Umeshawahi kuchoka kula nyama? Wapenda nyama tukutane hapa

Umeshawahi kuchoka kula nyama? Wapenda nyama tukutane hapa

amu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2012
Posts
16,132
Reaction score
31,149
Mimi napenda sana nyama hasa iwe ya ng'ombe, mbuzi kuku, samaki, kima. Ilimradi nyama tu iwe tamu na siwezi kuichoka.
Mfano nyama ya ng'ombe nitakunywa supu asubuhi mchana na ugali au wali na usiku na chochote.

Kesho yake nikala kavu, keshokutwa yake hivo hivo. Naweza kula kila siku ni kubadilisha mapishi tu. Mara mchemsho mara mchuzi mara kavu, mara nimechanganya na majani ya maboga nw nazj mara ya kuchoma.

Nisipokula nyama siku moja inakuwa kama mwezi hivi ninapata arosto kali mno.

Mfano kuku wa kienyeji huwa nina muanzia supu, nakuja mchana iwe pilau au biriani au wali mweupe kwa mchuzi usiku nitamkaanga tu nimtafune tafune.

Ninaweza letewa nyama ya kula wiki nzima sisi tukala siku 2. Sina familia kubwa nina mtoto mdogo tu na mie. Wakati nasoma nilikuwa prefect he he he siku ya nyama nina hot pot special ya kujaza nyama zangu.

[emoji12][emoji12][emoji12][emoji491][emoji490][emoji491]
 
Asee nyama mm Hadi naogopa mahari yangu nisije kuomba nyama [emoji23][emoji23]napenda sana, especially beef
 
  • Thanks
Reactions: amu
Suala sio kupenda au kutopenda..suala ni maamuzi ya mtu husika..kila kitu Mungu amepanga kinapotumika kitumike kwa kiasi..uwe unapenda au kukipendi..
Na si vizuri na hekima kusema Mimi napenda nyamaa..mwingine mayai..mwingine maziwa..mwingine kekiii..mwingine chaii..mwingine chocolate..mwingine pombe..mwingine sigara.nk

Hoja ni kuwa vinafaa kwa afya??kwa kiasi Gani??nakuomba sana fanya mazoezi ya kujitawala kwa kila kitu unachokipenda sana..wakati mwingine sio kupenda ni addiction fulani tuu.jitahidi utaweza.

Kama una familia ni hatari sana kuwazoesha hiyo life style..watashindwa kuishi na watu huko mbele..

Nilikuwa na mwenzangu wa dizaini hiyo niliongea nae na mazoezi ya kujitawala leo hataki kabisa nyama mpaka mnaweza gombana kila akila anasema anaisikia tumboni haiyeyuki.
 
Ahsante.
Huwa tunaiyeyusha na wine.
 
Nyama ni swala mtambuka 🤣🤣🤣 wanasemaga "Japo Ng'ombe mkubwa ila superstar kuku!"
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hivi hakuna madhara yoyote ya kiafya yanayotokana na kula sana nyama ?
 
Ulipotaja nyama,kwenye ulimwengu wa roho nimemuona mchawi mmoja kule akiwaza kitu
 
Back
Top Bottom