Umoja wa Mataifa (UN) wapiga kura kupitisha ramani mpya ya dunia ili kuonyesha ukubwa halisi wa Afrika

Waafrika wamafanikiwa katika kampeni Yao kutaka ramani ya Dunia ichorwe upya ikioneha Ukubwa Halisi wa bara la Afrika.

Ramani ya Dunia ilivyokua ikitumika siku zote ilionesha bara la Afrika kuwa ni dogo kuliko Greenland, Sasa sijui hii ikitokea Kwa bahati mbaya au kwa makusudi

WAJUMBE wa umoja wa mataifa wanaohusika na mambo hayo walipiga kura kuridhia kutumika kwa ramani mpya ya Dunia ikionesha ukubwa Halisi wa bara la Afrika, nchi zote zilizoshiriki kikao hicho zilipiga kura ya kukubali ramani mpya kasoro nchi moja TU ndio ilikataa. Nchi hiyo ni Marekani.

Imeonekana kwamba ukubwa wa bara la Afrika unaweza kuzimeza nchi za Marekani, China, India na Ulaya na nafasi ikabaki.

Naomba wadau mnaojua mambo haya ni Kwa Nini walikua wanadogosha ukubwa wa bara la Afrika,Kuna faida gani walikua wanapata,au ni bahati mbaya TU?

Na baada ya UN kukubali kutumika kwa ramani mpya je ni faida gani Afrika itapata?

1788694385601.png
 
Umoja wa Mataifa umepiga kura ya kupitisha ramani mpya rasmi ya dunia iliyobuniwa kuonyesha ukubwa halisi wa kijiografia wa bara la Afrika na maeneo mengine ya kanda ya ikweta.

Mabadiliko haya yanalenga kuchukua nafasi ya "Mercator projection" (ramani ya kale ya Mercator), ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu lakini imekuwa ikikosolewa kwa kupotosha vipimo—ikionyesha maeneo ya kaskazini mwa dunia (kama vile Ulaya na Marekani ya Kaskazini) kuwa makubwa zaidi kuliko yalivyo, huku ikipunguza ukubwa wa bara la Afrika na maeneo mengine ya kusini.

Ingawa nchi kama Marekani zilipinga mabadiliko haya, kura hiyo ya UN inalenga kuleta uwakilishi wa kijiografia wenye usawa na unaoonyesha ukweli wa ukubwa wa maeneo duniani.

View attachment 3663525View attachment 3663526
Kweli nchi yetu Mjerumani alicheza mchezo mkali ukiangalia tu ramani ya Africa unajua iko wapi, imezungukwa na maziwa makubwa matatu; Victoria, Tanganyika na Nyasa.
 
cha ajabu leo hii nchi za kiafrika ikiwemo tanzagiza pia zinaruhusiwa chini ya agoa ku-export goods to the USA bila ya kodi, i.e tuna tarif free export of goods to the USA market hizi kodi za USA zinazoliza dunia nzima tarifs za Trump nchi za kiafrika (sub- sahara) zimesamehewa, haulipii chochote ku-export products zako USA na USA ndiyo soko kubwa la bidhaa duniani ambalo kila nchi inaligombania lkn wanapigwa kodi sisi ni free na Trump amesha renew lkn hausikii chochote upande wa afrika kimya badala ya kukaa kujipanga jinsi ya kunufaika wako kwenye mambo yasiyo na maana.
sasa ramani sijui inayoonyesha afrika kubwa inakusaidia nini labda kwenye kuzalisha ajira? sana sana inazidi kukuchoresha tu inaonekana big continent but the poorest na halina mchango wowote wa maana kwenye world economy.

exports create emplyment na kujenga middle class na siyo ujinga, dhuluma, utapeli na wizi wa mafremu ya gsm ...
Hayo ni mambo magumu kwa vichwa vya waafrika; si unaona Afrika inafanya vyema sana ktk kuiba uchaguzi, kuteka, kuua, n.k wanaotishia 'amani'.

Karne ya 21, ngozi nyeusi ikiwa kwenye ardhi yake anamwibia mwafrika mwenzake, anaenda kuficha Ulaya au kwa mwafrika mwenzake - mwizi, ambako anadhulumiwa
 
Kweli nchi yetu Mjerumani alicheza mchezo mkali ukiangalia tu ramani ya Africa unajua iko wapi, imezungukwa na maziwa makubwa matatu; Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Na raia walio km chache kutoka kwenye hayo maziwa hawana maji safi na salama tangu kuumbwa ulimwengu.

Yaani Arabuni wanasafisha maji ya bahari kwa gharama kubwa, Mtanzania anashindwa kutoka maji toka ziwa Tanganyika kwa pampu isiyozidi 2, kuyatibu na kuwapatia wanakijiji - ambao watalipia kupitia tozo.

Inafikirisha sana!
 
cha ajabu leo hii nchi za kiafrika ikiwemo tanzagiza pia zinaruhusiwa chini ya agoa ku-export goods to the USA bila ya kodi, i.e tuna tarif free export of goods to the USA market hizi kodi za USA zinazoliza dunia nzima tarifs za Trump nchi za kiafrika (sub- sahara) zimesamehewa, haulipii chochote ku-export products zako USA na USA ndiyo soko kubwa la bidhaa duniani ambalo kila nchi inaligombania lkn wanapigwa kodi sisi ni free na Trump amesha renew lkn hausikii chochote upande wa afrika kimya badala ya kukaa kujipanga jinsi ya kunufaika wako kwenye mambo yasiyo na maana.
sasa ramani sijui inayoonyesha afrika kubwa inakusaidia nini labda kwenye kuzalisha ajira? sana sana inazidi kukuchoresha tu inaonekana big continent but the poorest na halina mchango wowote wa maana kwenye world economy.

exports create emplyment na kujenga middle class na siyo ujinga, dhuluma, utapeli na wizi wa mafremu ya gsm ...
Mafrem ya GSM.
 
mkuu elimu muhimu hao wanao sahihisha raman sio wajinga maendeleo ya tech kuanzia ngazi ya ai inahitaji raman sahihi raman ikiwa inamakosa nayo ai nayo uwenda zikafanya makosa na pakazuka balaa ambalo ujawahi fikilia wewe uwezi ona manufaa ya raman kwa sababu upo tz tech iko chini hata vituo vya setelait czan kama vio hapa iyo raman mpya inamanufaa kwao japo wewe uyaon direct tech inakua cku za mbele ai zinaweza endesha hata ndege
 
aliletea hii ishu ni raisi wa togo akaipelka au, au wakailivalia njuga mpaka un, ktk mambo yooote yanayoisumbua afrika na wala siyo mambo ya ai, ni togo ndiyo ndiyo walioanzisha ...
 
Back
Top Bottom