Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Nilikula bakora za hatari na adhabu ya kubeba mawe mikono juu kwa kosa la uzurulaji baada ya kutoroka wakati tuliingia makubaliano nibaki home maana wote waliondoka. Niliamua kutoroka ili nikaangalie Sinema ambayo nilikuwa tayari kwa lolote ila lazima niiangalie. Nilimchukia mother ila nilimuelewa baada ya kufaulu peke yangu Drs la Saba katikati ya watoto watukutu mtaani kwetu. Mkono wa chuma wa mama ni zawadi tosha maishani mwangu.
Vizuri na hongera mkuu!!!
 
Mdogo angu alikua anamsumbua mama akitaka kuchapwa!!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] atamchenga mpaka mama hasira zinaisha! Mama akaja na mbinu mpya, anategea yuko sebleni ndo anafunga milango ya kuingilia sebleni na funguo!!! Watakimbizana humo ndani... Dogo akitoka ana alama za fimbo mwili mzima [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Miaka hiyo ya 50's to 60's kulikuwa na kama kikapu kilichofumwa kwa kamba za manila,pia kilitumika kama fimbo,ilikuwa ikining'inizwa jikoni,kwa yeyote aliye haribu fimbo ilikwenda tunguliwa na kuanza kula micharazo,.......
sintasahau siku niliyotoka nyumbani bila kuaga na kwenda kuogelea mtoni nilikuwa na umri wa miaka 7 hivi.
Balaaaaaaaaaaah😱😱
 
Naanza na mimi!!!
Wakati niko darasa la tatu nilimuomba jirani yetu hela nikatumie shuleni akaniambia njoo kesho kabla hujaenda shule... Nyumbani tulishakatazwa kuombaomba hela kwa watu [emoji3] [emoji3] Sasa mimi kesho yake nikaaga nyumbani mapema kua naenda shule, nikapitia kwa jirani na kumsubiri anipe hela... Nimekaa kama nusu saa, ile nageuza shingo namuona mama yulee anapita... Akanichunia na kupita kimya kimya.
Nilivyorudi jioni... Nilidakwa na fimbo kuanzia getini... Mama yule alinichaaapa fimbo zilivyokatika akachukua ndala... mpaka nikajikojolea ...
Yaani milele sintasahau kike kipigo.
Duuh kumbe we ukipigwa unajikojolea [emoji40] [emoji40] [emoji40],,pole...

Sio mzaz tu ulikua unaoigwa na yyte aliekuzidi umri ukikosea tu chochote hata barabaran,,anakamata fimbo anakutandika na ukifika home kama kawa unakula vitasa vya ukwel,,

Umeqnza kupenda hela zamaaaaan std 3 hongera...(jokes [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji17] )
 
Mimi nilikuwa Mtundu sana. Hii ilisababisha mpaka nikapelekwa shule ya boarding nikiwa na miaka minne pekee.

Siku moja ambayo mama na baba walinichangia ni siku ambapo nilienda kumtega mzee kipofu na kumwangusha. Nilitengeneza kamba alafu nikaitegesha njiani, mzee kipofu alipokuja anatembea na mkongojo wake nikainyanyua na kumuangusha. Nikabaki hapo pembeni nacheka kwa nguvu.

Asee, hiyo kipigo nilichopata sitakaa nisahau asee. Nilichapwa fimbo za kutosha maana nilishakuwa sugu kwenye mkanda.

Mungu anisamehe kwa niliyomtendea yule Mzee. Naamini hata huyo mzee kanisamehe pia, nilikwenda jumuomba msamaha kabla hajafariki, RIP.
bora ulipelekwa boarding
 
Nilikuwa mtundu sana nilipokuwa primary, kuna siku mzee alirudi na radio mpya, nikaifungua yote, nikashindwa kuifunga, na hii ilikuwa radio ya tatu kuiharibu. Sasa mzee aliporudi toka job alipa bakora nne za maana, na adhabu ikaendelea kwa wiki nzima kila akitoka job ni salam na fimbo moja then tunaendelea na mambo mengine.
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] aisee utoto una mengi
 
Duuh kumbe we ukipigwa unajikojolea [emoji40] [emoji40] [emoji40],,pole...

Sio mzaz tu ulikua unaoigwa na yyte aliekuzidi umri ukikosea tu chochote hata barabaran,,anakamata fimbo anakutandika na ukifika home kama kawa unakula vitasa vya ukwel,,

Umeqnza kupenda hela zamaaaaan std 3 hongera...(jokes [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji17] )
Hahahaha!!!
 
