Katika taarifa yake huko Simiyu, waziri Ummi ameonekana na kusikika akitoa ruhusa kwa Madaktari kutumia government facilities kuendesha huduma zao binafsi.
Jambo hilo lina ukakasi na limezua sintofahamu, sababu haliingii kichwani, hata ukijaribu kupunguza ubongo ili ulipatie nafasi bado linakataa.
Namfahamu Ummi, nampenda sana kiutendaji, itoshe tu kusema ninamkubali utendaji wake.
Ninachoamini ni kwamba, either Waziri hakuzingatia maelezo aliyopewa ya utaratibu ulivyo, au hakuelewa vyema, ila vyovyote vile, utaratibu (IPPM) ambao waziri alijulishwa ni mzuri sana na Muhimbili unafanya kazi. Isipokua, siyo kwa namna ilivyokua presented na Waziri Ummi.
Ushauri wangu, Katibu wa Wizara au Chief Medical Officer mmoja wao ajitokeza kuliweka sawa hili jambo. Sioni nia mbaya ya waziri au serikali, bali naona kuna utoaji wa message tofauti na iliyokusudiwa.
I beg to move.