Umeshawahi kupiga One katika levo yoyote ya elimu? Tukutane hapa

Umeshawahi kupiga One katika levo yoyote ya elimu? Tukutane hapa

Nilibahatika kusoma shule kongwe, ila zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalum zilizitamani sana ila sikubahatika.

Katika familia niliyokulia mabroo 2 walienda Tobora na Mzumbe, walini inspire sana, ila uwezo ulikuwa mdogo.

Madogo 2 wa mwisho ambao walisapotiwa na hao 2 hapo juu, wao walibahatika kuchagiliwa Ilboru na Kibaha, lakini kwao haikuwa jambo la kushangaza kwani ule maarufu wa vipaji maalumu ulikuwa umezoeleka na kuyeyuka ikawa jambo la kawaida.

Binafsi nilipopata matokeo enzi hizo wanaita kupass ilikuwa yanatoka pamoja na shule uliyochagulia, nikawa nimechaguliwa hiyo shule kongwe ya bweni, nilifurahi sana sikupata usingizi siku hiyo,nilikuwa nawaza na kuvuta picha ya mazingira nitakayoyakuta pamoja na maisha ya bweni kwa ujumla.

Huu mzuka aliwahi kuuelezea Infantry Soldier
Hahahahaaa, yes brother upo sahihi, niliwahi kuandika mada kama hii miezi kadhaa huko nyuma.
 
Mie kuna mtu namjua ana Phd nw...ila ana maisha ya hovyo bodaboda ana uafadhari...!nadhan wasomi wetu kuna sehemu wanakosea
Huyo ni mmoja kati ya 200 wenye Phd. Kama mwarabu mmoja ni gaidi, hauwezi ukasema waarabu wote ni magaidi.

Jaribu kukusanya watu 1,000 randomly wenye maisha mazuri Tanzania kisha uchambue viwango vyao vya elimu ndio utagundua kuwa kusoma sana ni raha.
 
Na wanyantuzu..masuala ya milion 600 hadu 1b kwao kugusa tu...ukiwaona hawajahi hata kuvaa tai ..🥵
Mwaka jana niliingia bureau de change fulani pale Kariakoo nikamkuta Msukuma mmoja amechenji tshs akaondoka na $200,000. Ungeweza kumdharau kwa jinsi alivyokuwa simple!
Huenda hata mlango wa darasa la sekondari haujui. Tusitishane na hizo division one!
 
Umejibu kisomi sana
Thanks. Mkuu, kuna watu walikuwa wakipewa ada wanafikisha shuleni ila wengine walikuwa wanaenda kuchezea kamari alafu leo wanaleta kejeli kwa wasomi.

Suala la msoto kwa msomi ni la muda tu, kwa maana pesa anayotengeneza kilaza aliyekuwa anacheza kamari, msomi anakuja kutengeneza mara 5 yake.

Elimu/shule haiongopi mzee baba.
 
O-level, nikapelekwa vipaji PCB,
Kwa mara ya kwanza nilijuta kufaulu kwa shughuli niliyokutana nayo kule.

Matokeo nayo yalivyotoka......😂😂😂😂.
Sitaki mazoea humu.

Anyway
Nasajili laini kwa alama za vidole,
Naunganisha Line za chuo,
Narudisha line zilizopotea,
Naweka liquid protector
Nabadilisha ringtones,
Nasafisha nyota,
Mkuu hii nimei-screen shot na naitumia sasa kama wallpaper ya simu yangu kwa sababu maalumu za kielimu na mafanikio.
 
Umaskini sio sababu ya kuto kusoma mkuu.. kuna watu wamesoma huku hali zao za kimaisha zikiwa duni kupita kiasi
Wapo watoto waliosoma wakitokea katika familia za kimasikini, lakini ni wachache sana. Labda ni watatu kati ya 100.
 
Nyie ndio design ya Magufuli akina Mpango kusoma kwenu kwa shida inapelekea kuwa na roho mbaya zaidi ya Jambazi.nawafahamu wengi sana waliosoma kwa namba yako baada ya kuwa viongozi yani ni roho mbaya.
I wish ungepata kunifahamu au japo kusikia kutoka kwa marafiki zangu,nadhani ungebadili mtazamo wako....ugumu wa maisha humjenga mtu kiakili na kumpa nidhamu ya maisha kwa wenye uelewa mzuri japo sio wote.
 
Back
Top Bottom