Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
"History doesn't repeat itself but it often ryhmes" Mark Twain

Kabla ya mwaka 1914, Ujerumani na Austro-Hungary walikuwa ni mataifa ambayo hayawezi kutenganishwa kwa lolote lile. Mkubwa alikuwa Ujerumani na mdogo alikuwa ni Austria.

Austro-Hungary lilikuwa ni taifa linalotawaliwa na familia ya Habsburg (The Habsburg Family) ambayo pia ndiyo familia iliyokuwa inatawala dola la rumi takatifu almaarufu kama The Holy Roman Empire kwa miaka zaidi ya 500.

The Habsburg Family ilikuja kudidimia na dola lao la rumi kuanguka na kubakiwa na nchi ndogo yenye mipaka midogo ya Austro-Hungary. Ujerumani kama taifa ilizaliwa mwaka 1871, na baada ya hapo ilishikamana na Austria wakiwa na imani kwamba Austria ni ndugu zao wa damu.

Austro-Hungary ilikuwa na mikakati ya kutawala makoloni yake ya Ulaya Mashariki ambako watu wengi ni Slavic, tena wenye dini tofauti. Jambo baya ni kwamba Austro-Hungary aliamini kabisa kwamba wao walikuwa na haki kutoka kwa MUNGU ya kutawala eneo lote la Ulaya hasahasa maeneo yaliyowahi kuwa sehemu ya The Holy Roman Empire.

Austro-Hungary aliyakalia maeneo kama Serbia, Slovenia, Croation, Bosnia na Herzegovina ambayo baadaye yalikuja kuunda taifa liitwalo Yugoslavia. Slavic People walianza harakati za kudai uhuru kwa njia ya vurugu dhidi ya Austro-Hungary na kupelekea machafuko na umwagikaji mkubwa wa damu.

Slavic People waliungwa mkono na taifa kubwa la kislav la Urusi, ambalo lilikuwa ni adui mkubwa wa Ujerumani na Austro-Hungary. Hivyo Urusi akawa anawatumia Slavs walioko ndani ya dola la Austro-Hungary na Ottoman Empire kuleta taharuki.

Ikumbukwe, mwaka 1914, wanaharakati wa kundi la kigaidi na wadai uhuru wa Kislavic liitwalo The Black Hand lilifanya mauaji ya mwana mfalme wa Austro-Hungary, Archduke Ferdinand alipoenda kufanya matembezi kwenye makoloni hayo. Kijana mdogo aitwayo Gavrilo Princip alimuua Ferdinand na mke wake Sophia na kusababisha vita ya kwanza ya dunia.

=============================================
Uhusiano wa hiyo nadharia yangu ya hapo juu, unafanan na kile kinachoendelea leo duniani, hasahasa kule Mashariki ya kati, ambapo Marekani ndiyo Ujerumani ya leo na Israeli ndiyo Austro-Hungary.

Ujerumani lilikuwa ni taifa lenye nguvu zaidi za kijeshi barani Ulaya kwa wakati ule na lilikuwa ndilo linamkingia kifua Austro-Hungary alipotishiwa na Urusi na mataifa mengine ya Ulaya.

Austro-Hungary kama Israel, walikuwa wanaamini kwamba maeneo yaliyowahi kuwa ya The Holy Roman Empire na The Habsburg Empire ni lazima yarudishwe na kuendelewa kushawishiwa kwa namna yoyote hata kama jambo hilo lingezua taharuki. Habsburg waliamini kabisa walikuwa na haki kutoka kwa MUNGU maana miaka ya nyuma watawala wake walipakwa mafuta na Papa wa Vatican ili watawale Ulaya nzima. Haya mawazo yaliendelea kuwakaa hata baada ya falme zao kuanguka.

