Umoja wa Ulaya: Afrika iungane na dunia yote kuipinga Urusi

EU kupitia wanachama wenye ushawishi , kwa kuanzia waanzishe mchakato ili baadhi ya Nchi wanachama wa UN hasa nchi za Afrika zipate nafasi kuamua baadhi ya masuala ya kiusalama kupitia kura ya veto.
Lakini waangalie namna nyingine ya mfumo wa uendeshaji wa sera na mifumo ya kulinda Amani ya Dunia.
Ingelipendeza sana UN ingelibadilishwa kukidhi Dunia ya leo na kuundwa chombo kimoja kitakachoondoa jumuiya za Kibara na Kikanda bila kuathiri Sovereignty za Nchi husika.
 
Mi Bado siamini kama hatujawaunga mkono,Sijasikia mwanasiasa yeyote au kiongozi akiongelea hili ingawa wananchi wanaonesha msimamo....Halafu kwa nn Hili Tangazo wamekuja kulitolea huku kwetu inatia mashaka sana. Ngoja tusikie...
 
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuendelea kulaani kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine na kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi.

Tamko hilo limetolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

Wakizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, leo Jumanne Machi 22, 2022 mabalozi hao wa Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uholanzi, Sweden, Finland, Hispania, Italia na Balozi wa EU wamesema kuwa vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake wote wanaojihusisha na vita hiyo kwa kuwa siyo jambo la kuachwa liendele.

Wamesema nchi za Afrika japo zipo ambazo hazijaweka wazi msimamo wao kuhusu kuchagua upande katika vita hiyo ikiwemo Tanzania ambayo haikutaja upande wake katika kura zilizopigwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, lakini wanaamini kuwa hawafurahishwi na kinachoendelea nchini Ukraine kwa kuwa raia wengi wanaathirika.

“Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ambayo pia inajulikana kwa jina la Mahakama ya Dunia imeshatoa tamko la kuitaka Urusi kusitisha mapigano na kuondoa vikosi vyake Nchini Ukraine.

“Demokrasia, uhuru na haki za raia wa Uraine zinapotea, EU ina uwekezaji mkubwa katika Afrika kuliko Urusi. Tunajua Tanzania haikupiga kura ya kuchagua upande lakini haifurahishwi na kinachoendelea Ukraine,” anasema Balozi wa Ufaransa, Nabil Hajlaoui.

Balozi Hajlaoui anaongeza kuwa wa Ufaransa hawana nia ya kuchocheza vita wala uchagua upande lakini kuendelea kwa vita kutamaanisha kuwa watu wengi ambao hawana hatia watazidi kumia, pia nia yao ni vita imalizike kwa mazungumzo.

“Lakini kama vita itaendelea vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake katika vita hiyo kwenye nafasi mbalimbali za kiuchumi na kwingineko,” anasema Balozi Hajlaoui.

Krzysztof Buzalski (Balozi wa Poland)
“Nchini kwetu tuna wakimbizi takribani milioni 2, takwimu zinaonyesha kuwa kama vita itaendelea inamaanisha kuwa wakimbizi wanaweza kufikia hadi milioni nane, hii ni kitu kibaya.

“Kuhusu madai ya uwepo wa ubaguzi kwa watu Weusi hatujapata taarifa hizo rasmi japo tulisikia, lakini kama kweli vitendo hivyo vipo basi tunalaani kwa nguvu zote.”

Manfredo Fanti (Balozi wa EU)
“Tanzania inatambua maana ya kuwa na wakimbizi na imekuwa ikiwapokea kutoka nchi za jirani, kuna mamilioni ya watu wanateseka.

“Hii ndiyo maana EU imeamua kuweka bajeti ya kununua silaha kuisaidia Ukraine kujilinda. Tunategemea wafuasi mbalimbali wa UN wataunga mkono hiki kinachoendelea.”
View attachment 2160664
View attachment 2160665

View attachment 2160666
Dawa imewaingia kweli kweli
 
Utapangiwa tuu,una nini mpaka usipangiwe? Anapangiwa mchina sembuse wewe
... sidhani kama atakuelewa huyo. Machina leo kapeleka msaada Ukraine. Ila pro-Putin wana traits fulani hivi za ajabu ajabu.
 
