Uchaguzi 2020 Umoja wa Ulaya (EU) wasikitishwa na baadhi ya mambo katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Umoja wa Ulaya (EU) wasikitishwa na baadhi ya mambo katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Umoja wa Ulaya (EU) umesikitishwa na kitendo cha kuiminya mitandao ya kijamii kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 ambao umelalamikiwa kuwa na viashiria vya udanganyifu.

Pia wamesikitishwa na malalamiko ya upinzani kutopewa nafasi sawa pamoja na kuwa na nafasi finyu kwa waangalizi wa Uchaguzi jambo ambalo linapelekea kufinya uwazi na uthabiti wa uchaguzi.

Wamesikitishwa na Vyombo vya usalama kutumia nguvu hadi kupelekea vifo Zanzibar. Umoja wa Ulaya unatumaini kuwa na misingi ya kimakubaliano kati ya wadau ili kuwa na amani.

EU imeomba kuwepo na majadiliano ya wazi kati ya serikali, vyama vya upinzani na asasi za kiraia hatua ambayo itakuwa ni muhimu kuweka uhuru wa mawazo ambayo ni msingi wa Demokrasia.

===

Representative on behalf of the EU on the elections in Tanzania​

The Tanzanian National Electoral Commission and Zanzibar Electoral Commission have declared the results of the elections.

Election day was well organised and peaceful in many parts of the country. Nonetheless, the European Union (EU) notes with regret the disruption of social media before, on and after election day, claims of opposition candidates that they did not benefit from a level playing field during the electoral process, as well as the limited possibilities for electoral observation. Reports of irregularities in some districts are also raising concern. These serious allegations have an impact on the transparency and overall credibility of the process. They should be processed through legal means of redress.

In Zanzibar, tensions were reported, with deadly violence, including allegations of excessive use of force by State organs. The EU hopes that it will be possible to lay the foundation for a sustainable reconciliation between all stakeholders, in order to contribute to long-lasting peace and stability in the archipelago.

The EU encourages an open, constructive and inclusive dialogue between the Government of Tanzania, opposition political parties and civil society, and recognises peaceful expressions of opinions as essential to multi-party democracy and civic freedoms.

Tanzania has a strong record of stability, peaceful cohabitation and tolerance among its people. The EU and Tanzania have a long history of good relations, and the EU reaffirms its preparedness to contribute to joint next steps for political dialogue and economic cooperation.
 
Screenshot_20201103-054928_Chrome.jpg
 
Watu wa JF mnashangaza na kuchekesha.

Tanzania ina asilimia kubwa ya watu masikini ambao hawana hata hiyo elimu ya kukariri.
Na wengi kati ya hao masikini hawajui internet ni nini hivyo hata mitandao ya kijamii kama JF hawaitambui ambako CHADEMA ndipo walipokuwa.
Ila CCM ilisikika kwenye radio ambazo asilimia kubwa watu wasiojiweza ambao ni masikini wanazo sababu radio ni cheap kuliko simu yenye internet.

Hawajui yanayotokea kama kutoongezwa mishahara au kukosa ajira sababu hata shule hawakwenda na hata hawajaajiriwa na serikali.
Hivyo hayo hawayaoni.

Jamii Forums ina members 1000000 tu.
Na kwa kukisia asilimia 50-65 tu kati ya hao ndo walikuwa CHADEMA.
Na wengi ni wanachuo waliokosa ajira.
Wafanyakazi wa serikali ambao hawajaongezwa mishahara.
Wastaafu waliokosa mafao yao.
Wafanya biashara nk
Pia hao ni wachache ukilinganisha na masikini walioko Tanzania.

