Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Kila mmoja anajihesabia haki ndio sababu vita haiishi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila mmoja anajihesabia haki ndio sababu vita haiishi.
Bahati mbaya wenye tabia hizo sio hao watoto unao wasema bali ni watu wazima na mbaya zaidi ni wanajiita wasomi.Changamoto sana humu watoto wamejaa sasa hivi napata uvivu
Kwahiyo hao ni rahisi kupress button vita vipiganwe?? Hawana imani na maridhianoImepita miaka 79 tangu itokee vita baina ya mataifa makubwa, hivyo kimekuja kizazi kipya ambacho kinadhani amani ni haki yake tu, na kusahau dunia ilipotoka. Zamani watu walikuwa wakisikia Urusi kaweka silaha za nyuklia nchini Cuba walikuwa wanaogopa, siku hizi watu wanachagua upande na kushangilia.
Hata wanasiasa na wanadiplomasia wote walioishi kipindi cha vita ya pili ya dunia na vita baridi, walikuwa ni watu makini wanaofahamu madhara ya siasa za mlengo mkali. Hata kama walikuwa wanatetea maslahi ilikuwa ni lazima kuwe na mazungumzo na maelewano.
Marekani siku hizi haina wanasiasa kama Henry Kissinger, Zbigniew Brezhinski na George Kenan, ina watu kama Pompeo, Blinken na Tillerson ambao kiuhalisia ni kizazi chenye shida kidogo. Hili hata Prof Kishore Mahbubani aliwahi kulisema dhahiri kabisa.
Kizazi cha Baby Boomers, kama Putin, Trump, Jinping, Ayatollah, Netanyahu n.k wote hawakuiona vita ya pili ya dunia na waliishi nyakati za mwisho za vita baridi. Ila walau wangeshuhudia matukio kama The Siege of Leningrad, Invasion of Normandy na Bombing of Dresden ni lazima wangekuwa na uwoga fulani hivi.
Kama umemjua leo umechelewa sanaINgawa siamini Sana ulichotabiri
Ila nikupongeze kwa uchambuzi mzuri Sana wa kihstoria una kitu mkuu
Kwahiyo hao ni rahisi kupress button vita vipiganwe?? Hawana imani na maridhiano
Mkuu MALCOM LUMUMBA maana ya andiko hili ni kwamba USA tutegemee kuporomoka kiuchumi na Uchina kupanda?
Wengi huzungumzia huo mgogoro kidini na mahaba ya dini yakizidi tegemea matusi na kufedheheshana mbele.Asante Sana ndg MALCOM LUMUMBA . Hizi ndo brain zinazotakiwa kuleta mada za kujadiliwa humu.
Humu wengi huwa wanaleta mada bila kushirikisha Ubungo Kwa kiwango kinachotakiwa na matokeo yake tunaishia kuwa Machawa wa tusiyoyajua na yasiyotuhusu.
Asante sana mkuu nimekuelewaHapana, jibu siyo rahisi kwasababu POLITICS ARE BINARY AND UBIQUITOUS, NOT ONE WAY TRAFFIC. Unaweza kukuta Marekani akapanda kiuchumi pamoja na kushinda vita vilevile, kinyume na ambavyo wengi tunategemea. Unakumbuka kilichotokea Urusi, mbali na maelfu ya vikwazo baada ya kuvamia Ukraine ??? Urusi ilipanda na mpaka leo iko tu.
Japo, Conventional Wisdom inasema hivi: Endapo Ikitokea vita in The Persian Gulf dunia nzima itaguswa kama ilivyoguswa kwenye vita ya Ukraine. Hasahasa mataifa madogo kama sisi ambayo hayazalishi bali ni Net Importers. Wote tutatembea kwa mguu kutoka Mbezi hadi Kariakoo kwasababu mafuta yatakuwa ni bidhaa ya anasa.
Jambo la kujiuliza ni hili: Unadhani Israeli, taifa lenye watu milioni 9 linaweza kufanya vita dhidi ya Iran, taifa lenye watu takriban milioni 90 bila msaada wa Marekani ???
Kupambana vita ni rahisi sana, changamoto kubwa inakuja kwenye kufanya kitu kinaitwa OCCUPATION. Ili Israel ashinde vita dhidi ya Iran, mbali na kuipiga ni lazima afanya OCCUPATION kuhakikisha anaondoa kabisa mfumo wa kiislamu uliozaliwa na kujengwa tokea mapinduzi ya 1979.
Hili lilifanyika Ujerumani baada ya 1945, ambapo iligawanywa vipande vinne (Occupation Zones) na kimoja kikashikiliwa na Marekani, kimoja Muingereza, Kimoja USSR na kimoja Mfaransa ili kuhakikisha wanazi hawajipangi tena. Kufanya OCCUPATION siyo rahisi ndiyo maana Marekani ameondoka Afghanistan nchi yenye watu milioni 41, baada ya takribani miaka 20 kwenye nchi hiyo.
