Umewahi kuvielewa vyama vya siasa vya upinzani Tanzania?

Umewahi kuvielewa vyama vya siasa vya upinzani Tanzania?

hakuna mtu asietaka katiba mpya,suala ni mbinu za kuweza kuingia na kushawishi upate uungwaji na makundi mbalimbali kwenye kuidai...ukikariri mbinu za jicho kwa jicho basi kwenye maisha utashindwa vitu vingi mno....Mengi huenda kwa ushawishi na sikufichi ndugu...walipata kiongozi mrahisi sana kumuingia sababu alikuwa mpenda sifa sana kupitia hiyo hulka yake wangefanikisha mengi mno,sababu angejichukulia ndio rais wa kihistoria kuweza kuonganisha vyama vyote vya siasa na makundi yote katika jamii ila BAHATI MBAYA WAKAWAACHIA WENZEO WAKAFAIDIKA NAE BAADA YA KUMJULIA....ukweli na waambia hiyo nafasi haitarudi tena KAMA HIVI VYAMA HAVIBADILIKA......
Wabadilike waweje?
 
Mkuu watu walishindwa kuandamana kwa lisu kuibiwa kura kama anavyosema usitegemee wataandamana kwa jambo hili.

Watu wanafanya mambo mengine sasa hivi.

Hawa wanaohamasisha maandamao sio yanawapa kula ndo mitaji yao ilipo.
Huu ndio ukweli mkuu.

Zanzibar wameamua kukaa chini kwa pamoja na kujenga nchi yao. Ona mambo yao yanavyowaendea vyema.

Halafu, kwani nchi hii wapinzani ni CDM tu??
 
Huu ndio ukweli mkuu.

Zanzibar wameamua kukaa chini kwa pamoja na kujenga nchi yao. Ona mambo yao yanavyowaendea vyema.

Halafu, kwani nchi hii wapinzani ni CDM tu??
Yes mkuu.

Hapa bara bado kuna watu wanafurahi tu kutaka kuleta upinzani katika kila jamboo,wanaogopa wasipopknga kila jambo hawatakuwa na mtaji kisiasa,wanaogopa chama kitakufa hivyo wanatafuta kila njia chama kiendelee kusikika.
 
Upinzani wa kweli upo Zanzibar. Kikifika kipindi cha kupiga kura wanakuadhibu kwenye sanduku la kupigia kura.

Ila baada ya matokeo na maridhiano huwezi kusikia chokochoko za maandamano au harakati tena, wanasubiri tena miaka mitano.

Huku kwetu bara kila kukicha CHADEMA wanaibuka na ajenda mpya kuikwamisha serikali. Hawa viongozi wao 24/7 wanawaza siasa tena za fujo na ubabe. Wamesahau wananchi wengi tunafanya vibarua ili tupate mkate wa kila siku.

Mbaya zaidi hakuna jambo wanalo litimiza likaisha, mengi wanaweka pending wanaibuka na jingine.

Wamalize kwanza suala la wabunge wao 19 liwe closed.
 
Back
Top Bottom