Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

INgawa siamini Sana ulichotabiri
Ila nikupongeze kwa uchambuzi mzuri Sana wa kihstoria una kitu mkuu
Ana kitu !? Wewe unamjua huyo ,? Kweli jf now days ina watoto

Huyo ni complete package of intelligence wakati wa zama zao hili jukwaa na jukwaa la JI lilikuwa Lina shushwa nondo tu, watu tulikuwa tuna kimbilia jf kufuata madini , now days jf kumekuja kizazi kipays cha hovyo watu badala ya kubishana Kwa fact Wana bishana Kwa mihemko iliyokosa weledi
 
Tatizo ndio huwa linaanzia hapa.......yaani ile tarehe 7 wenyewe wanaona kama kafa kuku mwenye kideli.. yaani waislael walistahili kufa kitu ambacho hata umoja wa mataifa kupitia katibu wake amekaa kimyaa baada ya kuchagua upande........ndio msingi na ndio shida kubwa iliyopo hapa.......wale wanajeshi wa UN wanaona kabisa matukio na shida zote za hawa prox lakin wako tuli hata hawaonyeshi ushirikiano hata tu wa kukemea kwamba msitukalibie sisi sio ninyi .......yenyewe yako kimya kama yako kwenye kufatilia VAR ndio maana nyau nyau kasema wewe katibu wa UN usije tena islael sababu umechagua pa kupendelea.......na hamisha hawa mgambo wako la sivyo watakiona cha mtema kunde.......Israel yuko sawa kujitetea na palestine pia wako sawa kudai kipande chao ila hao prox ndio wanareta udini na kutaka kuiretea vurugu inchi ya Israel........kwa mguu wa dini. ........hitimisho langu ningefanya kama india vunja kira kitu ambacho hawa jamaa wanaamini na kukitumia katika inchi yangu ili nimalizane nao jumla .....mwisho
Mnamsingizia Antonio Gutteres bure tu. Binafsi nilisikiliza ile hotuba aliyoitoa mwaka jana 2023 baada ya tukio. Alisema kwamba kilichofanyika 7 October 2023, hakikuwa sahihi, japo ni lazima Wazayuni wa Israel wakubali kwamba ule mgogoro una mizizi mirefu.

Gutteres alichokisema ni kwamba matatizo yalianzia kwenye The Nakba mwaka 1948 ambapo Israel mbali na kuvamiwa na mataifa ya Kiarabu, waliamua kuanza kuua maelfu ya wapalestina na kuwafukuza kwao. Mbona hili hamtaki kulisema nyie mnakazana na 7 October 2023 ???

Hakuna yoyote yule anayesema Israel ifutiliwe mbali. Hizi ni kauli za kinazi na mihemko ya kidini ambayo washabiki wote wa Israel na Palestina mnayo. Huwa mnasikiliza kauli za Netanyahu, Nasrallah na Ayatollah na kuzimeza bila kufanya tafiti za kitaalamu mkisahau kwamba wale ni wanasiasa wenye utaifa mkali (Ultra-Nationalists).

Kuna Resolutions nyingi tu za UN ambazo zinataka Israel na Palestina wafuate mipaka ambayo ilikubaliwa na UN General Assembly, ili kutekeleza A TWO STATES SOLUTION ambapo, taifa moja litachukua East Jerusalem na jingine West Jerusalem.

Binafsi ile kauli ya Gilad Erdan kusema kwamba hotuba ya Gutteres ni BLOOD LIBEL huwa inanishangaza kwasababu, wamemuwekea mzee wa watu maneno. Gutteres anafanya kazi kwa kufuata miongozo mbalimbali ya kisheria ambayo ameikuta toka kwa watangulizi wake. Hilo la kusema anapendelea upande mmoja mnalitoa wapi ???

NB: Hotuba yake ni hii hapa akirudia alichokisema kuhusu 7 October.

View: https://youtu.be/y7ihLto-fV4
 
Naomba unifahamishe, Kwa Sasa, ni taifa gani Dogo linatishia mustakabali wa Dola kubwa ya US? Huo udogo unapimwa Kwa mambo gani?

