Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

Mwamba wewe ni undisputed kwenye historia na evidence , hongera sana
Kuna nyakati huwa naogopa kujadili na wewe nabakia kuwa msomaji tu
 
Leo nimepata wasaa, walau niandike mawili matatu kuhusu hoja yako:

Mosi, umeingia kwenye kitu kiitwacho The Fallacy of Generalization, ambapo unaamika kwamba kila ni Myahudi ni Muisraeli, na kila Myahudi ni Mzayuni. Hii siyo sawa hata kidogo. Siyo kila Myahudi ni Muisraeli, maana kuna maelfu ya Wayahudi ambao ni raia wa Marekani, Ukraine, Urusi, Iran, Uingereza n.k. Pia, siyo kila Myahudi ni Mzayuni ambaye anaunga mkono siasa za Israel kule Palestina.

Hivyo kuwataja diaspora wa Kiyahudi na kuwaambatanisha na taifa la Israeli ambalo ni la Kizayuni, siyo sahihi hata kidogo. Kitaalamu tunasema "You Put People in a Monolith" jambo ambalo siyo sahihi. Mwaka 1920, Winston Churchill kwenye gazeti liitwalo The Sunday Herald (London), aliandika makala ndefu iitwayo "ZIONISM vs BOLSHEVISM: A STRUGLE FOR THE SOUL OF THE JEWISH PEOPLS"

Mle ndani aliandika kitu cha msingi sana, ambapo alisema falsafa kubwa mbili ambazo ziko Ulaya na kuasisiwa na Wayahudi ni zile za Uzayuni na Ukomunisti. Wayahudi baadhi kama Lenin na Trotsky ni Wakomunisti na hawaamini kabisa katika kurudi Palestina na walitaka mapinduzi ya kijamaa ya dunia nzima, huku baadhi kama Theodor Herzl na Max Bodenheimer walikuwa wanaamini katika kutengeneza taifa maalumu kwa ajili ya Wayahudi peke yao.

Haya makundi mawili yalikuwa mahasimu na yalivutana, huku Wayahudi wa Urusi kama Trotsky walikuwa hawataki kabisa kusikia jambo linaloitwa JEWISH NATIONALISM, jambo lililopelekea Wayahudi wengi kuuwawa bila hatia. Mbali na haya makundi, kuna maelfu ya Wayahudi ambao hawakufungamana na UZAYUNI wala UKOMUNISTI, wao ni wafuasi wa dini ya kiyahudi (JUDAISM).

Unapo kwamba kwasababu kuna mabilionea kadhaa wa Kiyahudi nchini Urusi, Marekani na Uingereza basi moja kwa moja fedha zao ni mali ya Israeli na Serikali yake. Huoni hapa kwamba hoja yako inakosa mantiki ??

Unachokisema hapa, hakina utofauti na kusema Singapore ni sehemu ya Uchina kwasababu tu, asimilia zaidi ya 50% ya wananchi ni Ethnic Chinese (Hakkas) na wanafuata dini na falsafa asilia za Asia kama Buddhism, Shamanism, Confucianism, Taoism n.k

Hii Fallacy of Generalization uliyoileta hapa ni moja ya sababu kubwa za kuchochea chuki na uonevu dhidi ya Wayahudi, ANTI-SEMITISM. Kwamba kwasababu Wayahudi ni kitu kimoja basi, kosa likifanywa na mmoja tu, duniani kote wayahudi waadhibiwe, watengwe na hata kuuwawa kwasababu ya makosa ya wahuni wachache kama Netanyahu, Ariel Sharon, Harvey Weinstein, Lenin, Trotsky n.k

Hii hapa chini ni video ya Msomi wa dini ya Kiyahudi, Rabbi Shapiro akikemea dhana nzima ya kulazimisha kusema kwamba ZIONISM IS JUDAISM. Hebu msikilize vizuri halafu utaelewa nini nachokizungumzia hapa:

View: https://youtu.be/JXS9bYuq3zU

Prof, Mahmood Mamdani kwenye kitabu chake "GOOD MUSLIM, BAD MUSLIM: AMERICA, COLD-WAR AND THE ROOTS OF TERROR" anazungumzia madhara ya kuwaweka watu kwenye kundi moja kama bidhaa. Akasema hivi kwenye mambo yote ya kisiasa ukizoea kuweka watu kwenye kundi moja "Putting People in a Monolith" kuna sehemu utajikuta unawanyima haki wanaostahili na unawapa haki wale wasiostahili.

