Umoja Party waelezea sababu ya kutumia picha ya John Magufuli

Umoja Party waelezea sababu ya kutumia picha ya John Magufuli

Chifu nisingependa kukaa mbali na wewe namba. 11 itapendeza halafu ninaishonea pamoja na kichinjio kwa lamination.
Safari hii na mimi nataka kumiliki kadi ya chama cha kisiasa. Nifanyieni mpango kadi namba 12.
 
Watanzania tutachezewa sana na ccm. Hicho chama kimeundwa kimkakati na ccm ili kuwapumbaza watu waelekeze mijadala kwenye vyama wasahau matatizo yaliyopo kwasasa kama kupanda kwa gharama za maisha, petrol juu, umeme kukatika katika na matatizo kede kede yaliyopo kipindi hiki.

Heko kwao ccm ni ma genius sana kucheza na upepo wa kisiasa kulingana na nyakati husika. Baada ya uchaguzi mkuu utakuta waanzilishi wanarudi ccm na chama kujifia kifo cha mende.

Big up tena ccm.
 
Chama kinakuja kwa kasi walahi.

Kimefunika mambo yote yanayoendelea duniani.

Kadi yangu iwe namba 10.

Hofu yangu wanaweza kukibania hiki chama maana hawataki tukombolewe kwenye lindi la Ujinga na Umasikini.
CCM ndo imekupa umaskini huo ulionao? Mbona mimi sio ccm lakini nimejikwamua sipo kwenye hayo unayolalamika.

Fursa zipo kibao tatizo hujishughulishi tu kucheza na fursa.

Halafu hicho chama ni mbinu za ccm kama kawaida yao panapotokea sintofahamu kama hivi kila kona malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda gharama za maisha.

Ikabidi wajinga waanzishiwe kitu cha kujadili ili wasahau matatizo yaliyopo na ccm wapate kuendelea na mipango yao pasipo kelele.

Ukiwa mwanachama wa hicho chama basi ujue kabisa wewe una kadi ya ccm kea mlango wa nyuma.
 
Chama kinakuja kwa kasi walahi.

Kimefunika mambo yote yanayoendelea duniani.

Kadi yangu iwe namba 10.

Hofu yangu wanaweza kukibania hiki chama maana hawataki tukombolewe kwenye lindi la Ujinga na Umasikini.

Chama hakiwezi kuwakomboa, mnajikomboa wenyewe.
 
Waanzishe magufuli part Ili tuwape nchi Chadema imeshindwa
Kumbe hicho chama kipo kushinda a na chadema?. Chadema Ina kazi Sana. Huku CCM huku wafuasi wa Magufuli wenye hasira kwa Nini Magufuli amefariki na tundu Lissu yupo hai.
 
Safari hii na mimi nataka kumiliki kadi ya chama cha kisiasa. Nifanyieni mpango kadi namba 12.
Nendeni kwenye ofisi mkajisajili sio Happ JF. Nachojua hakuna Mwana CCM anapenda kwenda upinzani na wengi huwa hawadumu upinzani. Upinzani kule game analiweza chadema tu wengine wanchungulia na kukimbia.
 
Watanzania tutachezewa sana na ccm. Hicho chama kimeundwa kimkakati na ccm ili kuwapumbaza watu waelekeze mijadala kwenye vyama wasahau matatizo yaliyopo...
Na wanajua kucheza na watu. Halafu Cha kushangaza wanaokishabikia hicho chama wanaiponda chadema Happ ndipo niliposhtuka.
 
Chama kinakuja kwa kasi walahi.

Kimefunika mambo yote yanayoendelea duniani...
Mwambie msajili aache usaniii akidhani atatupumbaza. Hicho chama kimeundwa na ccm kwa kushirikiana na Tiss, lengo ni kuipa ccm back up kwenye uchaguzi. Mbinu hizi za kizee za ccm ni kupoteza muda maana wananchi kwa sasa wanauelewa mpana.

Kutatengenezwa mgogoro fake ndani ya ccm ili kukitengenezea hicho chama popularity. Lakini mchezo wote tunaujua tumebaki tunawachora tu.
 
Back
Top Bottom