Ummy Mwalimu: Rais Samia amejenga madarasa 3,000 huko nyuma Serikali haikujali kuhusu madarasa na shule

Ummy Mwalimu: Rais Samia amejenga madarasa 3,000 huko nyuma Serikali haikujali kuhusu madarasa na shule

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Huko nyuma watu hawakujali kuhusu Shule/Vituo Shikizi. Ni Serikali ya Awamu ya 6 ya Rais Samia ndio imechukua hatua mahususi na za haraka za kujenga madarasa ya kisasa 3,000 tena kwa mpigo katika Shule Shikizi 970 kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

Niwahakikishie Watanzania kuwa TAMISEMI tutazifikia shule shikizi zote zinazokidhi vigezo (nyingine zimejengwa kwenye maeneo ya hifadhi au maeneo hatarishi kama karibu kabisa na machimbo ya migodi) na kujenga miundombinu ya kisasa. #KaziIendelee
 
Viongozi sometimes oneni aibu aise mpo kwaajili ya kulitumikia taifa yeye hakufanya wewe umefanya ila aliepita yapo aliyofanya so kila mmoja afanye awezalo.
 
(nyingine zimejengwa kwenye maeneo ya hifadhi au maeneo hatarishi kama karibu kabisa na machimbo ya migodi) na kujenga miundombinu ya kisasa. #KaziIendelee

My take: kaazi kweli kweli. Ina maana hizo zitavunjwa/kubomolewa na hivyo hasara kupatikana. Sisi wabongo ndivyo tulivyo.
 
Huyu naye anapitiliza katika kujikomba .Hivi ukisema serikali imejenga.madarasa mdomo wako utapinda.?.Hiyo hela ya ujenzi wa madarasa siyo ya ssh,ni kodi ya watanzania.
 
Aseme tu kuwa Magufuli alikuwa kichaa , kazi yake ni kununua midege cash tu

Hakuna mtu alijali Elimu kama Magufuli. Sijui wewe umezaliwa lini. Hata hivyo statement za mawaziri ni za kumpa kichwa bosi.

Elimu Bure ilianza na JPM.

Ukarabati wa Shule Kongwe zote umefanyika chini ya JPM.

Madawati yalitengenezwa mengi sana chini ya JPM tena mengine wananchi wenye nazo walitengeneza mengi sana.

Ujenzi wa shule ulifanyika kwa kiwango cha kutosha kwa wakati ule. Ukichunguza utagundua kwamba watoto wameongezeka kwa kasi sana hivyo inabidi kuongeza madarasa, hongera kwa serikali kuliona hili.
 
Huko nyuma watu hawakujali kuhusu Shule/Vituo Shikizi. Ni Serikali ya Awamu ya 6 ya Rais @samia_suluhu_hassan ndio imechukua hatua mahususi na za haraka za kujenga madarasa ya kisasa 3,000 tena kwa mpigo ktk Shule Shikizi 970 kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

Niwahakikishie watanzania kuwa @ortamisemi tutazifikia shule shikizi zote zinazokidhi vigezo (nyingine zimejengwa kwenye maeneo ya hifadhi au maeneo hatarishi kama karibu kabisa na machimbo ya migodi) na kujenga miundombinu ya kisasa. #KaziIendelee
" .... rais kajenga madarasa 3000..."

Huyu rais atakua na ela nyingi sana.

NB: Sijawahi sikia nchi kama USA, German, UK nk nk wakisema "rais katoa msaada kwa Tanzania dola milion kadhaa..".
 
Serikali ya Chadema hawakujali kuhusu shule na vituo shikizi. Bora walitoka madarakani
 
Huko nyuma watu hawakujali kuhusu Shule/Vituo Shikizi. Ni Serikali ya Awamu ya 6 ya Rais @samia_suluhu_hassan ndio imechukua hatua mahususi na za haraka za kujenga madarasa ya kisasa 3,000 tena kwa mpigo ktk Shule Shikizi 970 kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

Niwahakikishie watanzania kuwa @ortamisemi tutazifikia shule shikizi zote zinazokidhi vigezo (nyingine zimejengwa kwenye maeneo ya hifadhi au maeneo hatarishi kama karibu kabisa na machimbo ya migodi) na kujenga miundombinu ya kisasa. #KaziIendelee

Ummy Mwl ni as if ameikuta TAMISEMI haikufanya kitu wakati kuna mengi yamefanyika, ila wakubaliane tu kuwa kila mtu anafanya kwa sehemu as per budget aliyopewa.

Kumbukumbu za mwaka 2017 na 2018 zinaonesha kuna mambo Tamisemi walifanya;

Na utakuta kwenye hizo halmashauri ambazo baadhi shule zilikuwa choka mbaya, kuna mkurugenzi kaidhinishiwa kununuliwa na TAMISEMI V8 la mil 400 🙄;
 
Huyu dada na mishavu yake akiongea utadhani ulimi unataka kumchomoka. Samia kajenga hizo pesa katoka nazo Chukwani ama Fuoni.
 
sishangai maana huyu alishawahi hata kumnanga JK ilihali yeye ndiye aliyempa shavu (sijui kwa makubaliano gani)...naye ni walewale vilaza tu jamii ya Jeni sijuia hata wamewezaje kuwa mawaziri...
 
Back
Top Bottom