The Black Hand, walikuwa ni wapigania uhuru wa Bosnia waliotumia mbinu za kigaidi dhidi ya Austro-Hungary ambayo ilikuwa inatawala nchi yao na kusema kwamba ni haki yao ya KIMUNGU kufanya hivyo. Unaweza kudhani walikuwa wanatania lakini kwa kipindi hicho, watu wengi waliamini kabisa The Habsburg walichaguliwa na MUNGU kutawala Ulaya yote hasahasa kupambana na dola la kiislamu la Uturuki almaarufu kama The Ottoman Empire.

Hivyo, binafsi nalifananisha kundi la The Black Hand, kama makundi ya Hamas, Hezbollah na PLO, ambayo yanaamini kabisa yanapigania uhuru wao na kutumia mbinu za kigaidi kupata huo uhuru. Lakini upande wa pili, haya makundi yaliitwa makundi ya kigaidi na mataifa ya Ujerumani na Austro-Hungary, ambayo yalitumia mbinu zote kupambana nayo.

Urusi ya kipindi kile, ndiyo Iran ya leo hii. Urusi ilikuwa na imani kwamba inalinda dini ya Kiorthodoksi na kulinda jamii ya Kislaviki dhidi ya uvamizi wa Ujerumani, Austro-Hungary na Ottoman Empire. Hivyo warusi waliyaunga mkono makundi kama The Black Hand katika kusababisha taharuki.

Tatizo ni kwamba, alipouwawa Archduke Ferdinand, Austro-Hungary alisema The Black Hand wamefanya ugaidi hivyo Bosnia kama nchi itabidi iwajibike na isipofanya hivyo itavamiwa kijeshi. Ujerumani bila kufikiria aliiunga mkono Austro-Hungary kwa kusema wana haki na kuihakikisha msaada kijeshi endapo itatishiwa na Urusi wakati inavamia Bosnia.

Matukio ya mwaka 1914 yalikuwa hivi:
1. Archduke anauwawa na mke wake Sophia.
2. Austro-Hungary inatoa masharti na kusema Bosnia iwajibike.
3. Bosnia inagoma kuwajibika, Austro-Hungary anatangaza vita na kuvamia kijeshi.
4. Urusi kuona Austro-Hungary imevamia Bosnia, yeye anaitangazia vita Austro-Hungary.
5. Ujerumani kuona Austro-Hungary atabagazwa na Urusi, yeye anaitangazia vita Urusi.
6. Bahati mbaya sana, Urusi alisaini mkataba wa ulinzi na Ufaransa ambaye naye anaitangaza vita dhidi ya Ujerumani.

Mambo yameenda, mwishowe Uturuki na Uingereza wakaingia kwenye vita na jambo ambalo lilitegemewa kuwa la wiki tu, likaenda miaka minne na kuua mamilioni ya binadamu wasio na hatia. Ikumbukwe wakati vita inarindima, taifa la Marekani lilikuwa limekaa pembeni na kutofungamana na upande wowote (A Neutral State) hadi pale maslahi yake yalipoguswa.

Ikumbukwe kipindi hiki, Marekani ndiyo lilikuwa moja kati ya mataifa yanayokuwa kwa kasi kiwango cha kushindana na Ujerumani na Uingereza hata kuwapita kwenye uzalishaji na uchumi (GDP in PPP). Hivyo dunia nzima ilitegemea kukopa na kununua kwa Marekani ili kuendesha vita tokea mwaka 1914-1917.

Leo hii, Marekani ya mwaka 1914 haina tofauti na Uchina ya mwaka 2024. Mbali na kuwa na mvutano na Marekani, lakini ukweli ni kwamba dunia nzima kuanzia Marekani, Ulaya, Asia na Afrika tunategemea Uchina kwa uzalishaji wa kiviwanda. Uchina anatumia mabavu, lakini mpaka sasa hajawahi kutumia jeshi lake kuvamia nchi yoyote ile duniani, mbali na kuvamia Vietnam mwaka 1979.

