Pre GE2025 Umoja wa Vyama vya Siasa: Hatukubaliani na Maandamano ya CHADEMA, walijitenga nasi, sasa hivi wanatushirikisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa unaoundwa na Vyama 13 vyenye usajili Nchini unazungumza na Wanahabari, leo Jumatano Januari 17, 2024.

View attachment 2874297
Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa, Abdul Mluya

Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa, Abdul Mluya anasema "Mnamo Tarehe 13/01/2024 Mwanasiasa mwenzetu ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) alizungumza na Waandishi wa Habari na kutangaza maandanamano kuishinikiza Serikali kuiondoa Bungeni Miswada Mitatu inayoleta mageuzi ya Kisiasa hapa Nchini, Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi, Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi.

"Mimi ni miongoni mwa Watu ambao tuliwasilisha Miswada yetu pale Bungeni kama Chama na Vyama vingine na Siku Mwenyekiti anafunga nilikuwa miongoni mwa Watu waliokuwepo mule ndani na alihitimisha kwa kusema Vyama 18 vimetoa maoni Bungeni, vingine kwa maandishi vingine kama tulivyokwenda lakini Taasisi mbalimbali alizitaja na Viongozi wa Dini.

"Mara baada ya tukio lile kumalizika Mwanasiasa mwenzetu ambaye ni Katibu Mkuu mwenzetu (John Mnyika wa CHADEMA), kazi yetu ilikuwa ni kutoa maoni sio kukosoa Muswada kwa maana ya kuutupa."

Abdul Mluya: Chama kitengeneze sera za kuungwa mkono
Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Abdul Mluya anasema "Tufanye siasa za hoja tusigusane maungoni, hata Sheria ya Vyama vya Siasa inasema Chama kitakuwa na wajibu wa kuunda sera kwa lengo la kuungwa mkono, hilo limekaa sahihi sana kuliko njia wanayotaka kuitumia."

Abdul Mluya: CHADEMA waache ubinafsi
Tunawasii sana viongozi wenzetu na chama chao (CHADEMA) kuendelea kutumia njia sahihi zilizopo za Kisheria kushirikina na wengine (sisi) pamoja na kuacha ubinafsi na kuacha tabia ya kupinga kila jambo.

Abdul Mluya: Mbowe aombe radhi
"Viongozi wa Kidini tunaowaheshimu sana walitoa maoni yao, sasa nikitokea Mluya Mimi nikasema utupwe maana yake ni kwamba wale wote waliotoa maoni hawana akili, kwahiyo tunamtaka huyu Kiongozi mwenzetu (Freeman Mbowe) aombe radhi kwa Viongozi wa Dini ili kuleta mustakabali bora kwa Taifa letu.

Abdul Mluya: Maandamano yanakinzana na Utamaduni wetu
"Malengo yetu ni kuanzisha malengo mahsusi dhidi ya amani na Umoja wa Kitaifa wa Nchi yetu, njia hii ya maandamano yanakinzana na Utamaduni wetu kwa sababu Ina viashiria vya kuvunja amani, ni haki lakini si kila haki uitumie, haki nyingine unaziacha sio maandanamano tu, ni haki kwa Chama kupeleka maendeleo kwa Wananchi wake lakini hatufanyi."

Abdul Mluya: Waliopinga Kikosi Kazi, leo wanasema maoni ya Kikosi Kazi yamepuuzwa
"Inashangaza kuona waliopinga mchakato wa Kikosi Kazi leo wanasema maoni ya Kikosi Kazi yamepuuzwa, huu ni unafiki, kiburi na kwenye Demokrasia kama hatutaepuka unafiki, kiburi, kutoshirikiana na wenzako hatutofika, tutaendelea kupingana mpaka pale tutakuwa sote ni wamoja, malengo yetu ya Kikatiba.

"Tunapaswa kutanguliza maslahi ya Wananchi mbele na sio maslahi yetu sisi na matumbo yetu au Vyama vyetu, leo inashangaza sana kuona leo unasikia eti maoni ya Kikosi Kazi yametupwa, maoni mengi ya Kikosi Kazi yamechukuliwa na Vyama vinaendelea kutoa maoni kuboresha Miswada husika, maoni yale tuliyoenda kutoa ni zao la Kikosi Kazi."

