kwasababu ni kiongozi wa dini na amenizidi umri, naomba nitofautiane naye kwa heshima, kila alichoongea ni story za vijiweni, wamedanganywa sana na wasikilizaji wake wanaendelea kuaminishwa uongo mkubwa sana. huyu shehe ni kama anatajiru kuwaaminisha watu kuwa wayahudi halisi ni Falasha wa Ethiopia. naomba nimweleweshe kwamba hao ni mojawapo tu ya wayahudi, ial hata hao waliopo israel ni wayahudi kweli.
Falasha au kwa jina lingine BETA-ISRAEL, ni wayahudi weusi waliotokana na kizazi cha Mfalme suleiman kuzaa na mkushi/muethiopia aliyekuwa malkia, Biblia inaeleza kwamba Malkia huyo wa Kush alimtembelea Suleimani na alikuwa mzuri sana, na suleiman kwa historia iliyopo hakumwacha salama, alilala naye hivyo malkia alivyorudi Africa alirudi na mimba. icho ndio kizazi cha Wayahudi weuzi wa Ethiopia na sio wote, ni wachache tu na wote walikuwa wanajitambua na wamekuwa wakiabudu uyahudi tangu enzi. Ethiopia ina makabial mengi, mfano, kuna OROMO, kuna TIGRAY, kuna HOSANA na wengine, wote wanatambuana hivyo hata hawa beta israel walikuwa wanajitambua kama distinct tribe ambayo mbegu yao ilitoka israel.
kwa habari ya Wayahudi, hata kwenye Biblia ipo wazi, mfano, Biblia inaeleza mwonekano wa Daudi kipindi kile anaenda kupakwa mafuta na alipoenda kupigana na Goliati na baadaye Sauli, kuwa alikuwa kijana mzuri mwekundu, hivyo hakuwa mweusi, alikuwa mzungu mwekundu kama hao watu wa iraq n.k. hakuwa mweusi, waisrael halisi ukiondoa ile mbegu sulemani aliweka kwa malkia wa sheba/kushi sio weusi kama sisi, ni weupe tangu enzi zote. sasa baada ya kuchukuliwa uhamishoni Babeli na kwengine (mfano tunakumbuka jinsi walivyochukuliwa uhamishoni Iran na Iraq, soma kitabu cha Esta story za Esta na Modekai, na kitabu cha Jeremia), walizaliana uko walikoenda. hao ashkenaz anaowasema ni wayahudi waliochanganywa na damu ya wazungu wa ulaya, na ni kawaida kuchangamana damu kwani myahudi akioa mzungu mwingine si atazaa mtoto? yule mtoto hatakua myahudi? na si atakuwa chotara fulani wa kizungu na kiyahudi?
kote wayahudi wameenda wamezaa na wazawa, africa tu hawakuja ila wangekuja wangezaa na wazawa na tungekuwa na kipande kingine cha wayahudi weusi ukiondoa wala falasha/beta israel ambao majority wameshapelekwa israel. pia mheshimiwa shehe angetusaidia kujua kama haya hapa chini ni ya kweli au uongo na kama ya kweli, ile ardhi ni ya nani?
1. Yesu Kristo alikuwa myahudi aliyeishi nchi ya kiyahudi, mji wake ulikua Nazareth ambao ni mkoa ndani ya Israel. sasaivi.
2. Mfalme Daudi alikuwa Mfalme wa Waisrael, na alijenga mji wa hebron (ambako kunatawaliwa na wapalestina) na Yerusalem, vipo hadi leo.
3. Mfalme suleiman alijenga hekalu, likaja kubomolewa pale Yerusalemu, bahati mbaya walisahau kubumoa lote, wakaacha baadhi ya kuta zipo hadi leo, ndio ule ukuta wa maombolezo wayahudi hua wanaenda kuombolezea upo hadi leo.
4. karubi la mariam mamake Yesu, karubi la Absalom mtoto wa Mfalme Daudi aliyetaka kumpindua babake na karubi la Daudi, lipo hadi leo. hao wote walikuwa waisrael.
5. miji yote ya israel imetajwa kwenye Biblia kama miji ya waisrael, na ipo hadi leo. mfano, Kapernaumu, Yafa, Yerusalem, Nazareth, Galilaya na kadhalika.
6. upo ushahidi mwingine mwingi sana.