Umiza akili katika maswali matatu, uongeze IQ yako

Umiza akili katika maswali matatu, uongeze IQ yako

Hizi ni chemsha bongo tatu tu ,na atakae patia chemsha bongo zote tatu bila kukosea namba hata moja, atapata zawadi ya Vocha ya mtandao atakao taka papo hapo.

Zinaenda kwa mfumo wa maswali hivo kuwa makini, Fikiria kabla hujajibu.

SWALI LA KWANZA
Je , ukiwa ndani ya mashindano na ukampita mtu wa pili, wewe unakuwa mtu wa ngapi?

SWALI LA PILI
Imagine ulikuwa na Mbuzi 15 ,wakafa wote isipikuwa Mbuzi 7 , Je utakuwa umebakiwa na Mbuzi wangapi?

SWALI LA TATU
Baba na mtoto wakiwa safarini walipata ajali na Baba akafa pale pale, Wakati mtoto yuko maututi akawaishwa hospitali , Doctor akasema " Siwezi kukutibu mwanangu".

Je, Doctor ni nani?

Zawadi ipo wazi kwa atakae jibu kwa usahihi maswali yote matatu.

GOODLUCK!
Mkuu hutendi haki, naumiza kichwa mtaani na jf pia?

Huku mimi nafurahi tu umiza wewe bhana aah
 
1: Mi mtu wa kwanza
2: Mbuzi 0 make wote wamekufa
3: Doctor ni mchepuko

Tuma kwa namba hii hii jina litakuja Evelyn
Hivi unakimbiliaga kujibu maswali uonekane wakwanza au ubongo wako ndio huu mfumo wake wa ufikiriaji?
 
Majibu ya Maswali
Swali no: 1 , Jibu : Wapili
Swali no2: Jibu: Huna mbuzi yani (zero)
Swali no: Jibu 😀k ni yule baba Aliyekufa pale pale
 
MAJIBU
1. Utakuwa mtu wa pili.
2.Utabakiwa na Mbuzi 7
3. Doctor ni mama
-Doctor hawezi toa excuse ya kutomtibu mtu. Yule ndie mama mzazi wa mtoto ndio maana akatoa excuse.

Kama kuna aliejibu hivyo na sikuona , Nambie ni page post ngapi 🙏🏾
Nilikwambia, majibu haya yalishatolewa.
 
MAJIBU
1. Utakuwa mtu wa pili.
2.Utabakiwa na Mbuzi 7
3. Doctor ni mama
-Doctor hawezi toa excuse ya kutomtibu mtu. Yule ndie mama mzazi wa mtoto ndio maana akatoa excuse.

Kama kuna aliejibu hivyo na sikuona , Nambie ni page post ngapi 🙏🏾
Nini maana ya mbuzi "wote kufa".... hao 7 walifufuka?
 
1.mtu wa 3
2.watabaki 7
3.doctor ni mama wa mtoto
 
Ukimpita mtu wa pili si ndio wewe unakuwa wa pili?
Ukimpita mtu wa pili obviously utakuwa mtu wa tatu kaka😁😁
Yaani tayari alikuwa mtu wa kwanza,na wa pili,na wewe utakuwa mtu wa tatu.
 
Back
Top Bottom