View attachment 2874343
Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo

Doyo: Watu 7 walikufa kabla ya maandamano Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo anasema “Tunaiomba Serikali isitishike kwa ajili ya maandamano ya Chama kimoja kwa faida ya wengi.

“Maandamano ni ajali, nikiwa CUF Mwaka 2001 kabla ya maandamano walikufa watu saba.”

Pia soma:
= Maandamano ni Haki ya Vyama vya Siasa, Serikali itoe kila ushirikiano kwa CHADEMA hata kama uelekeo ni Ikulu
= Kama Jeshi litafanya usafi tarehe 23-24, basi CHADEMA ifanye maandamano tarehe 25 wapite njia zikiwa safi
= Hizi ndizo sababu Watanzania hawatoshiriki maandamano ya CHADEMA

Hawa hawataki hata katiba mpya
 
Hivi vyama vidogo havilalamiki chama dola kongwe CCM kukataa katiba mpya ya nchi, CCM kuendelea kupora mchakato mzima wa uchaguzi mkuu 2024 / 2025 kwa kupitia makada wake ambao ni wakurugenzi wa wilaya DED na wizara ya TAMISEMI, hali ngumu ya maisha, elimu ya kibaguzi kupitia shule za kata ....

Toka Maktaba :

17 February 2023

John Cheyo: Mazungumzo ya maridhiano kuendeshwa kwa gredi yaani ya 'ukubwa' wa vyama viwili tu siyo sahihi​

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki

Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima. Sasa vyama kama Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kinalalamika.

Tanzania kuna vyama vingapi vya Siasa? Sina uhakika kama vinazidi vitatu.
 
Halafu ktk mkutano wao wanakimbia maswali ya waandishi wa habari huku wakidai vyama hivi vidogo ni makini.

Umakini wa chama chochote cha siasa ni uwezo wa kushawishi umma ili kiingie madarakani / kuchukua Dola lakini muungano wa vyama hivi ni kukitetea chama kongwe dola CCM kuzidi kuisigina katiba, rais kuvunja katiba, rais kuonekana kuwa ni nusu Mungu anayeweza kutoa hisani wakati kakiuka misingi ya katiba ya nchi .... anapambwa, kusifiwa, kuimbiwa mapambio, kusujudiwa hata pale anapokandamiza uhuru ukiotamkwa ndani ya katiba ya nchi kifupi rais wa CCM kuitwa Mungu kama Julius Caesar wa dola ya Warumi

1705501276495.png
 
Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa unaoundwa na Vyama 13 vyenye usajili Nchini unazungumza na Wanahabari, leo Jumatano Januari 17, 2024.

View attachment 2874297
Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa, Abdul Mluya

Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa, Abdul Mluya anasema "Mnamo Tarehe 13/01/2024 Mwanasiasa mwenzetu ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) alizungumza na Waandishi wa Habari na kutangaza maandanamano kuishinikiza Serikali kuiondoa Bungeni Miswada Mitatu inayoleta mageuzi ya Kisiasa hapa Nchini, Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi, Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi.

"Mimi ni miongoni mwa Watu ambao tuliwasilisha Miswada yetu pale Bungeni kama Chama na Vyama vingine na Siku Mwenyekiti anafunga nilikuwa miongoni mwa Watu waliokuwepo mule ndani na alihitimisha kwa kusema Vyama 18 vimetoa maoni Bungeni, vingine kwa maandishi vingine kama tulivyokwenda lakini Taasisi mbalimbali alizitaja na Viongozi wa Dini.

"Mara baada ya tukio lile kumalizika Mwanasiasa mwenzetu ambaye ni Katibu Mkuu mwenzetu (John Mnyika wa CHADEMA), kazi yetu ilikuwa ni kutoa maoni sio kukosoa Muswada kwa maana ya kuutupa."

Abdul Mluya: Chama kitengeneze sera za kuungwa mkono
Mwenyekiti wa Umoja Umoja wa Vyama vya Siasa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Abdul Mluya anasema "Tufanye siasa za hoja tusigusane maungoni, hata Sheria ya Vyama vya Siasa inasema Chama kitakuwa na wajibu wa kuunda sera kwa lengo la kuungwa mkono, hilo limekaa sahihi sana kuliko njia wanayotaka kuitumia."

