Umeshawahi kukata tamaa ya maisha? Ipi ilikuwa sababu

Umeshawahi kukata tamaa ya maisha? Ipi ilikuwa sababu

Pole sana mkuu,

Mimi nilivyoona wabongo wengi hawaaminiki na hawana uaminifu,nikaona hapa nitachelewa,nikatimkia ughaibuni kama wewe na sijawahi kurudi tena huko coz nimesha settle life huku tayari.

Mkuu wabongo wanaongoza dunia kwa sadism, tunafurahia sana kuona wengine wanaumia, tunashehekea kabisa, na kuua ndoto za wengine kwa namna zote, kimwili na kiroho!
 
Mkuu wabongo wanaongoza dunia kwa sadism, tunafurahia sana kuona wengine wanaumia, tunashehekea kabisa, na kuua ndoto za wengine kwa namna zote, kimwili na kiroho!
Upo sahihi kabisa Kaka,
Unajua sometimes kuna vitu vingine ukiwa Bongo unaviona ni vya kawaida tu,ila ukitoka nje ndio unakuja kutambua,
Mfano watu wanapigana vikumbo njiani bila hata kumwambia mwezake sorry,ni kama limekua jambo la kawaida tu.
😀
 
Hatuna uungwana kabisa yani, hata basic ethics tu za kibinadamu hatuna, ukitoka ndio unakuja kujua tunaishi kama wanyamapori tu tofauti yetu na wao ni kwamba sisi tuna lugha tu ya kuwasiliana baaasi!, Ndio maana mtu anaweza kuua tu mtu mwingine na anaona kawaida tu wala hajutii au dhamira kumsuta
 
Mkuu move on usiendelee kuweka akili sehemu hauhitajiki.... Dunia hii haina huruma na watu sio wema....

Back then around 2017 nilikua na kazi fresh tu akaja jamaa ambaye ni contractor mwingine ambaye tunafanya kazi sawa wakani approach wakapandisha dau. Nilipiga hesabu na nilipo mishahara ilikua ni mpaka miezi 3 ndio unalipwa nikasepa.

Nikasaini contract wakaniwekea kipengele cha probation 3 month. Nikachapa kazi kwa uaminifu mkubwa kumbe wadau hawapendi. Imefika mwisho wa probation nashangaa nakuwa terminated.

Ingawa nilipigwa na butwaa ila sikuuliza sababu wala sikulalamika ila baadaye ndio nikaambiwa wana walipiga dili wakasingizia kwa boss ni wewe na mia sikula wala kujua hiyo dili.

Nikala buyu nikasepa nilikula msoto 2017-2019 hatari sana. Plus wakati nipo home dogo mmoja akapindua gari yangu ikawa right off halafu sina bima kubwa (story ya siku nyingine nilitokaje hapa)......

Nilifikia kipindi sina mia mtoto yupo shule yani nilikuwa namkopa mpaka housegirl wetu, mama watoto alikua akipata buku 10 ananisukumizia nikapate jibapa nitoe mawazo.

Niliuza mpaka mihogo kudadeki ila ile ya kishua buku buku na mishikaki.

Ila niliapa wale jamaa sitafanya nao kazi tena hata iwaje. And karma is a good bitch anakulipa kadri ya matendo yako. Ile kampuni walifitiana tena mpaka ikaja kufa after only 2 years toka wanifitini...

Back to me 2020 nikaamua kubadili fani ya engineering nikahama field na kuingia field nyingine ya engineering on the same sector nikachapa cv upya nikapata dili temporary nilikula msoto pale mwanzo nilikuwa napiga msuli usiku asubuhi naingia job wanaona expert si ndio huyu. Kumbe msuli usiku asubuhi kazini baadae nikapelekwa field nikanyoosha project. Nilifanya miezi mitatu mkataba ukaisha.

Nikaapply kazi kwingine nikapata nmekaa pale mwezi mmoja naona mapicha tu naingia ofsini sipewi kazi nashangaa tu mwezi wa kwanza umeisha sioni mshahara. Wa pili hola naambiwa sijui mifumo sijui nini. Nikawaambia sikilizeni mi ngoja nirudi kitaa. Kumbe nilivyoajiriwa kuna boss alikua na mtu wake anataka amweke nafasi yangu. Akawa aapprove mishahara yangu. Nilivyosepa tu mtu akawekwa pale.

Nikasota miezi kama miwili boss mmoja pale akaniita akanipa dili la nje... From there the rest ikawa history.... Nikaanza upya nikachapa kazi mpaka yule mshua aliyenichomoa akaona noma.

Kilichoendelea yule boss akaja kugombana na share holder wenzake wakagawanya kampuni ile kampuni yake ikawa hoe hae. Ile niliyobaki tunadunda mpaka sasa na kuna vihaki haki nikapewa pale viasilimia flani nasukuma gurudumu level za juu....

So mangi achana na kusikitika kaza moyo songa mbele haya ndio maisha duniani hatujaja kutia huruma ni kukaza nginja nginja....