===================================================
Binafsi naamini kwamba tayari WW3 imeshaanza, sema itachukua muda mrefu mpaka tuje kukubali kwamba imeshaanza. Ukisoma historia utafahamu kwamba vita ya kwanza ilianza mwaka 1871 baada ya Franco-Prussia War, ambapo Ufaransa alitandikwa na Ujerumani na kunyang'anywa vipande vya ardhi. Matukio ya vita ndogo-ndogo na uaduia yaliendelea duniani kote kwenye makoloni hadi kufikia tamati mwaka 1914.

Mambo muhimu kuzingatia kwasasa ni haya
-Anguko la USSR 1991,
-Uvamizi wa Yugoslavia na NATO 1999,
-Uvamizi wa Afghanistan 2001 na Iraq 2003,
-Kujitanua kwa makundi kama NATO, QUAD, ANZUS n.k
-Uvamizi wa Ukraine 2014
-Arab Spring 2011
-Kukua kwa Uchina (The Ascendancy of China)
-Kukua kwa sayansi na teknolojia ambako kumeleta mataifa kujiamini mno.
-Gaza Genocide, Invasion of Lebanon, Hamas Invasion of Israel.

NB: Hapa litakuja kutokea tukio moja baya mno na wote watabwaga manyanga.

ENIWEI, ni mtizamo tu na kuna sababu nyingi nimeziacha zilizosababisha WW2 ambazo pia ni muhimu kuzipitia, mfano kufeli kwa UMOJA WA MATAIFA (The League of Nations) ambapo Adolf Hitler kama afanyavyo Benjamini Netanyahu leo na watawala kama Trump, Bush, Putin, Blair, Clinton wamefanya waziwazi kupuuza maamuzi ya UNITED NATIONS na kutumia mabavu kulinda maslahi yao.

Mussolini na Hitler waliyatoa mataifa yao LEAGUE OF NATIONS na kuapa kwamba watapambana na umoja huo kwa namna yoyote ile. Hili halina utofauti na kile ambacho Israel na Marekani wamekionesha juzi baada ya kutishia waziwazi kusema watavishambulia vikosi vya walinda amani wa UNITED NATIONS endapo hawataondoka.

=================================================
Indeed these are interesting times, and I say "What a good time to be alive"

Ninatamani sana Wamagharibi washinde, unfortunately, hawana uwezo huo kwa sasa.
Ukiangalia kinachoendelea United Nations hasa kwenye upigaji wa kura ndiyo unaweza ukabaki mdomo wazi. Nchi kama Ireland imeweka wazi kabisa msimamo wake dhidi ya Israeli. Nimeshangaa kuona Mfaransa na Italia wanaikosoa Israeli waziwazi, jambo ambalo siyo kawaida kuliona.

Mauaji ya kimbari kule GAZA na LEBANON ni jambo ambalo limewagharimu NATO na EU, na litaendelea kuwagharimu. Baada ya haya matatizo kuisha Wayahudi watakaa chini na kujutia mno hiki ambacho wanakifanya. Wajerumani walipooneshwa video za muaji ya watu yaliyofanywa na The SS walibaki wanalia na kujutia tu.
 
  • Kukua kwa Uchina (The Ascendancy of China)
  • Kukua kwa sayansi na teknolojia ambako kumeleta mataifa kujiamini mno.
  • Gaza Genocide, Invasion of Lebanon, Hamas Invasion of Israel.

NB: Hapa litakuja kutokea tukio moja baya mno na wote watabwaga manyanga.

ENIWEI, ni mtizamo tu na kuna sababu nyingi nimeziacha zilizosababisha WW2 ambazo pia ni muhimu kuzipitia, mfano kufeli kwa UMOJA WA MATAIFA (The League of Nations) ambapo Adolf Hitler kama afanyavyo Benjamini Netanyahu leo na watawala kama Trump, Bush, Putin, Blair, Clinton wamefanya waziwazi kupuuza maamuzi ya UNITED NATIONS na kutumia mabavu kulinda maslahi yao.

