Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Mtoa mada tumikisha ubongo wako, siasa ni dymic Sio static. Hoja mahusi wakati muwafaka.Kila kikao na agenda zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Calvin ungependeza sana kuwa baa unachoma mishikaki na kuuza makongoro, huku siyo kwako wala haufanani nako, mbona Rombo, Mwika na Marangu zipo baa nzuri tu zinahitaji wachoma nyama nadhifu kama wewe!
 
Kama kikatokea chama fulani cha wahuni, kikawa na wabunge wengi, halafu serikali ya chama hicho ikapeleka bungeni mswada kuwa serikali inapendekeza kusiwepo uchaguzi; kwa fikra zako wewe, wananchi wote wanatakiwa kukaa kimya kwa sababu kuna wabunge wataenda kuujadili wakati unajua kabisa kuwa wabunge wale wapo kwenye genge lile lile la wahuni?

Zinatakiwa kutumika njia zote ili kuondoa mambo ya kihuni ambayo serikali inaweza kukusudia kuyafanya kuwa sheria dhidi ya watu wake.

Bunge litumike kupinga uhuni. Likishindwa Bunge, mahakama itumike. Mahakama ikishindwa, nguvu ya wananchi itumike. Ni lazima kuukataa utumwa, kuukataa udikteta, kuukataa uonevu, kuukataa ubaguzi wa namna yoyote ile, kukataa watu kutekwa, kupotezwa, kuuawa kama kuku, kukataa vyombo vya usalama kutumika katika njama za kisiasa.

Hakuna aliye juu ya umma. Bunge ni taasisi ndogo sana ikilinganishwa na umma wa wananchi. Bunge linapogeuka kuwa kama kikundi cha propaganda cha chama, wananchi wakiamua wanaweza kufutilia mbali hata Bunge.

Juu ya wote, hata juu ya Rais, kuna umma, ndio wenye uamuzi wa mwisho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna kituhapo
 
Wataungana kila uchwao ila muungano wa kinafiki. Muda ndio muamuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa,unawashauri,unawapinga au unawashambulia. Mara nyingi mmewasema watu wanaokosoa uongozi wa Rais,na kuwaona siyo wazalendo,mkawataka wamshauri. Waliopeleka kesi ya kupinga huo muswada ni viongozi,wana watu zaidi ya 6m nyuma yao. mbona mnawapinga na kufurahia kitachowapata? Je nanyi siyo wazalendo,au asiye mzalendo ni yule anayempinga Rais tu? Alafu oooooh watanzania tuungane kupambana na wazungu! Wakati ninyi ndiyo mnaoligawa taifa. Uvccm kule kigoma wanataka kuandamana kutaka uhamiaji kuangalia uraia wa zito Kabwe. Je hii ni akili timamu? Zito amekuwa kiongozi miaka mingapi,hao uhamiaji walikuwa wapi? Basi kama Zito siyo mtanzania,nchi haiko Salama. Yaelekea kila taasisi INA mamluki toka nje ya nchi wanafanyakazi bila taasisi za ulinzi na usalama kujua. Je wategemea wanaomuamini zito na kuamini kuwa ni mtanzania wataungana nanyi kupigana na wazungu vita mnayoiita ya kiuchumi? Mfalme suleman,aliomba hekima na akapewa,ALIJUA KUWA AKILI ANAZO. NINYI OMBENI AKILI MTAPEWA TENA BUREEEE,MUNGU NI MUAMINIFU NAYE ATAFANYA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…