baro
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,129
- 4,028
Mwamba wewe ni undisputed kwenye historia na evidence , hongera sanaUmeongea mambo mengi sana bila kuweka ushahidi wowote, hili ni kosa. Chanzo chako kikubwa cha haya uliyoyasema hapa ndiyo kile tunaita TRUST ME BRO. Lakini pia umepinga hoja zangu bila kueleza dhahiri hoja yako ni ipi na wewe unasimama wapi (Your Points are Vague, and they lack veracity), japo ntajitahidi kuzijibu kwa ushahidi:
Mosi, taifa la Israel limeundwa mwaka 1948 na UNO kwa msaada mkubwa wa USA, USSR na Great Britain. Unaposema Israel na USA wamekutana njiani sielewi ulikuwa unamaanisha nini.
Pili, unaposema taifa la Israel linaweza kuendelea bila hata msaada wa USA au taifa lolote lile bila kuleta ushahidi wa kuthibitisha hoja yako ni udhaifu mwingine mkubwa wa hoja yako. USA anaisaidia Israel DIPLOMATICALLY, FINANCIALLY, TECHNOLOGICALLY and MILITARILY, na ni mtu mjinga tu ndiyo anaweza kupinga hili. Kila mwaka, USA anaipa Israel msaada wa USD 3.8 Billion kama msaada wa kijeshi.
Tatu, unaposema makampuni ya Israel yanafanya vizuri na yako kwenye Black Market, napata wasiwasi na uelewa wako wako wa uchumi. Hebu nitajie walau makampuni matano makubwa ya Israeli ambayo yanaweza kulinganishwa na yale Top Ten of Fortune 500.
Nne, Israel haijamsaidia USA kupata Misri. Marekani amekuwepo LEVANT hata kabla ya kuundwa Israel 1948. Ukisoma historia utafahamu kwamba, Middle East/Persian Gulf kushawahi toke THE IRAN CRISIS 1946, ambapo USA na USSR walikuwa wanagombania kutawala Iran baada ya WW2 kuisha. Harry Truman walivutana na Joseph Stalin hadi kupelekea USSR kuondoa vikosi vyake kule.
Wewe unaposema Israel ndiyo imemsaidia USA kuzipata nchi za Middle East umeliokota wapi, ilhali tunafahamu kwamba USA amekuwepo eneo hilo hata kabla ya Israel haijawa nchi ???
Kuna nyakati huwa naogopa kujadili na wewe nabakia kuwa msomaji tu