Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

baba hajawai ila mama duuh, utaratibu ulikuwa saa kumi na mbili jioni kila mtu ndani na tena uwe umeaga unaenda wapi, kuna siku nikazidisha masaa, nilichapwa hata kula nilisamehe, eti hao marafiki unaoenda kwao lakini sisi hatuwaoni wakija hapa ni kina nani?
Wamama wote tuko hivyo
 
Mmh... mi nimechapwa hadi niliwachukia. Tena saingine kosa la mmoja tunapigwa wote watatu. Mdogoetu alikua mdogo.
Nilichokuja kugundua baadae ni kua wazazi walikua na stress mno.
Watu na ndugu walitamani maisha yetu ila hawakujua tu yanayoendelea. Migogoro yao ya ndoa ilitutesa sana sana.. SANA!
Mkisikia ukatili kwa watoto ndio ule. Kila siku Nilitamani kuihama ile nyumba. Nilivyomaliza six tu nikabahatisha kibarua cha hela nzuri halafu mkoa wa mbali. Nilishukuru

Mdogoangu anaenifatia ni wa kiume. Yeye alifaulu mkoani kuanza kidato cha kwanza ikawa sababu. Hakurudi tena hata likizo.

Nimepigwa hadi form 6 nachapwa vikosa vyenyewe sasa. Saingine kutoa Radio Tumaini kuweka radio One.
Pole mkuu Mungu akutie nguvu,wazazi ni wa kuwaombea saanaa huwa tunakufa na tai shingoni inatesa familia nzima
 
Sikuwahi kupigwa kipigo kidogo.
Vyote ni vipigo heavy si home kwa bi mkubwa sio shule.


Hata sijui niweke kipi ila vyote ni heavy. Mfano nani humu kapigwa na mama na fimbo ikiwa "wanchoma kumoyo"? Niliwahi pigwa na hio kitu nikiwa std 3 tena utosini. I almost fainted if only I wasn't a "nunda"
Poleeee
 
Mungu akutie nguvu ndugu yangu
Asante ndugu, nilishasamehe na mungu amweke mahali pema peponi, kipigo wanaohadithia huku bado sana, Unasahau ilipo soap dish unapigwa bila nguo[emoji24] uchi kabisa, Wao bia mwendo mdundo Nyumbani ugali na mchicha aisee!! Nawashukuru sana kunisomesha mana nahisi nisingestarabika. Nimejiahidi kutouvunja moyo Wa mwanangu awae yote na hata Wa pembeni.
 
Nilipigwa mara ya mwisho na baba nikiwa la tano.

Kaondoka zake mjini kaniambia nifanye kazi za nyumbani, nioshe vyombo na kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kuteka maji.

Kidume nikapiga chai nikaaenda misele ile narudi nakuta mzee kafika alikuwa na boot moja imeandikwa chini ya unyayo BASE basi bhna nikasalimia mzee na kuingia ndani.

Ile naingia ndani naona giza la ghafla kumbe milango imefungwa nipo na mzee ndani hakuna kazi imefanyika, stiki zikaanza za rejareja hadi shingoni.

Duh BASE ikanikalia shingoni nikapewa stiki za kutosha ili kujiokoa nikavunga nimezimia anapiga silii wala kutikisika.

Mzee anahisi ameua akafungua milango wee nilitoka nduki kama Hamorapa.
Uwiiiii BASE
 
Mama alikuwa master wa leather belt ass whooping,mdingi mpole so yeye alikuwa ni vifinyo tu.Kipigo cha mzazi shurti ulie na uonyeshe kuwa unaumia asa ww jifanye nunda.Uzuri wazazi wangu walikuwa hawachapi ovyo ovyo ni vile tu nlikuwa mtundu sana.walikuwa wanakuhesabia makosa tu ukifanya mara moja unakemewa tu ikifika mara ya tatu lazima uchezee kipondo cha kibabe.

Nakumbuka kichapo kikubwa nlichowahi chezea ilikuwa sababu ya kucheza msikitini wakati wa swala,ebana mzee aliniwamba balaa,tena fimbo nliambiwa nkachume mwenyewe.kuanzia siku hyo mpaka leo nikiingia msikitini nakuwa na utulivu wa ajabu(ushuiy).
 
Wazazi wana aina tafauti tafauti za uchapaji
-Kuna ile anakuchap huku anakusema na kukutajia kosa ulilolifanya alafu mwishowe anakuuliza "utarudia tena?" huku kichapo kinaendelea ukisema sirudii anauliza tena kwa msisitizo "UTARUDIA?"mpka aridhike na jibu lako ushachezea nyingi
>Aina nyengine ni ile unapigwa huku uko kwenye movement(freestyle),unachapwa mkwaju wa mguu ukishika mguu unalambwa ya mgongo,ukirudi nyuma unayo,ukienda mbela imo mara mnaanza kuzunguka kama mduara huku mikwaju inaendelea alimradi tu mko kwenye motion.
>Nyengine ni ile ya kimya kimya,yaani anayekuchapa haongei kitu na hataki unayechapwa ulie,unachapwa kiafsa,mara nyingi hiiq ni kwa wale wanaokaa nyumba za kupanga au mzazi asiependa ijulikane kama anakuadhibu
 
Daaa nakumbuk cku moja tumezngua mimi na kaka na dgo anaenifata,,,sas maza alivkua mtata akataft fimbo ote watatu, tukakimbia ,mimi kwa ujinga wangu hata kabla hasira hazijamuish bi mkubwa nikasema aaah ngja nirud kwan atanifanyej,,, mamaaaa!!!! nlikutana na jiwe usoni kiasi kwamba nikalal apoapo nilpokua huku damu zinamwagika usoni,,,ila damu ni nzito kuliko maji coz yy mama huyohuyo nd alini take care mpk nkarud kweny hali ya kawaida ,,,tangu cku ile mama akiwa amekasirka mimi nakaa mbaliiii yasije jirudia ya kipindi ichooo ,,,yote kwa yote nampenda sana mama yangu kunifundsh mengi
 
Hivi wazazi wa kipindi hiki wanapiga watoto kama zamani? Mimi nimepigwa ila kuna rafiki wakati tupo shule ya msingi alipigwa na mzee wake sijawahi kuona kipigo kile ingekuwa leo yule mzee jela ingemuhusu kabisa jamaa aliletwa shule hawezi kutembea amekatwa sikio, alama za visu mgongoni na bado akampiga mbele ya mwalimu mkuu walimu wakamuombea msamaha jamaa angekufa. Wakati mwingine wazazi wetu walitumia vibaya nguvu zao kutuabuse. Mada imenigusa mno
 
Hivi wazazi wa kipindi hiki wanapiga watoto kama zamani? Mimi nimepigwa ila kuna rafiki wakati tupo shule ya msingi alipigwa na mzee wake sijawahi kuona kipigo kile ingekuwa leo yule mzee jela ingemuhusu kabisa jamaa aliletwa shule hawezi kutembea amekatwa sikio, alama za visu mgongoni na bado akampiga mbele ya mwalimu mkuu walimu wakamuombea msamaha jamaa angekufa. Wakati mwingine wazazi wetu walitumia vibaya nguvu zao kutuabuse. Mada imenigusa mno
Wazazi wengine sijui wakoje wamelaaniwa[emoji19] [emoji19]
 
Back
Top Bottom