ryan riz
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 423
- 683
Moja ya vitu vya kustaajabisha hapa nchini,ni namna vyama vya upinzani vinavyoshindwa kula na kipofu na chama tawala na serikali pia
Watanzania tunajijua na rahisi sana kutekwa kisiasa ni mbinu tu za mtekaji akijipanga vizuri,yaani wapinzani wanashindwa kutumia mbinu hizi kwa serikali na chama tawala? Hivi vyama vya upinzani haviwezi kuendesha upinzani wao kwenye majukwaa mengine.
Kama vile mitandao,magazetini,radio na tv zao au watu binafsi kwani huko hoja ambazo wanazitaka kwenye hadhara zisikike mbona hata kwenye haya majukwaa zitatufikia?
Mbona wanayoyaongea kwenye mikutano ya ndani hutufikia nchi nzima, kama akina amber rutty mambo yao waliyafanyia chumbani na si uwanja wa mpira ila watanzania karibu 80% yaliwafikia na hawa watu sio maarufu ila kupitia haya haya majukwaa watu walipata taarifa.
Hapa na maanisha kwamba hoja zenye nguvu na mantiki zitawafikia walengwa wote hata ikiwa mwenye hoja kazitolea akiwa chooni anajisaidia ili mradi tu ayatumie hayo majukwaa vizuri. HIVI HUKO MITAANI MNAENDA KUONGEA NINI AMBACHO MNASHINDWA KUKIONGELEA KWENYE HAYO MAJUKWAA?
Yaani badala ya kuutumia huu wakati kuwapenyeza watu wenu sehemu mbalimbali nyeti kwa kutumia angalau kampasuko chao ila ndio mnastua mapema aanze kuwaona wale aliokuwa anawapinga kwenye chama chake kwamba walikuwa wako sahihi.......! Na hii itapelekea ajiimarishe kotekote ndani na nje.
Suala la katiba tusidanganyane kama hamjapata nguvu kwa wananchi na ushawishi angalau kwa maafisa wa vyombo vya usalama mtabakia hivyo hivyo,maana kule ndio kuna waanzilishi na ndio wanaowa´boost wananchi kukomalia hiyo inshu lakini nyie kupata msaada wa wananchi kudai katiba mpya kwa sasa bado sana maana hamna kitu kinachowaunganisha pamoja.
Wenzenu wanafanya juu chini kuja na mbinu za kuwatenganisha nao hata hao wachache mlionao. Suala la ajira mmeliacha,suala la huduma za kijamii hususani maji na umeme mmeliacha wakati Serikali inadanganya kwamba wamefikia karibu vijiji vyote kwa huduma hizi mmenyamaza ,uzembe makazini na huduma mbovu mmeliacha n.k. Haya ni baadhi ya mambo yangeweza kuwaonganisha na wananchi mkawashawishi hicho mnachokitaka.