Kama lengo ni "The balance of power", mara baada ya WWII, Kwa nini Dunia ilikubali US kuwa superpower? Dunia haikujua kwamba wanaokuwa vilanja wa Dunia mara nyingi ndiyo wanaokuwa chanzo Cha machafuko? Kwa nini Sasa hivi ndipo Kuna umuhimu wa kuwepo hiyo inayoitwa "The balance of power"?.

Kama balance of power itapatikana (au ipo) Kwa muktadha wa kutooneana; je, inamaana kwamba hakutakuja kupatikana superpower mwingine? Au machafuko mengine?

Superpower "the controller of world" .
Jinsi nilivyo pitia hii comment na thread yote ni wazi kwamba binaadamu kuikwepa vita ni ngumu kutokana na Tamaa aliyonayo ya kuwa na mamlaka na kulinda mamlaka aliyokuwa nayo , Inshort Dunia ni uwanja wa vita ilikuwa hivyo Ipo hivyo na itaendelea kuwa hivyo
 
Imepita miaka 79 tangu itokee vita baina ya mataifa makubwa, hivyo kimekuja kizazi kipya ambacho kinadhani amani ni haki yake tu, na kusahau dunia ilipotoka. Zamani watu walikuwa wakisikia Urusi kaweka silaha za nyuklia nchini Cuba walikuwa wanaogopa, siku hizi watu wanachagua upande na kushangilia.

Hata wanasiasa na wanadiplomasia wote walioishi kipindi cha vita ya pili ya dunia na vita baridi, walikuwa ni watu makini wanaofahamu madhara ya siasa za mlengo mkali. Hata kama walikuwa wanatetea maslahi ilikuwa ni lazima kuwe na mazungumzo na maelewano.

Marekani siku hizi haina wanasiasa kama Henry Kissinger, Zbigniew Brezhinski na George Kenan, ina watu kama Pompeo, Blinken na Tillerson ambao kiuhalisia ni kizazi chenye shida kidogo. Hili hata Prof Kishore Mahbubani aliwahi kulisema dhahiri kabisa.

Kizazi cha Baby Boomers, kama Putin, Trump, Jinping, Ayatollah, Netanyahu n.k wote hawakuiona vita ya pili ya dunia na waliishi nyakati za mwisho za vita baridi. Ila walau wangeshuhudia matukio kama The Siege of Leningrad, Invasion of Normandy na Bombing of Dresden ni lazima wangekuwa na uwogafulani hivi.
Mkuuu national nanga hebu njoo na kisa japo kwa ufupi tuoshe macho ni mambo gan haya dah watu mko deep
 
Umeongea mambo mengi sana bila kuweka ushahidi wowote, hili ni kosa. Chanzo chako kikubwa cha haya uliyoyasema hapa ndiyo kile tunaita TRUST ME BRO. Lakini pia umepinga hoja zangu bila kueleza dhahiri hoja yako ni ipi na wewe unasimama wapi (Your Points are Vague, and they lack veracity), japo ntajitahidi kuzijibu kwa ushahidi:

Mosi, taifa la Israel limeundwa mwaka 1948 na UNO kwa msaada mkubwa wa USA, USSR na Great Britain. Unaposema Israel na USA wamekutana njiani sielewi ulikuwa unamaanisha nini.

Pili, unaposema taifa la Israel linaweza kuendelea bila hata msaada wa USA au taifa lolote lile bila kuleta ushahidi wa kuthibitisha hoja yako ni udhaifu mwingine mkubwa wa hoja yako. USA anaisaidia Israel DIPLOMATICALLY, FINANCIALLY, TECHNOLOGICALLY and MILITARILY, na ni mtu mjinga tu ndiyo anaweza kupinga hili. Kila mwaka, USA anaipa Israel msaada wa USD 3.8 Billion kama msaada wa kijeshi.

Tatu, unaposema makampuni ya Israel yanafanya vizuri na yako kwenye Black Market, napata wasiwasi na uelewa wako wako wa uchumi. Hebu nitajie walau makampuni matano makubwa ya Israeli ambayo yanaweza kulinganishwa na yale Top Ten of Fortune 500.

Nne, Israel haijamsaidia USA kupata Misri. Marekani amekuwepo LEVANT hata kabla ya kuundwa Israel 1948. Ukisoma historia utafahamu kwamba, Middle East/Persian Gulf kushawahi toke THE IRAN CRISIS 1946, ambapo USA na USSR walikuwa wanagombania kutawala Iran baada ya WW2 kuisha. Harry Truman walivutana na Joseph Stalin hadi kupelekea USSR kuondoa vikosi vyake kule.

