Umoja Party waelezea sababu ya kutumia picha ya John Magufuli

Umoja Party waelezea sababu ya kutumia picha ya John Magufuli

BORA CCM IGAWIKE NAYO
WAMEZOWEA KUWAGAWA VYAMA VYA WENZAO TUU.
LAKINI NAHISI KAMA MSAJILI ANAANZA KULETA FIGISU.

Natamani Ndungae awemo kwenye chama Hicho,
Kabudi na Lukuvi.
Mashetani wakikutana nyasi huwaka moto.
 
Nauliza, kwa sababu sijawahi kuwasikia wakisema wanampenda Jiwe kwa sababu anawauwa na kuwateka.

Kawaulize sukuma gang maana ndio walikuwa wanamkubali the likes of Makonda etc
 
Kawaulize sukuma gang maana ndio walikuwa wanamkubali the likes of Makonda etc
Basi wanayo yaliyokuwa yanawafanya wampende Jiwe, kuteka na kuuwa si miongoni mwa hayo mambo.

Tatizo ni kutaka watu wote tumtazame Jiwe kwa mtazamo kama Zitto kabwe.
 
Mwanzilishi wa Chama cha Umoja Party, Seif Maalim ametoa sababu za kwanini chama hicho kinatumia picha ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika fulana zao.

Maalim amesema chama hakina nia mbaya kutumia picha hiyo kwa kuwa ni moja ya njia ya kujitangaza kwa wananchi.

"Unajua sera zetu zinaendana mrengo wa falsafa za yule anayeonekana katika picha (Hayati John Magufuli) kwenye fulana. Ni harakati za kujitangaza kwa wananchi na hatuna nia mbaya. Kama ni kosa kisheria basi tupo tayari kujirekebisha," amesema.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, ilidai kuwa Umoja Party imewasilisha maombi ya usajili wa muda na mchakato bado unaendelea lakini chama hicho kimekuwa kikikiuka utaratibu wakati maombi yao yakishughulikiwa.

Ameongeza kuwa, kuna picha zinasambaa mtandaoni zikionesha watu wanaonekana kuwa wanachama na wamevalia fulana zenye bendera ya chama hicho pamoja na picha ya kiongozi ambaye si mwanachama wao.

"Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatumia fursa hii kuwakumbusha wanaotengeneza, wanaovaa fulana hizo na Watanzania wote kuwa, ni kosa la kisheria kwa taasisi yoyote kufanya kazi kama chama cha siasa wakati sio chama cha siasa kilichosajiliwa," ameeleza

---
Pia soma - Kwanini Umoja Party wanaweka picha ya Hayati Magufuli kwenye tisheti zao?
Kaole sanaa group.

You can fool some peow sometime.

Chama cha Mtungi hicho.
 
Back
Top Bottom