Katika siasa za dunia, sehemu moja tu ambayo tunatakiwa kuwaweka watu wote kwenye kundi moja ni kwenye ENJOYMENT OF HUMAN RIGHTS. Mfano, leo hii hata wakitokea watu wawili tu ambao wanadai uhuru "RIGHT TO SELF DETERMINATION" kutoka kwa wakoloni au utaifa kwa kujitoa kwenye kubwa linalowabagua na kuwakandamiza kama ilivyokuwa kule Sudan Kusini, basi hao wachache watahesabiwa kuwawakilisha wengi. Japo hata hii hoja nayo ina ukakasi mwingi.

Leo hii, ukisema kabila la WAHAYA wana tabia fulani, ukiwachunguza sana utafahamu hata wao wenyewe mle ndani wana makundi tofauti-tofauti yenye tabia zake na hawapikiki chungu kimoja. Hili aliwahi kulinukuu Mwalimu JK Nyerere mwaka 1995 kwenye Uchaguzi Mkuu alipokuwa anakosoa siasa za kikabila. Hili wazo Mwalimu Nyerere alilotoa kwa mwanafalsafa wa Uingereza aitwaye Prof Charles Allen, aliyekuwa anawakosoa wasomi wa Kijerumani kama Prof Carl Friedrich Von Savigny ambao waliamini kwenye kitu kiitwacho The Collective Consciousness of the People.

==============================================

Pili, ushahidi wa kihistoria unaonesha kwamba Marekani amekuwepo Misri bila hata msaada wa Israel kama ulivyonieleza. Mwaka 1956-1957, ulitokea mgogoro wa Suez (Suez Canal Crisis) ambapo Raisi wa Misri, Gamal Nasser aliamua kutaifisha mfereji wa Suez ambao unamilikiwa na Ufaransa na Uingereza. Ufaransa, Uingereza na Israel wakaandaa mpango wa pamoja kumtwanga Misri kijeshi.

Aliyemsaidia Misri asitandikwe na haya mataifa matatu ni Marekani. Raisi wa Marekani, General Eisenhower alipiga simu kwa viongozi wa hizi nchi tatu (David Ben Gurion, Anthony Eden na Rene Coty) na kuwapiga mkwara mzito kwamba wakiendeleza vita atavuruga chumi za Uingereza, Ufaransa na Israel ndani ya muda mfupi na kuwalima vikwazo. Uingereza, Ufaransa na Israel wakafyata mikia na kuacha uvamizi huo, huku Waziri Mkuu wa Uingereza akijiuzulu kwa aibu.

Hivyo huwa nawashangaa mno watu wanapopiga Propaganda kwamba Israel au nchi nyingine yoyote ya NATO inaweza ikafanya jambo lolote kubwa bila ruhusa ya Marekani. Kiufupi, ukweli mchungu ni huu: Bila Marekani hakuna NATO, ISRAEL, JAPAN, TAIWAN wala SOUTH-KOREA. Mataifa kama Urusi na Uchina yangefanya vurugu kubwa mno kule Ulaya na Asia.


======================================================

Tatu, kuhusu Misri kununua silaha za Urusi, nachelea kabisa kusema hii hija yako ni nyepesi isiyo na mashiko. Misri chini ya Gamal Nasser ilikuwa na misimamo mikali lakini lilikuwa siyo taifa la kikomunisti kama ambavyo Czechoslovakia na Romania ambayo yalikuwa hayashirikiana kabisa na Magharibi.

