Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)


wakati wa maomboleza ya Mwendazake pale uwanja wa Uhuru huyu jamaa alikuwa msaidizi wa MC akishirikiana pia na Mkuu wa Wilaya Gondwe. kweli aliendesha vibaya sana na kusababisha vifo vingi, kuna wakati aliombwa na Raia pamoja na Mc mwenyewe atangaze kuwa kuna vifo uwanjani AKATAA bado wakapenyeza majina ya watoto waliopotea wakiwatafuta walezi wao yanatajwa majina, akarukia Microphone na kufuta utaratibu huo, hapo nilijua Mnyakyusa huyu aliyetokea Ukurugenzi huko Kakonko ni kichaa na sio mbabe tu, hapohapo angefukuzwa kazi, mbona mikoa mingine hawakuwa hivyo
Bravoo Ummy Mwalimu
 
Jaffo ajiangalie na huko alipo.
akitoka hapo ataenda kulima

Una uhakika hawakuwa watoto pendwa wa jiwe?
Si unaona dj mpya anavyopiga ngoma kali kali....anaweza asipende ngoma yake
 
Hongera Ummy mwalimu, bado sasa tumbua wakurugenzi wafuatao, Tarime, chunya ,ikungi, bukombe, GeitaDc, arusha dc,arusha mjini, chalinze, mtama, kilosa, Bahi,karatu, babati, Kahama,igunga, simanjiro, siha, biharamulo, nyangwale. Na ninashauri Rais asiwateue wakurugenzi kwanza asubiri ufangio wa Ummy mwalimu upite ndipo ateue.
 
Unakimbilia wapi? Ni Mwakabibi na sio Mwakibinga. Mkiitwa misukule mnasema mmetukanwa.
 
Asije akamsahau na wa manispaa ya Kahama ,kwa mda alioachwa nao kutuligishia hilo gari inatosha saana
 
Huyo mkurugenzi wa Temeke kwa namna alivyokuwa anaendesha ofisi ni sahihi kutumbuliwa.
Malalamiko juu yake yalikuwa mengi sana, shida sijui ilikuwa wapi kwa mamlaka yenye dhamana ya uteuzi kumtoa toka awamu ile ya hayati Magufuli.
Huyu Mwakibibi lazima atakuwa mtu mjinga sana.
Hakusoma alama za nyakati hata baada ya Mama Samia kutoa onyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…