Ukikata tamaa na kutia huruma kuna fala ni advantage kwake..

Ukijiua ni kumpa funza chakula cha bure. Tunakomaa hapa hapa duniani.

Mimi ukinitendea ubaya naachana na wewe sihangaiki sikusumbui nasonga yatakayokupata ni kadri ya matendo yako.

Kuna demu nilimpenda 2007 huko fala yule kuna siku ananitumia message kuwa hanipendi after 3 yrs ni alikua anapretend... nikateseka ila siku niliamka nikaenda baharini nikapiga ukunga na kelele pale mpaka stress zangu zikaisha nikaapa kwa majina yote. Yule mpuuzi mpaka leo haolewi wala hazai. Mwaka jana ananitafuta nmsamehe aendelee na maisha yake after fucken 18yrs....

Ngoja nisikumbuke haya mambo.
Hii imenifunza….Naamka sasa
 
Ukisoma posts zote kwa huu uzi utaona kila mtu hapa alitaka kukata tamaa kwa sababu ya kuumizwa na mtu mwingine tazama dada yetu Joanah aliyeanzisha uzi hadi wa mwisho kbs hamna aliyekutana na tukio natural, ni watu tu waliotaka aumie na wakamuumiza!
Huyo Joanah alivamia mapenzi akiwa bado mdogo ndio maana,
Unaweza kukuta sasa hivi yeye ndio anawaumiza watu kwa hayo hayo mapenzi.

😀
 
Huyo Joanah alivamia mapenzi akiwa bado mdogo ndio maana,
Unaweza kukuta sasa hivi yeye ndio anawaumiza watu kwa hayo hayo mapenzi.

😀

Aliumizwa lakini ndio cha msingi, unakuta aliyemuumiza alikuwa mkubwa kwake na kibinadamu alikua anamuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi, tunasema wanawake wakorofi lakini ukitazama utakuta wamepitishwa njia rough sana tangu wakiwa wasichana na hatimaye wanakuwa na roho zilizokufa ganzi yani!

Kibongobongo unaweza kumtafuta msichana mdogo tu na ndoto zake ukamdanganya na ukamuwin kumbe wewe akilini kwako humaanishi unachoongea naye umeplan "kuonja" tu then unatembea unafikiri huyo binti anaumia kiasi gani, na trust yake inakuwaje kwa mwanaume mwingine atakayekuja?
 
Mimi nimekata tamaa baada ya kujua mke wangu alikuwa ana mchepuko chuoni kwao na wameishi kama mume na mke mda wote walipo kuwa wanasoma japo ni inshu iliyo tokea miaka mitatu imepita ila mimi nimejua juzi wakati namfungulia akaunti ya Facebook aliyo kuwa anatumia wakati huo yupo chuo ndiyo nikagundua mesenja za mapenzi nikaamua kuomba ushauri jamiiforium nikaishia kubezwa
 
Kwani si mapenzi yana-run dunia 😂
 
Huyo Joanah alivamia mapenzi akiwa bado mdogo ndio maana,
Unaweza kukuta sasa hivi yeye ndio anawaumiza watu kwa hayo hayo mapenzi.

😀

Siwezi kuumiza mtu kwenye mapenzi labda aamue yeye tu kujiumiza 😁

Na wakati ule ungenikuta sasa ningelichukulia kwa namna ya kawaida sana 🤦‍♀️
 
Aliumizwa lakini ndio cha msingi, unakuta aliyemuumiza alikuwa mkubwa kwake na kibinadamu alikua anamuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi, tunasema wanawake wakorofi lakini ukitazama utakuta wamepitishwa njia rough sana tangu wakiwa wasichana na hatimaye wanakuwa na roho zilizokufa ganzi yani!

Kibongobongo unaweza kumtafuta msichana mdogo tu na ndoto zake ukamdanganya na ukamuwin kumbe wewe akilini kwako humaanishi unachoongea naye umeplan "kuonja" tu then unatembea unafikiri huyo binti anaumia kiasi gani, na trust yake inakuwaje kwa mwanaume mwingine atakayekuja?

Alikuwa kanizidi mwaka mmoja tuuu na miezi kadhaa
Nafikiri maumivu yalitokana na kwamba alikuwa mtu wangu wa kwanza,nilimpenda kweli kweli na sikuwa na mtu wa pembeni wa kunifariji wakati yeye ananiacha
 
Mimi nimekata tamaa baada ya kujua mke wangu alikuwa ana mchepuko chuoni kwao na wameishi kama mume na mke mda wote walipo kuwa wanasoma japo ni inshu iliyo tokea miaka mitatu imepita ila mimi nimejua juzi wakati namfungulia akaunti ya Facebook aliyo kuwa anatumia wakati huo yupo chuo ndiyo nikagundua mesenja za mapenzi nikaamua kuomba ushauri jamiiforium nikaishia kubezwa
Daah nimecheka!!
Kinachokuuma ni mkeo alishawahi kuolewa,kwamba wewe ni mume wake wa pili 😂
 
Back
Top Bottom