Mussolini na Hitler waliyatoa mataifa yao LEAGUE OF NATIONS na kuapa kwamba watapambana na umoja huo kwa namna yoyote ile. Hili halina utofauti na kile ambacho Israel na Marekani wamekionesha juzi baada ya kutishia waziwazi kusema watavishambulia vikosi vya walinda amani wa UNITED NATIONS endapo hawataondoka.

=================================================
Indeed these are interesting times, and I say "What a good time to be alive"

INgawa siamini Sana ulichotabiri
Ila nikupongeze kwa uchambuzi mzuri Sana wa kihstoria una kitu mkuu
 
Usiseme "ana kitu" Huyu ni gwiji wa haya mambo na ni hadhina ya Jamii forum,Sema kwakua uchammbuzi wa mada kama hii wachangiaji huwa tunaingiza udini ndomana mkuu MALCOM LUMUMBA na magwiji wengine hawaleti mabandiko kama haya sikuhizi.
 
Ukiangalia kinachoendelea United Nations hasa kwenye upigaji wa kura ndiyo unaweza ukabaki mdomo wazi. Nchi kama Ireland imeweka wazi kabisa msimamo wake dhidi ya Israeli. Nimeshangaa kuona Mfaransa na Italia wanaikosoa Israeli waziwazi, jambo ambalo siyo kawaida kuliona.

Mauaji ya kimbari kule GAZA na LEBANON ni jambo ambalo limewagharimu NATO na EU, na litaendelea kuwagharimu. Baada ya haya matatizo kuisha Wayahudi watakaa chini na kujutia mno hiki ambacho wanakifanya. Wajerumani walipooneshwa video za muaji ya watu yaliyofanywa na The SS walibaki wanalia na kujutia tu.
Kwahyo Ile October 7 haikuwa genocide? Israel ina haki zote za kujilinda kwanamna yoyote ile hata wafe wapalestina au walebanon wangapi, hao watapita ila Israel itabaki
 
Mkuu wa nini Israel imechelewa kulipa kisasi kwa Iran wakati sio tabia yao.
Unadhani Hesbullah na Hamas awamu hii watatoboa au ndio mwisho wao kabisa.
Andiko limekaa sawa sana.
Tofauti na wengi tunavyoamini, Israel hawezi kufanya jambo lolote lile bila baraka za America's Military Industrial Complex. Hivyo kama mpaka sasa hajafanya lolote ni aidha Marekani kamwambia asifanye au wanatafuta njia nyingine ya kulipiza kisasi bila kusababisha vita kubwa Mashariki ya kati hasahasa eneo la The Persian Gulf ambako ni moja ya vitovu muhimu vya uchumi wa dunia (An Oil Choke Point).
 
Hapo nimekuelewa maana nilimsikia kiongozi mmoja wa Iran anasema moja ya mikakati kama vita itazuka ni kuigunga hiyo ghuba kabisa. Hapo matokeo yake yatatuathili wote.
 
Kwahyo Ile October 7 haikuwa genocide? Israel ina haki zote za kujilinda kwanamna yoyote ile hata wafe wapalestina au walebanon wangapi, hao watapita ila Israel itabaki
Naomba kuuliza tu: Nini kilipelekea matukio ya October 7 ????
=======================================================
Lakini pia kumbuka hili: Wakati Ufalme wa Judea, unapambana na Warumi mwaka 70 A.D kule kwenye ngome ya MATSADA, Wayahudi wengi wenye msimamo mkali waliamini kwamba hawewezi kushindwa vita, hivyo wakaamua kufanya uasi dhidi ya Warumi.