Unadhani Iran kwenye watu takribani milioni 90 wataweza kufanya kama walivyofanya Afghanistan na Iraq ??? Iraq tu ilizalisha makundi kama ISIL/DAESH, unadhani Iran itazalisha makundi ya namna gani kutokana na POWER VACUUM itakayotengenezwa baada ya kuwaondoa kina Ayatollah ??
NB 1: NAZIs walipigana vita vizuri, ila OCCUPATION ya Poland, Ukraine na Russia zikawashinda, hivyo ili kupunguza gharama ya kutunza watu na kupata resistance kama kule Ufaransa, wakaanza kupeleka watu CONCENTRATION CAMPS na kufanya MASS EXTERMINATION.
NB 2: GAZA imeonesha ni gharama kufanya OCCUPATION, ndiyo maana waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon aliamua kuondoa vikosi mwaka 2005. Sasa ili kuzuia Hamas nyingine isizaliwe, njia ambayo Israeli itabidi atumia ni ile ya Ujerumani, Marekani na Australia, ya kuua wenyeji na kuwafukuzia mbali (Ethnic Cleansing, Extermination and Genocide)
Kwa mtazamo wako mkuu mauaji ya Gaza unayachukuliajeAndiko zuri lakini naona kama umeweka utangulizi mrefu sana ili kuficha hoja yako mwishoni “Gaza Genocide”.
Gaza genocide ni neno lililoibuliwa na South Africa na kubebwa na Al Jazeera kama sehemu ya kuizuia Isreal kuendelea kuwasaka Hamas huko Gaza na sasa Hezbollah huko Lebanon.
Pamoja na historia nzuri uliyoleta lakini hoja ya Gaza genocide imeharibu kila kitu logically kwani ukweli ukichanganywa na uongo unakuwa uongo.
Naomba tuweke historia sawa. Hekalu la Mfalme Suleiman liliteketezwa miaka ya 580KK na majeshi ya Mfalme Nebuchadnezzar. Hekalu lililoteketezwa na Titus ni la Zerubabeli ambalo likiboreshwa na Herod the Great. Hii ni historiaNaomba kuuliza tu: Nini kilipelekea matukio ya October 7 ????
=======================================================
Lakini pia kumbuka hili: Wakati Ufalme wa Judea, unapambana na Warumi mwaka 70 A.D kule kwenye ngome ya MATSADA, Wayahudi wengi wenye msimamo mkali waliamini kwamba hawewezi kushindwa vita, hivyo wakaamua kufanya uasi dhidi ya Warumi.
Jenerali Titus na baba yake Kaisari Vespasian waliwpiga vibaya mno Wayahudi. Walivunja ngome ya MATSADA na kuteketeza hekalu la Mfalme Suleimani na kuua maelfu ya Wayahudi ambao wengi walikimbilia Asia, Afrika na Ulaya. Halafu nchi ya Yudea wakaibadilisha jina na kuiita Ufilisti na kuwapa maadui wa Israeli waliokuwa wanaishi pale.
Mwisho kabisa : Mwaka 1914, Austro-Hungary na Ujerumani waliamini kwamba hawewezi kushindwa vita na taifa lolote Ulaya, kwasababu haki yao ya kutawala wengine ni Divine
==============================================
Swali langu kwako mkuu: Mwisho wa haya yote utakuwa ni upi ?
Andiko zuri lakini naona kama umeweka utangulizi mrefu sana ili kuficha hoja yako mwishoni “Gaza Genocide”.
Gaza genocide ni neno lililoibuliwa na South Africa na kubebwa na Al Jazeera kama sehemu ya kuizuia Isreal kuendelea kuwasaka Hamas huko Gaza na sasa Hezbollah huko Lebanon.
Pamoja na historia nzuri uliyoleta lakini hoja ya Gaza genocide imeharibu kila kitu logically kwani ukweli ukichanganywa na uongo unakuwa uongo.
Huo ni uoni wako hafifu unaotokana na udini na upofu uliokujaa. Hakuna mwenye akili timamu asiyeona genocide inayofanywa na Wazayuni waliyojificha kwenye koti la Uisraeli.Andiko zuri lakini naona kama umeweka utangulizi mrefu sana ili kuficha hoja yako mwishoni “Gaza Genocide”.
Gaza genocide ni neno lililoibuliwa na South Africa na kubebwa na Al Jazeera kama sehemu ya kuizuia Isreal kuendelea kuwasaka Hamas huko Gaza na sasa Hezbollah huko Lebanon.
Pamoja na historia nzuri uliyoleta lakini hoja ya Gaza genocide imeharibu kila kitu logically kwani ukweli ukichanganywa na uongo unakuwa uongo.