Nilibahatika kusoma shule kongwe, ila zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalum zilizitamani sana ila sikubahatika.
Katika familia niliyokulia mabroo 2 walienda Tobora na Mzumbe, walini inspire sana, ila uwezo ulikuwa mdogo.
Madogo 2 wa mwisho ambao walisapotiwa na hao 2 hapo juu, wao walibahatika kuchagiliwa Ilboru na Kibaha, lakini kwao haikuwa jambo la kushangaza kwani ule maarufu wa vipaji maalumu ulikuwa umezoeleka na kuyeyuka ikawa jambo la kawaida.
Binafsi nilipopata matokeo enzi hizo wanaita kupass ilikuwa yanatoka pamoja na shule uliyochagulia, nikawa nimechaguliwa hiyo shule kongwe ya bweni, nilifurahi sana sikupata usingizi siku hiyo,nilikuwa nawaza na kuvuta picha ya mazingira nitakayoyakuta pamoja na maisha ya bweni kwa ujumla.
Huu mzuka aliwahi kuuelezea
Infantry Soldier