Wewe unaposema Israel ndiyo imemsaidia USA kuzipata nchi za Middle East umeliokota wapi, ilhali tunafahamu kwamba USA amekuwepo eneo hilo hata kabla ya Israel haijawa nchi ???
Kiongozi una nondo ww mpaka hapa kibaruani wananiona kituko mpe mpe huyu mpuuzi mmoja
 
...mfano kufeli kwa UMOJA WA MATAIFA...
Asante sana Mkuu kwa uzi wako
====
UN imeishafeli pakubwa....walikataa Africa kupewa kiti cha kudumu Baraza la Usalama!! Baada ya kuona Sasa Africa inakwenda kujiunga mazima na BRICS...eti ofisi ya Katibu Mkuu UN Sasa inaratibu Africa ipewe kiti hicho!!
===
Huko ni kufeli.
 
Kukupa kiti kwenye baraza la usalama hakukuengui kuingia BRICS

Russia na China wapo kote kote

Kuingia BRICS sio bara zima ni kila nchi inajiamulia yenyewe kuingia ama kutoingia
 
Kukupa kiti kwenye baraza la usalama
Ni kweli ulichokisema. Hata hivyo, bandiko langu limelenga umuhimu wa Vyombo hivi viwili vya kimataifa.

Baraza la Usalama la UN limekuwa chombo cha nchi za Magharibi kudhibiti nchi nyingine badala ya kusaidia nchi hizo nyingine! BRICS inatoa furusa sawa Kwa wote, kiasi cha kuonekana ni more relevant than UN Baraza la Usalama.
 
Taasisi ya UNITED NATIONS inakuwaje biased kwa Israel ilhali yenyewe ndiyo imeliunda taifa la Israel mwaka 1948 ???
Inapokuja Israel akalalamika kuhusu tatizo analolipitia au lililompata kuanzia Antonio guiteres alie katibu mkuu mpaka wanachama WA umoja WA mataifa wenye kinyongo na Israel (waarabu,,waafrika na baadhi WA ulaya) watapinga solutions anayoitaka Israel...Mfano UNRWA ambayo ni taasisi ya umoja WA mataifa wafanyakazi wake kutoka nchi za kiarabu walishiriki October 7 kuwaua wayahudi lakini hakuna kuwajibishwa Kwa hio taasisi kulikofanyika hata baada ya maombi ya Israel...Leo inaendelea na Kazi kama kawaida..... Baada ya Israel kuanzia kulipa kisasi sio mara moja au mbili kumepitishwa resolution ya kumtaka israel aondoke gaza pasipo hata kupata mateka wake... Resolution ya mwisho ni ya hivi karibuni ambayo hata Tanzania imepiga kura ya Israel aondoke gaza...Swali ni je mbona hawazingatii kuwapata mateka wa kiyahudi walio mikononi mwa wapalestina...Kadiri ya muda nitaboresha uandishi tuwe na sources za kutosha.
 
Walichokifanya Hamas mpaka sasa tunakiita WAR CRIME, ila ukiletwa ushahidi wa kitaalamu unaonesha INTENTION TO DESTROY JEWISH PEOPLE basi WAR CRIME itageuka na kuwa GENOCIDE.
Unaye muelimisha ni wale "wafia dini Israel nchi takatifu teule ya Mungu".... .hawezi kukubali huo ukweli unaomwambia .....
 
Mosi, taifa la Israel limeundwa mwaka 1948 na UNO kwa msaada mkubwa wa USA, USSR na Great Britain. Unaposema Israel na USA wamekutana njiani sielewie ulikuwa unamaanisha nini.
Ni Sawa kwamba Israel iliundwa tena na United nations mwaka 1948 Kwa resolution 181 na hao wote uliowataja Pamoja na mataifa mengine 30 yaliunga mkono Hilo azimio...Maana yangu kwamba Marekani na Israel wamekutana njiani ni Kwa sababu USA alikuwa reluctant kuikubali Israel kuwepo pale kwenye mipaka yake...Na Kwa mtazamo wangu alikubali Ile resolution kutokana na kukubaliwa na wenzie wengi.Na sababu ya hio reluctance ni mahusiano yake na mataifa ya kiarabu yasiomkubali israel akaona atapoteza marafiki wa kiarabu.Kwa hio ile israel kukubalika kabisa na kuwa mshirika mkubwa na trusted kwa marekani ilikuwa mpaka miaka ya 1972 chini ya Richard Nixon.

