Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Nenda mahakamani wewe upigwe nyundo ndo utajua kwanini huwa wanapongeza
 
Hizi hatua ndio nazikubali sana.
Sio kuishia kulalamika au kutukana watu.

Mimi naomba washinde kesi mahakamani hii sheria inayokataza watu kufanya mikutano ya kisiasa huku watu wakiruhusiwa kwa kuangalia wa chama gani sio sahihi kabisa.

Tunataka watu wafanye mikutano na wazungumze hoja sio matusi, dhiaka na kejeli kwa viongozi.

Tunataka watu wakosoe ili tusirudi kwenye ufisadi utakaomeza maendeleo yote anayoyaleta Mh. Magufuli.

Ukosoaji ndio umetuletea mtu makini kama huyu wa sasa. Unafikiri CCM wangempitisha Magufuli kama kusingekuwa na mbinyo na ushindani mkali toka vyama vya upinzani?

Kama Magufuli ana nia kweli ya kutuachia maendeleo na nchi imara inabidi aache upinzani wenye nguvu siku atakapo ondoka madarakani.
 
hizi siasa za hapa nyumbani pasua kichwa tu, yaani mtu unakua mpinzani for more than 20 years wewe unapinga tu kila administration; hatujawahi kukuona ukisupport chochote!

badilikeni jamani.
 
Badala ya kufanya ziara kwenye majimbo yao na kutatua kero za wananchi wamekalia kula ruzuku ya vyama vyao kwenye mahoteli ya kitalii kwa vijihoja vya kijinga kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii njia ya kwenda mahakamani nimeependa tena ni njia iliyochelewa. Sasa hivi kuna uovu mwingi lakini wanapata mpenyo kwamba kama inaonekana kuna matatizo basi mahakama zipo. Na hapa tunataka mahakama zifanye kazi yake, kinyume na hapo itabidi zitumike mbinu nyingine ambazo si njema sana. Hata huu wizi wa kura na kukiuka sheria za uchaguzi, inabidi mahakama itumike sana.
 
Badala ya kufanya ziara kwenye majimbo yao na kutatua kero za wananchi wamekalia kula ruzuku ya vyama vyao kwenye mahoteli ya kitalii kwa vijihoja vya kijinga kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki kitu ndicho kinanishangaza! Ukianga ule Muswada unakataza tu kufanya mikutano sehemu isiyo yako! Yaani kama Zitto ni mbunge wa Kigoma mjini basi akafanye mkutano huko Kigoma mjini aongee na wananchi wake, asikilize kero zao awape mrejesho lakini hawataki wao wanataka wote waje kufanyia mkutano hapa Dar wakati si sehemu zao! watu wa Dar wanakuja kutumbia nini hasa?
 
Viongozi waandamizi wa vyama mbalimbali vya upinzani leo watazungumza na waandishi wa habari. Watazungumzia maazimio ya #Azimio la Zanzibar.

Muda: Saa tano kamili asubuhi

Eneo: Makao Makuu ya CHAUMMA, Makumbusho, Dar es salaam.

======

UPDATES;

Viongozi Waandamizi wa Vyama mbalimbali vya Upinzani ACT, CUF na CHAUMMA wamefungua kesi Mahakama Kuu ya TZ Kanda ya DSM kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa minajili ya kupitishwa kuwa sheria, kesi hiyo itatajwa kesho kwa mara ya kwanza.

Wanataka muswada wa vyama vya siasa ujadiliwe kabla ya kupitishwa kuwa sheria itakayozuia vyama hivyo visifanye mikutano ya hadhara.

Vyama mbadala tumefanya juhudi kupinga mswada huu, tumetoka matamko, tumeshirikisha nchi wahisahi, mashirika ya kimataifa, AZAKI hapa nchini na viongozi wa dini, hizi ndizo hatua tumechukua kupinga.

Serikali imepeleka bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaohararisha agizo la Rais Magufuli mkoani Singinga mwaka 2016 kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na kufanya shughuli za kisiasa kuwa suala la jinai. - Zitto Kabwe.

Ni mswada unao kwenda kufifisha nguvu ya vyama vya siasa baada ya vyama vya siasa kuimalika na kuwa na uwezo wa kushindana kwa hoja.

Muswada huo unalenga kumfanya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na Mamlaka ya Usimamizi (Regulatory Authority), na kuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutawala na maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa ikiwemo kusimamisha / kumfukuza mtu uanachama.


Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria.

Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.

Amesema muswada huo unalenga kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.

“Tunawaomba wanachama wetu wote kesho tufike kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi hii, wanademokrasia waone kwamba hatujakaa tunachukua hatua,” amesema Zitto.

leo wamegundua kuwa kuna mahakama, au kwa vile mabeberu hayajisumbui na upuuzi wao?
 
Nimemsikia ndugu yangu Zitto Zuberi Kabwe leo akiipongeza mahakama kwa kuacha likizo na kuja kusiliza shauri walilolifungua kama vile ambavyo wengine wamekuwa wakiipongeza pale inapotoa hukumu vile wanavyokuwa wakihitaji mfano. Abdul Nondo, Tundu Lissu, Halima Mdee na Wengineo wengi.
Je mahakama ikifanya maamuzi kinyume na matarajio yake ataipongeza au atasema mahakama imemezwa na serikali?
Doublestandards in the game.

Mahakama imegeuka kitengo cha watawala, inapotenda haki kwa wapinzani inakuwa ni jambo la kushangaza. Haki inafahamika sio kwamba chochote wafanyacho basi ndio haki.
 
Back
Top Bottom