2024 nilipofukuzwa kazi, ilikuwa n sehemu ya ndoto yangu kutokana na nilichosomea, mbaya zaidi niliondolewa kwa kusemewa mambo ya uongo 😭
Mpaka sasa bado siko Sawa kiakili, Hua najaribu kujiweka sawa ila bado ni kitu kinachoniumiza mno
Dah, jaribu ku move on mzee baba, kubaliana na uhalisia mshikaji wangu, maisha hayakupi unachotaka.. yanakupa yanachotaka yenyewe..
WAtu wengi maishani kuna vitu vimetutokea, vikaturudisha nyuma vikatupoteza kwenye ramani, vikaacha mafonda na makovu mazito, ila unapona ukikubaliana na uhalisia...
Kipindi mie nasoma, nilikuwa najiona kabisa mimi ni engineer, kuanzia msingi mpaka O level.. ile mtu anakwama anakuletea pepa unamsolvia.. kininja. Vigumu kwao, vyepesi kwangu, namaliza O level ninapewa cheti cha mwanafunzi bora katika MATHEMATICS, PHYSICS, GEOGRAPHY, KISWAHILI NA ENGLISH..
Kimbembe kikaja A LEVEL baada ya kumtia mtu mimba, misukosuko ikaanzia hapo, stress zile shule siendi, kibaya zaidi mie shule maza wangu alikuwa hanifuatilii sababu ya yale matokeo yangu ya hmkuanzia primary, alikuwa na imani na mimi..
Aisee zile stress za mimba shule pakawa hapaendeki, HAPASOMEKI, end of the day pepa la six nilifanya hovyo, NIKAFELI, ile hamu ya kusoma ikakatika moja kwa moja, nikapaswa niende diploma kwa cheti cha 4m 4, mwaka ule nikagoma akili inagoma mimi sio wa kusoma DIPLOMA, hapo mtoto tayari kaishajulikana na home.. nikapiga mishe fulani, kidogo hali ikawa sawa kiuchumi kwangu mimi,
Mwaka uliofuta nikaingia DIT, nikawa napiga diploma ya Telecom, semester ya kwanza fresh, ya pili nikaanza kujisikia unyonge, mie niko diploma mwaka wa kwanza wenzangu wa A LEVEL wapo degree mwaka wa 2, wakat wale wa shule ya msingi ni mwaka wa 3, pale 4m 1 nilizingua nikampiga ticha, nikaenda kuanza form 1 upyaa.. ile ikawa inanisumbua saana akilini, nasoma diploma na vitoto vidogo mnoo, nilikuwa na mwanangu mmoja mpemba, kidogo yeye umri ulikuwa umesogea, ndio alikuwa ananiletea sana maswali ya namba namchapia ngoma, alitokea nikubali sana, enzi hizo nasikiliza sana ngoma za 2pac, tunachapa ngoma, huku tunasikiliza ngoma za pac, lupe fiasco, naughty by nature, weezy..
Siku namwambia nina drop vhuo jamaa hakukubaliana na uhalisia, alijitahidi sana kunishauri lakini wapi..
Nikaacha chuo nikarudi mtaani kusaka pesa, aisee acha kabisa hali ikawa tata, kibaya zaidi nje ya mfumo miaka inaenda haraka, mie sijajipata wenzang wameua diploma, wengine wamekula ajira, jamaa yangu akaunga., anamaliza degree mie ndio kwa mbaali najipata pata..
Kibaya zaidi sasa ile hali ya mimi kutokumaliza shule, kutokuwa engineer, kutokufikia malengo.. hali ilikuwa inaniumiza sana.
Usiku nalala, naota nipo class, nimezungukwa na watu nawasolvia, mara naingia kwenye pepa, napiga pepa naiona hii rahisi kabisa, mara nipo shule ya msingi, ilikuwa asubuhi nawafanyia masahihisho ya pepa ya namba kila j3.. aisee ndoto zilinitesa zile ni miaka hii ndio zimepungua sana, miezi 6 ama 7 sioti chochote..
Na ndio sasa hivi kidooogo naona u ahueni wa maisha mzee, japo sijajipata kiviiile, ila 30k, 50, 100k tu nazipata pata daily..
Kuna kipindi nikapata uteja wa kubeti, aisee acha kabisa, kidogo nichizike.. kila senti ninayopata naipitisha kwenye betting, hela izae hela kuna muda nakula ila vipigo vilikuwa vingi, unaoata milioni paaaaap.. siku 1 au 2 huna, stress zake nahisi ni bora umfumanie mkeo anapigwa pumbu kuliko ile.
Mbaya zaidi, nilikuwa nina kipaji kikubwa sana ha kucheza mpira ila niliacha sababu ya shule, kipindi hiko naona mpira haulipi, wakati maisha yananigeuka nikakumbuka nina kipaji cha boli, kwanini nisipambanie..
At 25, 26 hivi
Nikarudi uwanjani sio kufanya mazoezi ni kusaka maisha aloo, kwamba mpira ndio ulete ugali, ndondo za kutosha huku nasaka team, uzuri washkaji niliochrza nao utotoni walikuwa wanajua uwezo wangu, simu zikawa zinaita, ndondo naenda kukipiga, aise mwaka huo huo, nikapata majeraha ya nyama za paja.. napona pona, narudi uwanjani goti, hili ndio nikaacha kabisaa, hospitali wakaniambi ni upasuaji tu, acha kabisa mzee ni stress juu ya stress, nikabwaga manyanga.. siku hizi imebaki nacheza mpira wa kifaza, mazoezi ya kupashia shahawa joto,
Nishota sana nipo uwanjani napiga pasi zangu, nakusanya kijiji nafanya mabalaa yangu.. lakini zile za shule ndio zilinitesa zaidi
Kipindi hiko arsenal mbovuuuuùu, Nikaanzishaga msemo
"Kama kubeti na arsenal haviniui, basi stress za mapenzi haziwezi niua kamwe
Natumai siku 1 nitafikia lengo.
So i can feel you mzee, usikate tamaa, potezea njia hiyo, njia zipo nyingi unaweza fanya kingine na ukatoboa.
Mubaliana na uhalisia, maisha yaendelee la sivyo utazua magonjwa mengine makubwa mnoooo