Dar kama jiji la kibiashara ambalo linaimpact kubwa kwenye uchumi wa Tanzania unaanza kudiss kwa kutumia maisha ya vijana wachache waliamua kuishi lifestyle zao.
 
Back
Top Bottom