Umewahi kufika mikoa mingapi Tanzania na ipi uliipenda zaidi?

Umewahi kufika mikoa mingapi Tanzania na ipi uliipenda zaidi?

Mimi sijatembea sana mikoani kwasababu sina connection yoyote ile ya ndugu wanaoishi mikoani, nimezaliwa na kukulia Dar hata kusoma pia nimesoma hapahapa dar, Baba na mama wote wamezaliwa Dar, Baba amezaliwa gerezani k/koo na mama amezaliwa Msasani.
Ila nimetembelea na kufika mikoa kadhaa ikiwemo;
°Lindi
°Tanga
°Morogoro
°Iringa
°Arusha
°Mbeya
°Pwani
°Pamoja na nchi ya Zanzibar [emoji23]
 
View attachment 2705519
Je umewahi kusafiri mikoa mingap Tanzania na ipi uliipenda zaidi na ipi uliichukia zaidi?
Arusha
Mwanza
Daresalaam.

Nilipapenda zaidi dar es salaam kwasababu Kuna mzunguko mkubwa WA pesa , hivyo ni jiji zuri kwaajili ya biashara ,masoko yapo kwasababu ya wingi wa watu ....

Lakin pia napenda Hali ya hewa ya Joto ndiyo maana nilipapenda ...

Lakin daresalaam huwezi kukosa vibarua hatakama ulikuwa unafanya Kaz ikaishia njian kupata vibarua ni rahisi ...

Napenda Daresalaam ni jiji la kibiashara Yan pamechangamka Sanaa ,
na MZUNGUKO WA PESA NI MKUBWA .


Arusha Ni mji Wa Gharama Sanaa kuishi
Na Kuna baridi Sanaa
Lakin pia Arusha biashara unafanya strategical hauanzishi tu gafla gafla hivyo sipendelei Sanaa .

Mwanza ni pana Hali ya hewa nzuri lakin pia watu wake ni wakarimu mnoo , watu wenye Upendo Sanaa ,
Shida yake ni kwamba mzunguko Wa pesa ni mdogo Sanaa na pia hata kwenye swala la biashara hakujachangamka kabisa kabisa .... Hivyo sipapendelei Sana pia .
 
Walahi, sijafika mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Zanzibar tu.😁😁😁😁😁🤔 Ninaipenda Tanganyika yangu na sijawahi kuchukia mkoa wowote ule. Sasa, kwaavile haujauliza sababu zipi za kupenda au kuchukia, mikoa hiyo basi kwa hiari kabisa, nitaongezea la ziada; nilikutana na wanawake wazuri kila mkoa na mkoa mmoja wapo, ndipo nilipompata Cheusi dawa wangu🤗😍🥰
 
Back
Top Bottom