Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Bonge Boy Kivule hapo aliibiwa Pikipiki ikapelekwa Arusha baada SIKU kadhaa anapigiwa simu ,kaka we ndo bonge Boy tafadhali Kuna chalii wameiba Pikipiki wakapeleka Arusha wanaomba warudishe na faini unayotaka wewe
 
Aaaah bro tunaomba uendeleee mkuuu pliiiiiiiiiiz tunaomba.
Mkuu ni hbri ndefu na mimi cyo story taller mzuri kwa maana ya maandishi na mda wangu pia ni mchache, nilimuuliza yule Mganga (Bibi) kwa nini nitembee kwa miguu mpka vijiji vyote hivyo na hela ninayo? Aliniambia inabidi nitembee! Nitakapokamilisha zoezi la kulala kwa wale mabinti wawili gari gari itanichukua kutokea hpo mpka ninapoenda! Na wala sitadaiwa nauli! Na itakua ni gari ndogo! ------ LKN NIKITHUBUTU KUFANYA MAPENZI NA WALE MABINTI YOTE NITAYAKOSA!-PMJA NA SHIDA ILIYONIPELEKA SITAFANIKIWA!
 

angalia inbox yako
 
Huyo mganga yuko wapi na anaitwa nani
 
Duh...
 
🤣🤣🤣
 
mimi nina babu yangu na uzuri anajulikana sana sana viunga vya mwahako,mwakidila,bagamoyo na mchukuuni hata mwarongo alikotokea mama kimbo wanamjua sana sana ni maarufu

Kisa chenyewe, nina ndugu zagu arusha walikua wana jirani yao anaumwa maradhi ya kuchanganyikiwa, yan vikipanda ni wa kufunga kamba,bas sjui ilikuaje mana ilitokea tu nilimpigia kaka angummoja akanambia sista niko tanga ila niko ndani ndani maramba huku nikimaliza nitakucheki nije nyumbani tukaongea kidogo tukaagana hapo hakunambia kilichomleta tanga bila taarifa ni nini

bas sku ya pili yake akanipigia akaniambia wamemleta mtoto wa jiran yao kwa mganga lakini wapo muda karibu wiki ila hawaoni nafuu yoyote zaidi ya kupoteza pesa hapo wazo la huyo babu yangu halikunijia nikamueleza mama yangu juu ya mkasa wao mama ndio kunikumbusha akanambia kwa nini usiwapeleke kwa babu yako wakajaribu mimi sasa nikamwambia mama mh wasipofanikiwa si yatakua yale yale lakini moyo ukanisukuma wasaidie kuwapeleka

nikampigia kaka nikamwambia kam vipi waje mjini tufunge safar kwa huyo babu kweli walikuja tukaenda tukiwa mimi, kaka zangu wawili,mgonjwa na mama yake,lakini kabla hatujatoka nikampigia babu nikamuuliza kama yupo kuna watu wana shida akanambia nipo njoo tukaenda

tulimkuta nje akatukaribisha ndani tukaingia kilingeni kwake, nikawatambulisha then wakaanza kujieleza shida yao bas babu alichukua tu karatas nakalam akawa anamuangalia yule kijana anaandika akanikabidhi list akanambia hizi ni dawa nazitaka lakini utakayokosa nipigie nendeni maduka ya dawa za asili tena akanambia ziko ghali lakini kazitafteni hizo dawa , tukarudi nyumbani mimi na kaka zangu hao had ngamiani sokoni kuna duka maarufu kwa dawa za asili katika ile list kulikua na mbegu za bangi na dawa kama mbili ambazo wao hawana muuzaji akanambia hizi hatuna, palepale nikampigia babu kumpa mrejesho akanambia nunueni zilizopo hizo nyingine ntazitafuta tukanunua tusirudi nyumbani straight had kwake tukaziacha akasema njoni kesho mje chukua dawa zenu

hio siku jioni yake vikapanda ambapp kesho ndio tukachukue dawa kaka wa watu katoka barabarani ikapita carry akaipanda kwa nyuma, ifahamike huyu kaka ni mgeni, hajawah kufika tanga yeye wala mama yake, hajui anaenda wapi lakini kulikua na watu walimuona wakatupigia kelele yule mgeni wenu amepanda gar inaelekea barabara ya pangani ikabidi kaka zangu wachukue boda kuiwah wakaikuta njiani wakaipigia honi wakasimam wakamchukua mgonjwa wao wakamleta ikabidi afubgiwe chumbani, ni alikua anaongea usiku kucha ukilala ukiamka unamsikia anaongea anaitaja majina yake matatu kwa kurudia rudia kulipokucha baada ya chai tukabebana had kwa babu akapwa za kupaka,za kujifusha za kuoga za kunywa

alitumia mchana na jioni hio siku alilala vibaya mno na kule kwa babu mimi ndio nikawa nauliza tatizo nn babu akajibu huyu ana mtoto wa kijini kichwani sasa alivuta bangi na huyo jini hapatan nazo ndio anamletea hizo shida hakutaka hata mia moja alichojibu akasema akimaliza hizo dawa babu apewe taarifa kuna watu hawana ustaarabu tangu waondoke kurudi arusha had leo kimyaaaaa
 
Upuuuuizi.. Huyo unayemuona fundi mwenyewe hawezi kujisaidia atakusaidiaje zaidi ya kutumia ujinga wako kukushawishi au kukaanga samaki kwa mafuta yake?
 
Liwale bwana waganga wakikupenda wanakusaidia ila kama wakikupenda majini Yao wanakusahaulisha kabisaa usiende kusema ahsantee Ili wakutoe kafara ya damu
Yeah nilikua naona ajabu alipokuwa anatoa ushuhuda kuna watu aliwasaidia halafu wakafanikiwa na wasirudi kusema asante .
Hili ni kweli kabisa.
Nb wanaozama pm. Mimi niliacha haya mambo, nilifanya tu once. Ila sasa nimeomba toba. Hata hivyo ni siku nyingi na nilishapoteza kontakt na huyo bibi.
 
Watu wa Arusha na ustaarabu ni kushoto na kulia na kupitia hao watu waso na shukrani ndo maana waganga siku hzi wamekuja na gharama plus Uongo Uongo anakupa tibu nusu usipone

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

pm yako umefunga __naomba connection yahuyo babu
 
Ndo ilivyo Sio Kwa akili zao ila ni kama wanasahaulishwa ,kulikua na Mzee mmoja mtwara,alikua anauza genge akaenda ngende alipofika akaambiwa akifanikiwa apeleke ahsantee Kwa muda aliopangiwa,ikawa Kila akitaka aende basi anasahaulishwa nafsi inamuambia ataenda ataenda ,ila pale gengeni alikua anaingiza pesa nyingi sana Kwa siku ,akajenga nyumba ,akannua Pikipiki ,muda wa wale kumtoa kafara ulipofika Sasa akaja Simba siku hyo akanguruma pale akazunguka nyumba akaondoka,mara ya pili akaja nguruwe ,mara ya mwisho akaja nyoka mkubwa akazunguka akaondoka walikua wanakuja usiku
Mwisho akaanza kuumwa akienda hosp hamna kitu,akahangaika sana mwisho akaenda Kwa waganga wa mwisho akawaambia Ndugu zake Ndugu yenu ameenda ng'ende huyu hatapona wanamchukua wenyewe,akasema kweli ikabidi waende liwale kufika akaambiwa kachelewa tayari,akafa yule baba na Kila kitu kikafa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Aliyekuja kwenye PM yako imekula kwake. Ila una kipawa kizuri sana cha usimulizi na utungaji wa hadithi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…