Vizuri na hongera mkuu!!!Nilikula bakora za hatari na adhabu ya kubeba mawe mikono juu kwa kosa la uzurulaji baada ya kutoroka wakati tuliingia makubaliano nibaki home maana wote waliondoka. Niliamua kutoroka ili nikaangalie Sinema ambayo nilikuwa tayari kwa lolote ila lazima niiangalie. Nilimchukia mother ila nilimuelewa baada ya kufaulu peke yangu Drs la Saba katikati ya watoto watukutu mtaani kwetu. Mkono wa chuma wa mama ni zawadi tosha maishani mwangu.
Duuh kumbe we ukipigwa unajikojolea [emoji40] [emoji40] [emoji40],,pole...Naanza na mimi!!!
Wakati niko darasa la tatu nilimuomba jirani yetu hela nikatumie shuleni akaniambia njoo kesho kabla hujaenda shule... Nyumbani tulishakatazwa kuombaomba hela kwa watu [emoji3] [emoji3] Sasa mimi kesho yake nikaaga nyumbani mapema kua naenda shule, nikapitia kwa jirani na kumsubiri anipe hela... Nimekaa kama nusu saa, ile nageuza shingo namuona mama yulee anapita... Akanichunia na kupita kimya kimya.
Nilivyorudi jioni... Nilidakwa na fimbo kuanzia getini... Mama yule alinichaaapa fimbo zilivyokatika akachukua ndala... mpaka nikajikojolea ...
Yaani milele sintasahau kike kipigo.
bora ulipelekwa boardingMimi nilikuwa Mtundu sana. Hii ilisababisha mpaka nikapelekwa shule ya boarding nikiwa na miaka minne pekee.
Siku moja ambayo mama na baba walinichangia ni siku ambapo nilienda kumtega mzee kipofu na kumwangusha. Nilitengeneza kamba alafu nikaitegesha njiani, mzee kipofu alipokuja anatembea na mkongojo wake nikainyanyua na kumuangusha. Nikabaki hapo pembeni nacheka kwa nguvu.
Asee, hiyo kipigo nilichopata sitakaa nisahau asee. Nilichapwa fimbo za kutosha maana nilishakuwa sugu kwenye mkanda.
Mungu anisamehe kwa niliyomtendea yule Mzee. Naamini hata huyo mzee kanisamehe pia, nilikwenda jumuomba msamaha kabla hajafariki, RIP.
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] aisee utoto una mengiNilikuwa mtundu sana nilipokuwa primary, kuna siku mzee alirudi na radio mpya, nikaifungua yote, nikashindwa kuifunga, na hii ilikuwa radio ya tatu kuiharibu. Sasa mzee aliporudi toka job alipa bakora nne za maana, na adhabu ikaendelea kwa wiki nzima kila akitoka job ni salam na fimbo moja then tunaendelea na mambo mengine.
Hahahaha!!!Duuh kumbe we ukipigwa unajikojolea [emoji40] [emoji40] [emoji40],,pole...
Sio mzaz tu ulikua unaoigwa na yyte aliekuzidi umri ukikosea tu chochote hata barabaran,,anakamata fimbo anakutandika na ukifika home kama kawa unakula vitasa vya ukwel,,
Umeqnza kupenda hela zamaaaaan std 3 hongera...(jokes [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji17] )
tehe tehe teheMe nilipomwambia nimeipigia kura CCM
ha ha ha nimecheka mpaka duhKaka yangu akiyeniachia ziwa alikua mtundu sana sana ,siku moja mama akiwa ameandaa chakula alituita ili tukapate mlo wa mchana,tulipofika akatuamuru tunawe nami nikaambiwa niombee chakula(ilikua zamu yangu)nikafumba macho nikaanza kuombea chakula kaka yangu akanifinya Mungu wangu!!nikafumbua macho tukatazamana huwezi amini wote tulicheka kwa sauti na sala ikakomea hapo,shetani mbaya sana jamani,mama alikasirika ,tulichapwa huku akitusimamia kula hakika sitasahau...hata hivyo jambo hilo limenisaidia sana kuheshimu ibada na sala namshukuru sana mama yangu...Apumzike kwa Amani mama.
jamani me niwe mkweli napenda watoto watundu .nadhani ningekupenda sanaMkuu, hiyo ya dynamo ilikuwa nikienda church nafungua baiskeli za watu.
Pole mkuu..same story tofauti yetu ni kidogo sana... Mie imenifanya nashindwa kujiamini, najitibu taratiibu..Mmh... mi nimechapwa hadi niliwachukia. Tena saingine kosa la mmoja tunapigwa wote watatu. Mdogoetu alikua mdogo.
Nilichokuja kugundua baadae ni kua wazazi walikua na stress mno.
Watu na ndugu walitamani maisha yetu ila hawakujua tu yanayoendelea. Migogoro yao ya ndoa ilitutesa sana sana.. SANA!
Mkisikia ukatili kwa watoto ndio ule. Kila siku Nilitamani kuihama ile nyumba. Nilivyomaliza six tu nikabahatisha kibarua cha hela nzuri halafu mkoa wa mbali. Nilishukuru
Mdogoangu anaenifatia ni wa kiume. Yeye alifaulu mkoani kuanza kidato cha kwanza ikawa sababu. Hakurudi tena hata likizo.
Nimepigwa hadi form 6 nachapwa vikosa vyenyewe sasa. Saingine kutoa Radio Tumaini kuweka radio One.
Yaani hivo ni vipigo heavyHahaha! Pole!!!
Kuzabua na kukong'otwa ndo inaeleze vizuri vipigo vingine.
Ulijikojolea? Nimewaza mbali sana. Mkojo!Naanza na mimi!!!
Wakati niko darasa la tatu nilimuomba jirani yetu hela nikatumie shuleni akaniambia njoo kesho kabla hujaenda shule... Nyumbani tulishakatazwa kuombaomba hela kwa watu [emoji3] [emoji3] Sasa mimi kesho yake nikaaga nyumbani mapema kua naenda shule, nikapitia kwa jirani na kumsubiri anipe hela... Nimekaa kama nusu saa, ile nageuza shingo namuona mama yulee anapita... Akanichunia na kupita kimya kimya.
Nilivyorudi jioni... Nilidakwa na fimbo kuanzia getini... Mama yule alinichaaapa fimbo zilivyokatika akachukua ndala... mpaka nikajikojolea ...
Yaani milele sintasahau kike kipigo.
mjeda huyoDah... Mie kosa nililofanya sisemi.....ila mshua alinipa kipondo cha kufa mtu... Magumi, mateke na vibao....kisha akanining'iniza mtini kichwa chini miguu juu siku2 bila kunywa wala kula [emoji13] [emoji13]
duh pole sana nimehuzunikaMmh... mi nimechapwa hadi niliwachukia. Tena saingine kosa la mmoja tunapigwa wote watatu. Mdogoetu alikua mdogo.