Kaka yangu akiyeniachia ziwa alikua mtundu sana sana ,siku moja mama akiwa ameandaa chakula alituita ili tukapate mlo wa mchana,tulipofika akatuamuru tunawe nami nikaambiwa niombee chakula(ilikua zamu yangu)nikafumba macho nikaanza kuombea chakula kaka yangu akanifinya Mungu wangu!!nikafumbua macho tukatazamana huwezi amini wote tulicheka kwa sauti na sala ikakomea hapo,shetani mbaya sana jamani,mama alikasirika ,tulichapwa huku akitusimamia kula hakika sitasahau...hata hivyo jambo hilo limenisaidia sana kuheshimu ibada na sala namshukuru sana mama yangu...Apumzike kwa Amani mama.
ha ha ha nimecheka mpaka duh
 
Mmh... mi nimechapwa hadi niliwachukia. Tena saingine kosa la mmoja tunapigwa wote watatu. Mdogoetu alikua mdogo.
Nilichokuja kugundua baadae ni kua wazazi walikua na stress mno.
Watu na ndugu walitamani maisha yetu ila hawakujua tu yanayoendelea. Migogoro yao ya ndoa ilitutesa sana sana.. SANA!
Mkisikia ukatili kwa watoto ndio ule. Kila siku Nilitamani kuihama ile nyumba. Nilivyomaliza six tu nikabahatisha kibarua cha hela nzuri halafu mkoa wa mbali. Nilishukuru

Mdogoangu anaenifatia ni wa kiume. Yeye alifaulu mkoani kuanza kidato cha kwanza ikawa sababu. Hakurudi tena hata likizo.

Nimepigwa hadi form 6 nachapwa vikosa vyenyewe sasa. Saingine kutoa Radio Tumaini kuweka radio One.
Pole mkuu..same story tofauti yetu ni kidogo sana... Mie imenifanya nashindwa kujiamini, najitibu taratiibu..
 
Naanza na mimi!!!
Wakati niko darasa la tatu nilimuomba jirani yetu hela nikatumie shuleni akaniambia njoo kesho kabla hujaenda shule... Nyumbani tulishakatazwa kuombaomba hela kwa watu [emoji3] [emoji3] Sasa mimi kesho yake nikaaga nyumbani mapema kua naenda shule, nikapitia kwa jirani na kumsubiri anipe hela... Nimekaa kama nusu saa, ile nageuza shingo namuona mama yulee anapita... Akanichunia na kupita kimya kimya.
Nilivyorudi jioni... Nilidakwa na fimbo kuanzia getini... Mama yule alinichaaapa fimbo zilivyokatika akachukua ndala... mpaka nikajikojolea ...
Yaani milele sintasahau kike kipigo.
Ulijikojolea? Nimewaza mbali sana. Mkojo!
 
Dah... Mie kosa nililofanya sisemi.....ila mshua alinipa kipondo cha kufa mtu... Magumi, mateke na vibao....kisha akanining'iniza mtini kichwa chini miguu juu siku2 bila kunywa wala kula [emoji13] [emoji13]
mjeda huyo
 
Mmh... mi nimechapwa hadi niliwachukia. Tena saingine kosa la mmoja tunapigwa wote watatu. Mdogoetu alikua mdogo.
Nilichokuja kugundua baadae ni kua wazazi walikua na stress mno.
Watu na ndugu walitamani maisha yetu ila hawakujua tu yanayoendelea. Migogoro yao ya ndoa ilitutesa sana sana.. SANA!
Mkisikia ukatili kwa watoto ndio ule. Kila siku Nilitamani kuihama ile nyumba. Nilivyomaliza six tu nikabahatisha kibarua cha hela nzuri halafu mkoa wa mbali. Nilishukuru

Mdogoangu anaenifatia ni wa kiume. Yeye alifaulu mkoani kuanza kidato cha kwanza ikawa sababu. Hakurudi tena hata likizo.

Nimepigwa hadi form 6 nachapwa vikosa vyenyewe sasa. Saingine kutoa Radio Tumaini kuweka radio One.
duh pole sana nimehuzunika
 
Mimi nilipokuwa darasa la kwanza nilimtundika mimba mdada wa form 2. Aisee. Kile kipigo, hata kuhadithia siwezi!
 
nimepigwa na mama tabia ya kwenda kucheza kwa majirani tobo na wavulana na mpira wenyewe itakawa . pigwa mno mpaga nikampa mama a,k,a ya simba ........... mbaya zaidi wadogo zangu nao michezo wakaiga na mama hataki mtoto kwenda kwa jirani bila sababu .. tukawa tunapemana zamu ya kumchunga akitokea tu unasikia mtu ana sema huyo simbaaa wote tunarudi nyumbani unajifuta vumbi wewe mama anapiga sana aisee ..
 
Back
Top Bottom