Abdul Mluya: CHADEMA waache ubinafsi
Tunawasii sana viongozi wenzetu na chama chao (CHADEMA) kuendelea kutumia njia sahihi zilizopo za Kisheria kushirikina na wengine (sisi) pamoja na kuacha ubinafsi na kuacha tabia ya kupinga kila jambo.

Abdul Mluya: Mbowe aombe radhi
"Viongozi wa Kidini tunaowaheshimu sana walitoa maoni yao, sasa nikitokea Mluya Mimi nikasema utupwe maana yake ni kwamba wale wote waliotoa maoni hawana akili, kwahiyo tunamtaka huyu Kiongozi mwenzetu (Freeman Mbowe) aombe radhi kwa Viongozi wa Dini ili kuleta mustakabali bora kwa Taifa letu.

Abdul Mluya: Maandamano yanakinzana na Utamaduni wetu
"Malengo yetu ni kuanzisha malengo mahsusi dhidi ya amani na Umoja wa Kitaifa wa Nchi yetu, njia hii ya maandamano yanakinzana na Utamaduni wetu kwa sababu Ina viashiria vya kuvunja amani, ni haki lakini si kila haki uitumie, haki nyingine unaziacha sio maandanamano tu, ni haki kwa Chama kupeleka maendeleo kwa Wananchi wake lakini hatufanyi."

Abdul Mluya: Waliopinga Kikosi Kazi, leo wanasema maoni ya Kikosi Kazi yamepuuzwa
"Inashangaza kuona waliopinga mchakato wa Kikosi Kazi leo wanasema maoni ya Kikosi Kazi yamepuuzwa, huu ni unafiki, kiburi na kwenye Demokrasia kama hatutaepuka unafiki, kiburi, kutoshirikiana na wenzako hatutofika, tutaendelea kupingana mpaka pale tutakuwa sote ni wamoja, malengo yetu ya Kikatiba.

"Tunapaswa kutanguliza maslahi ya Wananchi mbele na sio maslahi yetu sisi na matumbo yetu au Vyama vyetu, leo inashangaza sana kuona leo unasikia eti maoni ya Kikosi Kazi yametupwa, maoni mengi ya Kikosi Kazi yamechukuliwa na Vyama vinaendelea kutoa maoni kuboresha Miswada husika, maoni yale tuliyoenda kutoa ni zao la Kikosi Kazi."

View attachment 2874343
Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo

Doyo: Watu 7 walikufa kabla ya maandamano Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo anasema “Tunaiomba Serikali isitishike kwa ajili ya maandamano ya Chama kimoja kwa faida ya wengi.

“Maandamano ni ajali, nikiwa CUF Mwaka 2001 kabla ya maandamano walikufa watu saba.”

Pia soma:
= Maandamano ni Haki ya Vyama vya Siasa, Serikali itoe kila ushirikiano kwa CHADEMA hata kama uelekeo ni Ikulu
= Kama Jeshi litafanya usafi tarehe 23-24, basi CHADEMA ifanye maandamano tarehe 25 wapite njia zikiwa safi
= Hizi ndizo sababu Watanzania hawatoshiriki maandamano ya CHADEMA

Chama cha upinzani ni CDM TU. Wanatosha kuandaa maandamano.
Wengine wachumia tumbo!
 
Halafu ktk mkutano wao wanakimbia maswali ya waandishi wa habari huku wakidai vyama hivi vidogo ni makini.

Umakini wa chama chochote cha siasa ni uwezo wa kushawishi umma ili kiingie madarakani / kuchukua Dola lakini muungano wa vyama hivi ni kukitetea chama kongwe dola CCM kuzidi kuisigina katiba, rais kuvunja katiba, rais kuonekana kuwa ni nusu Mungu anayeweza kutoa hisani wakati kakiuka misingi ya katiba ya nchi ....
Vingine vinavyoitwa vyama vya aisas ni "mzigo" kwa Taifa! Bora "vikufe" instantly!
 
Vyama vya Siasa visipewe ruzuku iwe kujitolea.
Ingekuwa vizuri zaidi! Kila Chama kijiendesha kwa michango ya wanachama wake. Hata hivyo, endapo hilo litapitishwa, bado kutakuwepo na vichache vitakavyokuwa vikipewa "ruzuku" kwa mlango wa nyuma, hasa vile vinavyowanufaisha wakubwa fulani.
 
Back
Top Bottom