(Pili, unaposema taifa la Israel linaweza kuendelea bila hata msaada wa USA au taifa lolote lile bila kuleta ushahidi wa kuthibitisha hoja yako ni udhaifu mwingine mkubwa wa hoja yako. USA anaisaidia Israel DIPLOMATICALLY, FINANCIALLY, TECHNOLOGICALLY and MILITARILY, na ni mtu mjinga tu ndiyo anaweza kupinga hili. Kila mwaka, USA anaipa Israel msaada wa USD 3.8 Billion kama msaada wa kijeshi.)

Maana yangu ni Hii kwamba Israeli anayo nçhi tayari na wafanyabiashara wenye asili ya kiyahudi ni wengi Sana na wengine hufanya biashara zenye maslahi hata Kwa nchi Yao..Lakini wakijua hata kama watafukuzwa kama ilivyotokea Kwa ujerumani ya Nazi wanayo nchi Yao ya kukimbilia...USA anawapa Israel misaada ya kijeshi kutokana na Sera ya tokea wakati WA Richard Nixon qualitative military edge(QME)
Hii sio Sera ya faida Kwa Israel Tu hata Kwa Huyo USA inamfaidisha Zaidi.Usa kama akaamua kuwithdraw misaada Kwa Israel Israel ataweza kusurvive financially Kwa sababu anavyo vyanzo vingi ya income..Katika Nyanja zote wamepiga hatua kwenye innovation na entrepreneurship...Na watu wake walio ulaya ndio wenye viwanda,,makasino,,biashara za vinywaji na za vyakula na vyanzo vingine vingi vyenye maslahi hata kwa nchi yao ya israel.
Zaidi ninaamini hakuna nchi itaweza kurekebisha azimio namba 181 kuifanya Israel isiwe na uhalali WA kuwa nchi au kuiondoa kwenye mipaka yake hata Huyo USA.

Nne, Israel haijamsaidia USA kupata Misri. Marekani amekuwepo LEVANT hata kabla ya kuundwa Israel 1948. Ukisoma historia utafahamu kwamba, Middle East/Persian Gulf kushawahi toke THE IRAN CRISIS 1946, ambapo USA na USSR walikuwa wanagombania kutawala Iran baada ya WW2 kuisha. Harry Truman walivutana na Joseph Stalin hadi kupelekea USSR kuondoa vikosi vyake kule.
Hapa kuhusu Egypt ni kwamba Egypt alikuwa upande WA Soviet union Pamoja na mataifa mengi ya kiarabu ndio maana Silaha za vita ambazo nchi za kiarabu kama Syria,,Iraq,, Saudi na misri walizitumia kupigana na Israel walizipata Moscow ambaya ilikuwa kitovu cha USSR.Kwa hio Jeshi la Israel lilipoiteka miji ya misri Pamoja na kuwateka Askari wake 20,000 battalion moja na wakatishia kuwaua wale waarabu jangwani Anwar al Sadat alifanya concession,,alisign peace treaty na Israel,,akaitambua kama sovereign state na akakubali kujiondoa Katika ushirikiano wowote na USSR na akaanza kupokea misaada ya Marekani...Baada ya kuitambua Israel aliefuata ni Jordan...Saudi na washirika wake baadae walikuja kuwa pia washirika wa Marekani na wakaachana na misaada na influence ya Soviet union....

Kwa hio suala sio kuwepo middle east Kwa USA ila ni kuwa na influence na upper hand Kwa mataifa ya middle east Zaidi ya washindani WA Soviet Union.
 
Naomba tuweke historia sawa. Hekalu la Mfalme Suleiman liliteketezwa miaka ya 580KK na majeshi ya Mfalme Nebuchadnezzar. Hekalu lililoteketezwa na Titus ni la Zerubabeli ambalo likiboreshwa na Herod the Great. Hii ni historia
Ila watu wa dini flani watakwambia pale palikuwa na mosque sijui temple na mosque ni kitu kilekile?!
Mleta uzi katumia "Hekalu la Suleman" kwasababu kabla ya Suleman hapo mahali hapakua na jengo lolote; mjenzi wa kwanza alikua Suleman. Tuendelee kuelimika bila kuweka some sign of religious issues.
 
