Pre GE2025 Umoja wa Vyama vya Siasa: Hatukubaliani na Maandamano ya CHADEMA, walijitenga nasi, sasa hivi wanatushirikisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haya mapandikizi ya CCM hayana hata ofisi
 
Hivi vyama vidogo havilalamiki chama dola kongwe CCM kukataa katiba mpya ya nchi, CCM kuendelea kupora mchakato mzima wa uchaguzi mkuu 2024 / 2025 kwa kupitia makada wake ambao ni wakurugenzi wa wilaya DED na wizara ya TAMISEMI, hali ngumu ya maisha, elimu ya kibaguzi kupitia shule za kata ....

Toka Maktaba :

17 February 2023

John Cheyo: Mazungumzo ya maridhiano kuendeshwa kwa gredi yaani ya 'ukubwa' wa vyama viwili tu siyo sahihi​

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki


Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima. Sasa vyama kama Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kinalalamika.
 
Cheyo amekuwa mtamu sahivi kaongea point sn sijaona tatizo kwake
 
Halafu huyo Mwenyekiti wao anadai baada ya leo watakutana kupanga maandamano ..... sasa anapinga maandamano ya CDM halafu wanataka kupanga maanamano mengine .... ya kupinga maandamano ya CDM sijui!!?
Waulize hata ofisi zao zipo wapi
 

Hivi hawa jamaa wa akili kweli .......!!?
 
Mfahamu AGENT PROVOCATEUR
Huyu ni mtu ambaye ni mtu wa mfumo au anatumiwa na mfumo kuvuruga kikundi cha kisiasa au harakati ili kuleta migongano na mifarakano! Pia wanaweza kuhamasisha harakati itumie silaha, ifanye vurugu au kutumia mbinu haramu ili ipoteze uaminifu

NAMNA YA KUMTAMBUA AGENT PROVOCATEUR

👉🏽 huwa wanazuka na kujiweka karibu na kikundi husika

👉🏽 huwa wanaleta mijadala isiyo na manufaa ili kupoteza malengo

👉🏽 huwa wanapenda kuacha mifarakano katika makundi (groups) na huwa wao ndo chanzo

👉🏽 huwa wanatafuta watu wasioridhika na jambo na kuwakuza walete ugomvi

👉🏽HUWA HAWANA MAPATO YANAYOELEWEKA -

lifestyle yake mfano anamiliki gari ila vyanzo vya mapato yake hayaeleweki lakini hasumbuliwi na mfumo (siyo mhalifu)

👉🏽huwa wanatoa zawadi na kujiweka karibu na watu wenye ushawishi katika kikundi

👉🏽 wakiulizwa kuhusu kutumika kwao huwa wanageuza kibao na kuanza kushambulia

👉🏽 wanajifanya wana mapenzi sana na kikundi husika au harakati lakini kumbe hawajali

KUMBUKENI hawa huwa NDANI ya kikundi cha kisiasa au harakati mfano kama ni chama wana kadi ya uanachama na kama ni harakati ni group member - si watu wa nje!

Viongozi wana jukumu la kuwatambua na kushughulika na agents provacateur kabla hawajasambaratisha kikundi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…