Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Nenda mahakamani wewe upigwe nyundo ndo utajua kwanini huwa wanapongeza
 
Hizi hatua ndio nazikubali sana.
Sio kuishia kulalamika au kutukana watu.

Mimi naomba washinde kesi mahakamani hii sheria inayokataza watu kufanya mikutano ya kisiasa huku watu wakiruhusiwa kwa kuangalia wa chama gani sio sahihi kabisa.

Tunataka watu wafanye mikutano na wazungumze hoja sio matusi, dhiaka na kejeli kwa viongozi.

Tunataka watu wakosoe ili tusirudi kwenye ufisadi utakaomeza maendeleo yote anayoyaleta Mh. Magufuli.

Ukosoaji ndio umetuletea mtu makini kama huyu wa sasa. Unafikiri CCM wangempitisha Magufuli kama kusingekuwa na mbinyo na ushindani mkali toka vyama vya upinzani?

Kama Magufuli ana nia kweli ya kutuachia maendeleo na nchi imara inabidi aache upinzani wenye nguvu siku atakapo ondoka madarakani.
 
hizi siasa za hapa nyumbani pasua kichwa tu, yaani mtu unakua mpinzani for more than 20 years wewe unapinga tu kila administration; hatujawahi kukuona ukisupport chochote!

badilikeni jamani.
 
Badala ya kufanya ziara kwenye majimbo yao na kutatua kero za wananchi wamekalia kula ruzuku ya vyama vyao kwenye mahoteli ya kitalii kwa vijihoja vya kijinga kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii njia ya kwenda mahakamani nimeependa tena ni njia iliyochelewa. Sasa hivi kuna uovu mwingi lakini wanapata mpenyo kwamba kama inaonekana kuna matatizo basi mahakama zipo. Na hapa tunataka mahakama zifanye kazi yake, kinyume na hapo itabidi zitumike mbinu nyingine ambazo si njema sana. Hata huu wizi wa kura na kukiuka sheria za uchaguzi, inabidi mahakama itumike sana.
 
Badala ya kufanya ziara kwenye majimbo yao na kutatua kero za wananchi wamekalia kula ruzuku ya vyama vyao kwenye mahoteli ya kitalii kwa vijihoja vya kijinga kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki kitu ndicho kinanishangaza! Ukianga ule Muswada unakataza tu kufanya mikutano sehemu isiyo yako! Yaani kama Zitto ni mbunge wa Kigoma mjini basi akafanye mkutano huko Kigoma mjini aongee na wananchi wake, asikilize kero zao awape mrejesho lakini hawataki wao wanataka wote waje kufanyia mkutano hapa Dar wakati si sehemu zao! watu wa Dar wanakuja kutumbia nini hasa?
 
leo wamegundua kuwa kuna mahakama, au kwa vile mabeberu hayajisumbui na upuuzi wao?
 

Mahakama imegeuka kitengo cha watawala, inapotenda haki kwa wapinzani inakuwa ni jambo la kushangaza. Haki inafahamika sio kwamba chochote wafanyacho basi ndio haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…