Ni Sawa kwamba Israel iliundwa tena na United nations mwaka 1948 Kwa resolution 181 na hao wote uliowataja Pamoja na mataifa mengine 30 yaliunga mkono Hilo azimio...Maana yangu kwamba Marekani na Israel wamekutana njiani ni Kwa sababu USA alikuwa reluctant kuikubali Israel kuwepo pale kwenye mipaka yake...Na Kwa mtazamo wangu alikubali Ile resolution kutokana na kukubaliwa na wenzie wengi.Na sababu ya hio reluctance ni mahusiano yake na mataifa ya kiarabu yasiomkubali israel akaona atapoteza marafiki wa kiarabu.Kwa hio ile israel kukubalika kabisa na kuwa mshirika mkubwa na trusted kwa marekani ilikuwa mpaka miaka ya 1972 chini ya Richard Nixon.

(Pili, unaposema taifa la Israel linaweza kuendelea bila hata msaada wa USA au taifa lolote lile bila kuleta ushahidi wa kuthibitisha hoja yako ni udhaifu mwingine mkubwa wa hoja yako. USA anaisaidia Israel DIPLOMATICALLY, FINANCIALLY, TECHNOLOGICALLY and MILITARILY, na ni mtu mjinga tu ndiyo anaweza kupinga hili. Kila mwaka, USA anaipa Israel msaada wa USD 3.8 Billion kama msaada wa kijeshi.)

Maana yangu ni Hii kwamba Israeli anayo nçhi tayari na wafanyabiashara wenye asili ya kiyahudi ni wengi Sana na wengine hufanya biashara zenye maslahi hata Kwa nchi Yao..Lakini wakijua hata kama watafukuzwa kama ilivyotokea Kwa ujerumani ya Nazi wanayo nchi Yao ya kukimbilia...USA anawapa Israel misaada ya kijeshi kutokana na Sera ya tokea wakati WA Richard Nixon qualitative military edge(QME)
Hii sio Sera ya faida Kwa Israel Tu hata Kwa Huyo USA inamfaidisha Zaidi.Usa kama akaamua kuwithdraw misaada Kwa Israel Israel ataweza kusurvive financially Kwa sababu anavyo vyanzo vingi ya income..Katika Nyanja zote wamepiga hatua kwenye innovation na entrepreneurship...Na watu wake walio ulaya ndio wenye viwanda,,makasino,,biashara za vinywaji na za vyakula na vyanzo vingine vingi vyenye maslahi hata kwa nchi yao ya israel.
Zaidi ninaamini hakuna nchi itaweza kurekebisha azimio namba 181 kuifanya Israel isiwe na uhalali WA kuwa nchi au kuiondoa kwenye mipaka yake hata Huyo USA.

Hapa kuhusu Egypt ni kwamba Egypt alikuwa upande WA Soviet union Pamoja na mataifa mengi ya kiarabu ndio maana Silaha za vita ambazo nchi za kiarabu kama Syria,,Iraq,, Saudi na misri walizitumia kupigana na Israel walizipata Moscow ambaya ilikuwa kitovu cha USSR.Kwa hio Jeshi la Israel lilipoiteka miji ya misri Pamoja na kuwateka Askari wake 20,000 battalion moja na wakatishia kuwaua wale waarabu jangwani Anwar al Sadat alifanya concession,,alisign peace treaty na Israel,,akaitambua kama sovereign state na akakubali kujiondoa Katika ushirikiano wowote na USSR na akaanza kupokea misaada ya Marekani...Baada ya kuitambua Israel aliefuata ni Jordan...Saudi na washirika wake baadae walikuja kuwa pia washirika wa Marekani na wakaachana na misaada na influence ya Soviet union....

Kwa hio suala sio kuwepo middle east Kwa USA ila ni kuwa na influence na upper hand Kwa mataifa ya middle east Zaidi ya washindani WA Soviet Union.
Hongera sana, umeongea kitaalamu hadi nimefurahi. Nikimaliza majukumu nitarudi tuendelee na mjadala wetu.
 
Back
Top Bottom