Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Huyo mkali
 
Ilikuwa Ujiji. Nimepigika kinyama mimi na mwanangu Q. Ghafla mbele yangu naona bango la Uganga, kwa maelekezo hakukuwa mbali na pale. Tunafika tunapisha na wateja ( kama sikosei ni mtu na wakeze ).
Yule Mganga alikuwa ni mwanamke! Basi baada ya salam akaanza makeke yake, shida zetu akazipatia Mule mule toka mwanzo wa Safari yetu mpaka ile siku tunafika kwake! Shida ikawa moja tu! Anataka 40000, sasa nikajiuliza yaani huyu Bazazi ameona yoote lakini kashindwa kujua kama hatuna ata mia? Nikamwambia fresh Mmama we tufanyie kazi sisi tutakupa 60000 sio hiyo 40000, basi ile kainuka tu kuingia ndani kuchukua madubwana yake, mimi nikakusanya pesa 45000 zilikuwa pale kwenye ungo na kinokia Obama nikamwambia Q mwanangu hii nauli tusepe. Tukatokomea hivyo yaani mpaka Mwaloni. Tukauza kale kanokia 15000 jumla tukawa na 60, tukala 7000, tukalipia boti 6000 kwa kila mmoja. Kufika mbele mbele huko kuna kijiji kipo ndani ya Gombe, mida ya saa 1:30 ile Boti inazama, tunatumbukia kwenye lile ziwa, maji naanza kuyaona meusi mwanangu hajui kuogelea anakaba shingoni anaogopa kufa, hali inazidi kuwa tete kila nikijitahid anishike japo ukosi wa shati yule maaluni kakaza kabali......sitosahau. yule mama alitupiga kitu kizoto. Siiendelezi naishia hapa.
 
Ndugu sikia! Mim nlikuwa mshirikina najua vizuri haya mambo!
Mtalipa, tena Bora nimekupa alerts mapema ili wkt mnalipa ujue mnacholipia.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787]aseehh..malizia bwanaaa
 
Nilikua machimboni pande za ishokera hela nikaenda kwa mganga Bariadi nikifika vzr bila kupotea kwakua ramani Nilikua nayo, nikapokewa na mjukuu wa mganga. mganga ni Bibi kizee kbsa, nikaambiwa utaaguliwa mda ukifika! Kweli saa9 ucku nikaitwa mganga kapandisha mizimu yake! Bandugu yule Bibi ni kwere alinipatia tangia Hustle zangu mpka kufika machimboni!, mganga akaniambia kua cku nikikuaga hpa kwangu utatembea kwa miguu utavuka vijiji vi2, kijiji cha3 utaitwa na wadada wawili watakufananisha lkn ww uwakubalie watakupikia kuku na wali pia watakukaribisha kulala nao kitanda ki1 LKN USIFANYE NAO MAPENZI KBSA! mtihani ulianzia hpo ndugu zangu kwa leo niishie hpo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…