Wasalaam!
Niwape pole, pia pongezi kwa kuhitimisha ama kuendelea kuhitimisha majukumu ya leo
Leo napenda tukumbushane juu ya maisha ya chuo, na hasa kwa upande wa changamoto tulizopitia katika kukamilisha ndoto zetu za kielimu.
Katika maisha ya chuo kuna changamoto nyingi mno, kuna kushinda njaa, kufukuzwa chuoni kwa sababu ya ada, Kuna kutoelewana na wakufunzi na hapo kupitia magumu magumu kweli kweli, je, wewe mwenzangu umepitia yapi katika kuikamilisha ndoto yako itimie?
;
NILIYOPITIA MIMI NI HAYA;
mimi njozi yangu niliijenga chini ya msingi wa mambo ya afya ya binadamu, miaka Kadhaa iliyopita nilifanikiwa kumaliza form six, na kujiunga na chuo x, kilichopo hapa Dar es Salaam (kwani ndipo karata yangu ilipoangukia baada ya application), nakumbuka kabla post hazijatoka, nilikuwa najishughulisha na mambo ya mapindi kwa masomo ya Physics, Chemistry, Biology na Maths, kuanzia form 3 mpaka form six, lakini pia kilimo, hasa cha mpunga MKOANI HUKO.
Basi Bhana , post zikatoka, nimechaguliwa kitu nlichokipenda sana, but mkopo hakuna, nikajadiliana na mzazi, akaniambia nenda siwezi shindwa kukulipia, nikaingia mzigoni, mwaka wa kwanza ukawa poa sana, wa pili ukawa poa kwa wasiwasi ila ukapita salama, watatu ada ikagoma kabisa, msosi hakuna, ela sina Nikawa natamani angalau nipate vijana wa six niwabrash waniachie hata jero jero Walau mkono uende kinywani ila wapi!
Hali ilikuwa tete kias kwamba nutritional status zilikua very poor, magonjwa ya fungus na nutritional deficiency hayaishi , chuo nikikanyaga nafukuzwa sababu ya ada , kiukweli hata utamu wa masomo hakuna , kuiba siwez, madili mjini hapa sina, je, nifanyeje na future yangu inapotea? Maana kila nkimcheck mother , economically hayuko poa, kihomehome tuko mim na dogo na dogo yuko five private! Je, nitafanya nini?
ITAENDELEA!