shule ya msingi sikufaulu ,nikaenda shule za wazazi o level nikapata one ya 13 , A level nikapata one point 4 ( CBG) ,chuo nikamaliza na ufaulu mzuri tu.
Nikili tu kuna jamaa zangu tulifail pamoja wakaanza biashara ya kuuza samaki na wengine biashara za nguo na nafaka .nikili tu jamaa wako mbali sana kunizidi na wako na pesa nyingi .
Lakini sijutiii kwenda shule hawa jamaazangu hawajiamini kabisa katika maisha wana hofu sana na maisha
Ila pia wengi waliofail wanaishi maisha magumu sanaa kupitiliza
Mpango wangu lazima hii elimu niitendee haki ,lazima nibadili hizi " A" kuwa pesa na fursa kwangu na kwa wengine
Wito kwa wasomi " tupambane tuoneshe utofauti "