Umoja wa wanawake CCM wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko

Umoja wa wanawake CCM wasikitishwa na udhalilishaji wa Makonda, watoa tamko

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa.

View attachment 2999802
ERYTHROCYTE HILO NI LA CCM WAACHIE WENYEWE WEWE DEAL NA MBOWE TU HATA LISSU HAKUHUSU
 

Attachments

  • 20230630_184030.jpg
    20230630_184030.jpg
    49.6 KB · Views: 1
Makonda ni kiongozi bora hata zaidi ya Rais Samia. Kiongozi wa aina yake huwezi kumpata popote. Tatizo uchawa wa kipuuzi unawasumbua wengi sana na ndio products za CCM hizo.
 
Muda mfupi baada ya RC Makonda kusema hatishwi na wanamitandao wanaompigia makelele anapochapa Kazi, mjukuu wa baba wa taifa la Zanzibar Fatma Karume amemjibu Ukurasani X

Fatma Karume anasema RC Makonda amepigwa SPANA na Umoja wa Wanawake Tanzania na kisha akamuuliza " Unajua Power ya UWT ndani ya CCM?"

Kiukweli Bongo hakunaga jambo Dogo 😂😂

Ngoja tuone!
 
Anasema mtapata wengine wakuwa petipeti. Mpuuzi sana huyu MAKONDA
Ukifuatilia matendo yake ni kama hapajawahi kuwa na serikali wala RC hapo arusha
 
Anasema mtapata wengine wakuwa petipeti. Mpuuzi sana huyu MAKONDA
Ukifuatilia matendo yake ni kama hapajawahi kuwa na serikali wala RC hapo arusha
Sasa kulikuwa na uongozi gani mpaka watu wanatengeneza CONTROL NUMBER FAKE!??!?,wakuu wa vyombo vya usalama wapo, TAKUKURU wapo, wakuu wa wilaya wapo. Hii nchi ni kama ipo kwenye AUTOPILOT,inajiendea tu. Anatokea mtu wa kushurutisha wazembe k.enge zinatoka mafichoni kutetea wazembe.
 
Uongozi ni busara na kuwa na uchaguzi mzuri wa maneno,anachokifanya Paulo si sawa.....japo nchi yetu inamauza uza mengi inahitaji mtu asiyeyumbishwa
 
Power ya UWT ijielekeze kwenye kushughulikia majizi ya Halmashauri ya Arusha.
Hebu shangaa kidogo, kuna wamama wananyanyaswa mahospitalini, kuna wamama wastaafu(bibi zetu) wanazungushwa mafao yao, wengine mpaka wanakufa kwa pressure ila husikii huo umoja wa wanawake ukiwatetea, leo hii wanakomaa na ishu ya mtu mmoja tena mzembe kweli kwenye majukumu yake.
 
Sasa kulikuwa na uongozi gani mpaka watu wanatengeneza CONTROL NUMBER FAKE!??!?,wakuu wa vyombo vya usalama wapo, TAKUKURU wapo, wakuu wa wilaya wapo. Hii nchi ni kama ipo kwenye AUTOPILOT,inajiendea tu. Anatokea mtu wa kushurutisha wazembe k.enge zinatoka mafichoni kutetea wazembe.
Mpaka sasa amekomesha wazembe wangapi?
 
Mpaka sasa amekomesha wazembe wangapi?
List ipo TAKUKURU, sio kila kitu cha kuanika mitandaoni, ila vita anayopigwa Makonda Arusha ni kubwa sana. Mpaka sasa kuna watu zaidi ya 10 kwenye nafasi nyeti wapo kando wanasubiri kujua hatma yao na anytime utawaona wakifikishwa mahakamani karatasi zinawekwa sawa za ushahidi.
 
Zote hizo ni chuki tu kwani amemdhalilisha nini huyo nwanamke sems lugha aliyotumia ndio sio nzuri. Mimi namuomba radhi huyo mwanamke kwa niaba ya Makonda msamehe. Makonda tunamuhitaji sana mkoani Arusha.
 
😄

Ya Kasesela pale Mkwawa yalianzaga hivi hivi baadae tukasikia Utumbuzi 😂😂🔥
Ni kati ya indication ya serikali dhaifu inayoyumbishwa kirahisi. Hili jambo tayari rais analijua, ila kwa vile hawa wanajua kuwa wanaweza kumyumbisha basi watalirudia rudia hadi afanye wanavyotaka wao, na huo ndio udhaifu wa serikali wenyewe. Rais aliposema kuwa kila mtu atakaula kwa kamba yake kwa nini wao hawakusema kuwa huo ni udhalilishaji kwa wale wasiokuwa na kamba? Viongozi pia huteleza midomo na hiyo ikishatokea basi siyo vizuri kuigeuza kuwa ajenda ya taifa
 
Back
Top Bottom