Sasa fikiria watu 550000 wa JF ulinganishe na mamilioni ya masikini wengi wasio na elimu yoyote ambao wao wanaishi ili wapate chakula na ngono.
Hata ukiwapa chakula,kofia,nguo basi watapiga kula chama chochote kile.
Wao kupiga kura ni kama ushabiki wa simba na yanga.
Ndio maana huku mtaani kwangu watu walikuwa wakicheza uchi barabarani sababu ya ushindi.
Hawajali kuhusu mazingira mabovu wanayoishi au mfumo mbovu wa elimu wala haki zao mradi wao waendelee kuishi tu wapate chakula na ngono.

Hivyo mnavyoandika kama JamiiForums ndio Tanzania nzima lazima nitilie shaka ufahamu wenu.

Hao wazungu wangekuja kuona uhalisia wa watu waliopiga kura.
Asilimia kubwa hawajitambui sababu ya umasikini physically and mentally.

NB: Nimeandika kama mtazania na sio kwa itikadi za kisiasa.
Nimeandika ili muone uhalisia na sio kulalamika bila ya kufikiri.

Hakuna kilichoibiwa isipokuwa mindset ya kushindwa inapojaribu kupambana na uhalisia.
Na hao wazungu kujali maslahi yao binafsi.

Tokeni humu JF nendeni nje ya nyumba zenu tembeeni mitaa ya uswahilini na huko vijijini mkaone wapiga kula.
Na hao wazungu kumbe nao hawana akili kufikiri watanzania wote wanatumia mitandao au wanazo akili ila wanajali maslahi yao zaidi.
Jamiiforums sio Tanzania nzima mkumbuke.
 
Watu wa JF mnashangaza na kuchekesha.

Tanzania ina asilimia kubwa ya watu masikini ambao hawana hata hiyo elimu ya kukariri...
Nakubaliana na wewe. Mtaji mkubwa wa CCM ni ujinga na umaskini wa watu wengi. Kwao, watu wakielimika wanakuwa tishio. Na ndio moja ya sababu ya kuzima zima mitandao kipindi hiki. Hawataki ukweli wa kilichotokea na kinachotokea ujulikane na wengi.

Pamoja na ukweli wa yote uliyoandika, nitashangaa kama utakuwa hujui kwamba kulikuwa na rafu kibao uchaguzi huu, kila kona ya nchi. Mpaka unajiuliza yote hayo ya nini. Kama CDM ipo JF tu, hofu ya nini mpaka walazimike kucheza rafu kwa kiwango kile? Si wangeshinda tu kiulaini mapema asubuhi kwa mtaji wao wa kila siku - ujinga wa mamilioni ya wapiga kura.

Ni kama kujiuliza mantiki ya mtu kuua mende kwa risasi. Unaanza kujiuliza, hivi ni mende tu kweli au kuna kingine? Isije kuwa tunaambiwa ni mende kumbe sio mende.
 
Watu wa JF mnashangaza na kuchekesha.

Tanzania ina asilimia kubwa ya watu masikini ambao hawana hata hiyo elimu ya kukariri...
Asante ndugu yangu, umeandika kitu ambacho nami niliwahi kutamani kuandika hapa lakini wewe umeelezea vizuri sana.

Ukweli Ni kwamba huku nje ya mitandao kuna watu wengi sana ambao hawaoni haya yanayo hubiriwa kila Leo na Hawa watu wachache kwenye tweeter jamii forum Instagram Facebook nk.

Kwa hio haya matamko, dhana ya kuibiwa kura, sijui kunajisi uchaguzi sijui kulawiti na kubaka uchaguzi hawavielewi kamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipe sababu ya kuamini nilichoandika ni pumba.

Otherwise ulichoandika ni uongo ulioegemea emotions.
Hivyo ni sawasawa na kujiongelewa mwenyewe.

Yaani umeprove kauli yako ni pumba.

Pia huwezi kunielewa sababu unasikiliza bongo fleva.
Sasa nenda katoe taarifa celebrity forums kwamba diamond ametoa nyimbo mpya na cloud tv hawajaionyesha.

NB:nasikitishwa sana kuona africans wenye ufahamu uliodumaa.
 
Back
Top Bottom