Mradi mkubwa wa bwawa la Aswan (ASWAN HIGH DAM) ambao ulileta mapinduzi ya nishati nchini Misri ulianza kufadhiliwa na serikali ya Marekani miaka ya 50's kabla hawajavurundana na kuahidi kuipa Misri mkopo wa zaidi ya dola milioni 200. Unaposema Israel ndiyo imeisaidia Marekani Middle-East unamaanisha kusema kwamba, bila kuwepo Israel Marekani isingekuwa na ushawishi ukanda ule ???

Hii hapa chini ni Video ya Raisi Biden, akiwa Senator wakati huo, ambapo aliweka wazi kabisa kwamba taifa la ISRAEL ni uwekezaji mkubwa wa USA unaoleta faida kubwa kwa taifa hilo. Akaenda mbali zaidi na kusema hata ISRAEL isingekuwepo, USA ingelazimika kutengeneza ISRAEL nyingine. Hebu angalia hapa mwenyewe:

View: https://youtu.be/86Nrv5izaTs
NB: Huwa napata shida mno napoona watu wanakomaa kusema kwamba bila ISRAEL, USA isingekuwepo. Nachelea kusema hizo ni Propaganda hatari mno za Kikristo na Kizayuni ambazo msingi wake uko kwenye siasa.
 
NB: Huwa napata shida mno napoona watu wanakomaa kusema kwamba bila ISRAEL, USA isingekuwepo. Nachelea kusema hizo ni Propaganda hatari mno za Kikristo na Kizayuni ambazo msingi wake uko kwenye siasa.
Nimependa sana hapa ulivyomalizia. Ni ukweli mtupu kwamba hata siku moja mfinyanzi hawezi kuwa matokeo ya kazi ya chungu bali chungu ndo matokeo ya kazi ya mfinyanzi. USA ndiye Mfinyanzi wa Israel.
 
Nimependa sana hapa ulivyomalizia. Ni ukweli mtupu kwamba hata siku moja mfinyanzi hawezi kuwa matokeo ya kazi ya chungu bali chungu ndo matokeo ya kazi ya mfinyanzi. USA ndiye Mfinyanzi wa Israel.
Kuna kitabu kinaitwa "How To Hide An Empire: The History of Greater United State" by Daniel Immerwahr, kinaelezea kwamba USA alikuwa ana makoloni mengi tu duniani tokea karne ya 19, sema dunia ilikuwa imekazana kuangalia Europe ikasahau kumuangalia Marekani kwasababu yeye alikuwa anatawala kwa njia ya tofauti na wenzake.

Kiufupi ukisoma vizuri historia ya Marekani, utafahamu kwamba yeye anatawala kupitia Satellite States ambazo ni Sovereign. Mfano, Far-East Asia anatumia Japan na South-Korea. Middle-East anatumia Israel na Saudi Arabia, Europe anatumia Germany na UK, hapa Afrika alikuwa na Morocco, Egypt na South Afrika ya Makabulu chini ya mwamvuli wa The Safari Club.

Kiufupi haya mataifa yote tajwa uchumi, ulinzi na siasa zao zimefungamanishwa mno na Marekani kupitia milango ya nyuma ya taasisi kubwa za kimataifa kama The EU, NATO, Council on Foreign Relations, The Club of Rome, IMF, WB, IBS, The Five Eyes ambazo viongozi wake wengi (Elites) wanaandaliwa kwenye taasisi kubwa za elimu za kiliberali kama Harvard University, Oxford University, Cambrigde University na vyuo vingine vya Europe ambavyo hutegemea American Intellectual Expertise.

Dr Kwame Nkrumah alivyozungumzia Neo-Colonialism na kutaja sifa zake ambazo zineonekana leo, namvulia kofia na kusema kwamba yule Mzee alikuwa nabii ambaye alikosa heshima nyumbani kwao. He was too way ahead of his time. Lakini, naamini hakuna msomi hapa Afrika aliyewafahamu vizuri USA na michezo yao kama Nkrumah.
 
Mkuu asante sana kwa michango yako na muda wako.
Wengine tunaendelea kukuombea sana kwa huo moyo ulionao wa kugawa kile unachokijua. Mungu wa Mbinguni akubariki pamoja na familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…