Hatupazi sauti, kama zenu haziwatoshi ongezeni na speaker. Pumbav zenu Congo mpaka leo wanauwana sababu ni nyie ili mpate kuiba madini yao mbona hatukuwasikia kulaani. Nchi zote ulimwenguni zinazopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe sababu ni nyie ili muibe madini, mafuta, gas asilia na vinginevyo. Ingawa vita sio nzuri hata kidogo watesekao ni watoto,wazee na watu wasio kuwa na hatia.
Mkome kuyuingiza kwenye vita zenu.
 
In context, Putin gave Ukraine an entire year to resolve the issue diplomatically. Instead of doing that, Ukraine followed the US's lead and kept poking the bear. When Putin poked back the US stepped aside and let Ukraine take the full force of it.
 
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuendelea kulaani kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine na kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi.

Tamko hilo limetolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

Wakizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, leo Jumanne Machi 22, 2022 mabalozi hao wa Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uholanzi, Sweden, Finland, Hispania, Italia na Balozi wa EU wamesema kuwa vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake wote wanaojihusisha na vita hiyo kwa kuwa siyo jambo la kuachwa liendele.

Wamesema nchi za Afrika japo zipo ambazo hazijaweka wazi msimamo wao kuhusu kuchagua upande katika vita hiyo ikiwemo Tanzania ambayo haikutaja upande wake katika kura zilizopigwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, lakini wanaamini kuwa hawafurahishwi na kinachoendelea nchini Ukraine kwa kuwa raia wengi wanaathirika.

“Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ambayo pia inajulikana kwa jina la Mahakama ya Dunia imeshatoa tamko la kuitaka Urusi kusitisha mapigano na kuondoa vikosi vyake Nchini Ukraine.

“Demokrasia, uhuru na haki za raia wa Uraine zinapotea, EU ina uwekezaji mkubwa katika Afrika kuliko Urusi. Tunajua Tanzania haikupiga kura ya kuchagua upande lakini haifurahishwi na kinachoendelea Ukraine,” anasema Balozi wa Ufaransa, Nabil Hajlaoui.

Balozi Hajlaoui anaongeza kuwa wa Ufaransa hawana nia ya kuchocheza vita wala uchagua upande lakini kuendelea kwa vita kutamaanisha kuwa watu wengi ambao hawana hatia watazidi kumia, pia nia yao ni vita imalizike kwa mazungumzo.

“Lakini kama vita itaendelea vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake katika vita hiyo kwenye nafasi mbalimbali za kiuchumi na kwingineko,” anasema Balozi Hajlaoui.

Krzysztof Buzalski (Balozi wa Poland)
“Nchini kwetu tuna wakimbizi takribani milioni 2, takwimu zinaonyesha kuwa kama vita itaendelea inamaanisha kuwa wakimbizi wanaweza kufikia hadi milioni nane, hii ni kitu kibaya.

“Kuhusu madai ya uwepo wa ubaguzi kwa watu Weusi hatujapata taarifa hizo rasmi japo tulisikia, lakini kama kweli vitendo hivyo vipo basi tunalaani kwa nguvu zote.”

Manfredo Fanti (Balozi wa EU)
“Tanzania inatambua maana ya kuwa na wakimbizi na imekuwa ikiwapokea kutoka nchi za jirani, kuna mamilioni ya watu wanateseka.

“Hii ndiyo maana EU imeamua kuweka bajeti ya kununua silaha kuisaidia Ukraine kujilinda. Tunategemea wafuasi mbalimbali wa UN wataunga mkono hiki kinachoendelea.”
View attachment 2160664
View attachment 2160665

View attachment 2160666
Wasituingize katika ujinga wao....

Shetani hajawahi kuwa rafiki wa madhabahu ya BWANA......

#Siempre JMT🙏
 
Back
Top Bottom