Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Neno mahali pa kutumia 'kura' wewe umelirudia rudia kuwa ni 'kula'!
Nikawa ninawaza: kwa kuwa umesema waTz wengi ni masikini wasio na uwezo wa kumiliki vyombo vyenye kutumia internet,hivyo wanayaishi maisha yao kwa ajili ya kula na ngono zembe ama ulimaanisha 'kura' kiuhalisia?
Kuna sababu gani ya kupotosha spelling kwenye mada muhimu kama hii?
Itoshe kusema mantiki ya andishi lako imeeleweka vyema.
Ila sisi tusio na vyama ama kuegemea upande, kama haya maneno yasemwayo ya ghushi yakawa yalitokea kweli, basi hao waliyofanya hayo wameamua kumpaka matope rais Magufuli kwa makusudi mazima na bila ya ulazima wowote kwa sababu rais Magufuli hata uchaguzi urudiwe leo na wasimamizi wakawa ni malaika,yeye ni mshindi tu kutokana na anavyokubalika.
Hujuma kwa watawala sazingine hufanywa kisayansi na watu waovu na wapinzani wao wa ndani kwa ndani kuonesha kama wanaunga mkono upande wanaodhamiria kuhujumu.
Hilo liwe ni jambo la kwanza kuchunguzwa katika hadidu za rejea kama wataunda tume.
Kwa tuhuma zinazochefua hivi, haikutakiwa kuzikanusha kisiasa siasa na blah blah za majukwaani.
Walitakiwa kabla ya kutoa tamko lolote, waunde tume ikiwezekana juu ya tume kuchunguza ukweli wa jambo hili kama limetokea na limetendeka kweli, kina nani waliohusika, nani aliwatuma, wajulikane kwa majina na washitakiwe si kwa kuvuruga uchaguzi tu bali na kwa uhujumu uchumi pia.
Ikibainika figisu zozote kufanywa na watu waliolishwa viapo vya uadilifu ili kutenda haki, wakanajisi viapo vyao wachukuliwe hatua madhubuti zenye kuogofya mtu yeyote mwenye nia kama hiyo ovu kuja kutamani kufanya vitendo hivyo milele.
Rais Magufuli anakubalika sawa, je tume ya uchaguzi iliwajibika bila ya mawaa?
Yote hayo sasa yanatakiwa kujulikana kwa uwazi.