Umeshawahi kupiga One katika levo yoyote ya elimu? Tukutane hapa

Bonge la Point Mkuu..
 
Maisha yangu ya Elimu yalikuwa Kawaida.. sijatoka Familia ya Kisomi.. ila I was certainly fast learner.

Shule ya Msingi nilitandika A wastani.. sikuwahi tumia nguvu kabisa ati nasoma. Basi tu nilikuwa najua.

Olevel Nilivoingia ngeli ilinipa shida kiasi kwamba nikabase saana.. na Physics (Engineering Science) na Maths.. Kufika Form Four sikuwa nashikika.. nikatia Kijiti.. sikuwa wa kwanza kutokana na nature ya shule ila nilikuwa top 10.

I was proud ukizingatia akili za kitoto, Advance nikaenda PCM.. sikugusa Pindi hata kidogo yaani.. niliingia shule kichwa kichwa.. ila kwa kuwa I was curious nilikuwa na viconcept kadhaa.. niliipenda saana Physics na Namba.. ila mitihani nikawa sitoboi.. nikipata saaaana ni 50,

Chemistry nikipataa saana ni 42.. Namba ndo nilikuwa napiga hizi 80, 90 ilikuwa kawaida.. (si mnajua namba haihitaji akili nyingi.. mazoezi tu)

Kufika ile first semester ya form six nilikuwa sifai.. Darasani naogopwa hata na wale walioshiba Mapindi ya Mjini.. ujue hapo mie ni msuli yatimaa yaani.. concept unaanza nayo from zero Mpaka unaelewa.. kitu inaitwa Calculus nilikuwa sifai.. Mpaka namaliza shule nilishindwa integral moja tu katika maisha yangu ya Alevel nayo ni integral ya Root ya SinX ila baadaye nikaja gundua haina integral lazima uaply numerical.

Physics ndo kabisa.. nilikuwa sifai.. ila sikuwahi iamini Physics

Ujinga wa Physics bhana inakubadilikia saa yoyote, ila nikawa Mjanja, Topics zote zenye nature ya umeme kama Tonics,Tism na statics swali halichomoi.

Achana na Dimension, sjui simple harmonic mara circular, hizi zilikuwa easy..

Utata ni Projectile asee.. Hakuna Topic Ngumu ya Physics kama Projectile..

Finally nilitia Adabu Necta.. Kijiti nilitia ila Mpaka leo najuta kwanini Physics nipate B.. wakati nilikuwa naiona A.

Baada ya Hapo nikaenda Mlimani kupiga Civil..

Those were the days..

My take: Matokeo bhana yanakuwa exciting pale unapokuwa mwanafunzi.. shule ikiisha matokeo hayana umuhimu tena.. kwenye kazi hizi za CV ni rare saana.. unaweka matokeo, asilimia kubwa wanahitaji tu CV relevant na kazi husika.
 
Kumbe 1 ishafika point 18

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti hawajiamini.... Kuna watu wanao jiamini kuliko wenye pesa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana, shule zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalumu niliishia kuzisikia kwenye soga
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] katika familia yetu tumezaliwa watatu wote tumesoma shule kongwe mixer private

Mimi nimepiga technical school ,wengine wamepiga hizo special mmoja kagonga ya tabora mwingine ya moro
 

😂 😂 😂
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] katika familia yetu tumezaliwa watatu wote tumesoma shule kongwe mixer private

Mimi nimepiga technival school ,wengine wamepiga hizo special mmoja kagonga ya tabora mwingine ya moro
Nilibahatika kusoma shule kongwe, ila zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalum zilizitamani sana ila sikubahatika.

Katika familia niliyokulia mabroo 2 walienda Tobora na Mzumbe, walini inspire sana, ila uwezo ulikuwa mdogo.

Madogo 2 wa mwisho ambao walisapotiwa na hao 2 hapo juu, wao walibahatika kuchagiliwa Ilboru na Kibaha, lakini kwao haikuwa jambo la kushangaza kwani ule maarufu wa vipaji maalumu ulikuwa umezoeleka na kuyeyuka ikawa jambo la kawaida.

Binafsi nilipopata matokeo enzi hizo wanaita kupass ilikuwa yanatoka pamoja na shule uliyochagulia, nikawa nimechaguliwa hiyo shule kongwe ya bweni, nilifurahi sana sikupata usingizi siku hiyo,nilikuwa nawaza na kuvuta picha ya mazingira nitakayoyakuta pamoja na maisha ya bweni kwa ujumla.

Huu mzuka aliwahi kuuelezea Infantry Soldier
 
Hahahahahaaa, wee jamaa umenichekesha sana hadi machozi yamenitoka hapa.

Mziki wa PCB sio wa kitoto kabisa
 
Kuna utamu Fulani kusoma hizo shule kongwe

Juzi Kati nilienda shule moja kongwe iko pale Tanga mjini Ina advance tu aisee shule imekuwa Tamu balaa ukarabati wa Ile shule unaweza dhani Ni chuo [emoji15]

Staff office Kuna Hadi kiyoyozi na masofa ya ngozi huko njee ndio Usiseme .

Ni shule kongwe viongozi wengi maarfu wamesoma pale
 
Shule nyingi kongwe zilifanyiwa ukarabati kipindi cha mwendazake.

Mimi pia nilitembelea shule yangu ya Advance mwaka juzi nilikuta imekuwa nzuri sana baada ya ukarabati
 
Kuna watu wanaushambulia huu uzi utadhani kufaulu ni dhambi [emoji16][emoji16][emoji16]

Problem talk creates problems. Solution talk creates solutions

Ingependeza kama tungejikita zaidi kwenye kujadili nini kifanyike badala ya kujadili kila leo matokeo mabovu ya elimu yetu.
Je nini kifanyike? Watu wasisome? Na wewe unayeona elimu ni mbovu hutapeleka watoto wako shule? Hata mtoto wako Akipata ONE kali O level na A level hutampeleka chuo?

Na wengi wanasahau kwamba mtoto kutokwenda au kutofaulu darasani sio guarantee ya kufanikiwa kifedha. Kama ambavyo kufaulu darasani sio guarantee kufanikiwa kifedha

Anyway, O level one Ya 14 na A level one ya 6. A level Physics "A"[emoji16]
 
O- level nilifanikiwa kupata div. pointi 16. Huko mbele nikashuka. A level div. II, point 10. Chuo kikuu, GPA 4.1. Kazi iendelee....... na inaendelea.
 
Hongera mkuu banda la Phyz Advance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…