Umewahi kukataliwa hadharani kinyume na ulivyotarajia?

Umewahi kukataliwa hadharani kinyume na ulivyotarajia?

Hizi mambo za kukataliwa bn 🤣🤣 nliwahi kukaziwa na demu sura ya baba kinoma sema alikua na big mata core wanangu wa kwenye pool table walinicheka kinoma

Kuna manzi wahuni wengi walipita naye dadeq mi alinikazia
unaweza hisi una gundu pisi kitonga alafu inakukazia. Hao sura za baba wanakuwaga na wamenyimwa sura tu ila mambo mengine wapo vizuri.
 
Expectation kills , they kill us once when we wait for the same things we did for people. They kill us twice when we don't really get anything.
Maisha yanaenda kasi sana, leo nmekumbuka tukio moja lililowahi kunitokea miaka ya nyuma kidogo. Kuna dada wa kitanga niliwahi kumpenda sana, siku moja tukatoka out na ndugu zangu wawili tunaolingana umri, kila mtu alikuja na mpenzi wake na ndio ilikuwa mara ya kwanza kabisa kuwahi kufanya hivyo ili tufahamiane.

Tukafurahia sana mpaka pale ulipofika muda wa kutambulishana, furaha yangu yote ya siku ile ikazimwa baada ya kumtambulisha Ke wangu, aliongea akasema sifiti kwenye maisha yake alisimama na akashukuru kwa muda wetu na kuanza kuondoka, kila mtu miongoni mwetu alishangaa. Nilihisi naota nikanyanyuka kumfuata nje niongee nae lakini hakunipa nafasi hiyo, nikabaki nmesimama kama nimegandishwa mpaka alipokuja ndugu yangu kunichua.

Tulipofika tulipokua tumekaa hakuna nilichoweka mdomoni kikalika, niliona kiti nilichokalia kama kina miiba nikasimama napo nikaishia kuona kama sina hiyo nguvu ya kusimama. Pole na ushauri wa ndugu zangu niliona kama kelele tu hakuna waliloniambia nikapata unafuu, nilijiskia vibaya mno nikaona nimpigie simu akawa tayari ameshaniblock. Ile wiki nilikonda nikanyooka nikiwaza kwanini anifanyie vile kinyume na matarajio yangu? Tena hadharani alishindwa nini kunieleza hayo kabla/baada ya hapo?

Baada ya miezi 10 kupita alinitafuta na kuomba msamaha kwa alichonifanyia anaomba turudiane vinginevyo atajidhuru, bora afe kama sitoweza kurudiana nae haoni umuhimu wa kuishi bila ya mimi. Nilimwambia uliweza kuishi kabla ya kukutana nami na ukaweza ndani ya miezi 10 iweje sasa ushindwe? Safari njema huko uendako, Akataka kuongea nikamwambia sihitaji ujibu chochote alafu nikakata simu nikablock.

Aliwasumbua sana ndugu zangu sijui alipata wapi namba ya mama nikapigiwa simu nijaribu kuyamaliza na huyo binti nikakataa, kuna siku akafunga safari mpaka kwetu(mkoani) baada ya kuambiwa nimeenda nyumbani lakini msimamo wangu ukawa ni ule ule akaishia kuaibika na kudharaulika mpaka mama akaniambia mwanamke wa hivi hafai kabisa. Aliangaika kunigombanisha na niliokuwa nao kwenye mahusiano lakini hakufanikiwa mwishowe alitulia.

Leo kuna ndugu yangu kanitafuta ananiambia nasalimiwa sana na yule fulani, anasema amenitafuta kwa muda mrefu sana kwenye namba yangu anapokea mtu mwingine tofauti( namba ya mwanzoni niliipoteza post yake ipo humu), nmeishia tu kucheka na kukumbuka kilichowahi kunitokea kwenye mahusiano.

Ee bhana eeh! kupigwa na kitu kizito hadharani inaumiza sana hasa kwa yule unaempenda.
View attachment 2697404
Chai
 
😀😀😀Huu Uzi Umenikumbusha mbali sana niliwahi mkataa mtu kikatili sana Kuna mda namuoneaga huruma niliuza utu japo pia ulikuwa utoto kipind sijakua Bado Half american
Dah mpaka nine ogopa😃😃, una mkataa mtu mpaka ana ends kwenye Mizimu yao😂😂😂.
👉Ana iuliza amekosea wapi😂😂
 
Back
Top Bottom