Jenerali Titus na baba yake Kaisari Vespasian waliwpiga vibaya mno Wayahudi. Walivunja ngome ya MATSADA na kuteketeza hekalu la Mfalme Suleimani na kuua maelfu ya Wayahudi ambao wengi walikimbilia Asia, Afrika na Ulaya. Halafu nchi ya Yudea wakaibadilisha jina na kuiita Ufilisti na kuwapa maadui wa Israeli waliokuwa wanaishi pale.

Mwisho kabisa : Mwaka 1914, Austro-Hungary na Ujerumani waliamini kwamba hawewezi kushindwa vita na taifa lolote Ulaya, kwasababu haki yao ya kutawala wengine ni Divine
==============================================
Swali langu kwako mkuu: Mwisho wa haya yote utakuwa ni upi ?
 
Hapo nimekuelewa maana nilimsikia kiongozi mmoja wa Iran anasema moja ya mikakati kama vita itazuka ni kuigunga hiyo ghuba kabisa. Hapo matokeo yake yatatuathili wote.
Persian Gulf peke yake kwa siku hupitisha mapipa ya mafuta yasiyopungua milioni 16 kwenda duniani kote. Zaidi ya asilimia 20% ya nishati ya Uchina inayoendesha viwanda vyake inatokana na mafuta kutoka Iran. Hivyo yakitokea matatizo ni kwamba uzalishaji nchini Uchina utaathirika mno, kupelekea uchumi wa dunia nzima kuanguka.
 
Russia na china kama waki side na Iran basi ww3 inakuja...

Netanyahu na Hitler kama hawana tofauti
Binafsi naamini WW3 imeshaanza tayari, sema itachukua muda mrefu wengi kufahamu kwamba tayari dunia imeshavuka mstari na mambo hayawezi kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Siasa za dunia huendeshwa na RealPolitik a.k.a The Balance of Power. Mzani wa nguvu wa dunia usipowiana tu ni lazima mataifa makubwa yapigane kimabavu. Ukraine na Gaza vimekuwa vichocheo vikubwa.

Njia pekee ya kuzia vita baina ya Israel na Iran ni kuhakikisha The Balance of Power in the region is restored. Hapa itawalazimu Iran na Israeli waheshimiane kimaslahi (Spheres of Influence & Interests). Ambapo ni lazima Iran akubali kuitambua (Formal Recognition) Israeli kama taifa huru na sehemu ya Mashariki ya kati, huku Israeli akikubali The Two States Solution kama ambavyo United Nation Resolution 242 inataka.

Huku upande mwingine, itabidi Iran iwe A Nuclear Power ili kuhakikisha Absolute Deterrence dhidi ya NATO+ISRAEL. Yanayoikuta Iran leo hii hayana utofauti na yalichokikuta Pakistani kuanzia mwaka 1971-1998, ambapo India alikuwa ana nguvu kubwa kijeshi kuliko Pakistani, na mara zote alivamia na kumtandika vibaya mno. Mwaka 1998 India akamua kabisa kuandaa vikosi na kufanya majaribio ya silaha za nyuklia jambo ambalo lilimtishia kabisa Pakistani.

India alikuwa anajianda kumtafutia Pakistani sababu kule Kashmiri ili amtandike na kumvamia. Mataifa kama Uchina ikabidi waisaidie Pakistani kupata silaha za nyuklia kwa haraka ili kuweza kurudisha The Balance of Power in Central Asia. Baada ya Pakistani kufanya majaribio ya nyuklia, ikamlazimu India kurudisha makabrasha ya vita kwenye kabati na mpaka leo hajathubutu kuivamia Pakistani.

Hili linawezekana japo lina hatari kubwa mno: Litapelekea Nuclear Weapons Race duniani kote, ambapo Saudi Arabia, UAE na Qatar watazitaka hizo silaha kwasababu hasimu wao anazo. Pia NATO na QUAD wanaweza kuruhusu taifa kama Japan, Taiwan kuwa na silaha za nyuklia ili kumkomesha Uchina.

Dangerous times indeed.
 
Back
Top Bottom