Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje
Maelezo haya yote ni mazuri, lakini cha kujiuliza ni nini kiliwaziba midomo kupelekea hadi akina Mpina kujeruhiwa kwa hila?

Kwanini wasingelitoa ushuhuda wa tamko hili mapema haraka iwezekanavyo ili kuuweka ukweli wa tuhuma hizo potofu mapema?

Tz imegawika kwa kunyamazia maneno haya kwa kushindwa kuyatoa kwa wakati.

Wengi wapo upande wa Waziri kwa namna walivyoaminishwa na maneno yake ya shobo juu ya tuhuma nzito kuhusu wenye viwanda kuweka mazingira ya uhaba.

Ni wachache tu wenye akili kubwa ndiyo wapo na Mpina baada ya kutumia jicho la tatu kuusaka ukweli wa mambo.

Mnakujaje kutoa ushahidi wa mtu aliyetuhumiwa kwa kesi ya mauwaji ya uongo na tayari alikwisha hukumiwa na adhabu ya kunyongwa ilishatekelezwa?
Uliamini kwakua umeambiwa uamini au kwakua ulikuwa unaangalia facts?
 
Kwann mnamwonea bashe?tulikuwa hatuwasikii mawaziri wa kilimo ni km hyo wizara haipo,leo iko kwa bashe mnatupia mawe. why? huyu jamaa ni mchapakaz napia ni hodari.bashe piga kazi wache wapige kelele watanyamaza
Kuwajibu hawa ni sehemu ya uchapa kazi wake kwa hiyo ni matarajio yetu kuwa atawajibu
 
Namheshimu sana Balozi Ammy Mpugwe, anadai amekuwa kwenye tasnia ya sukari akiwa na miaka 10 sasa ana miaka 76, kuna wakulima elfu 80 na elfu kumi wana mashamba, obvious elfu 70 ni manamba,

sasa, sasa miaka hamsini ya kilombero suger still we are importing suger? yet we are exporting suger on smaggling way based on economic osmosis!

anasema yeye hauzi vocha that means he is a gianty man. why are we still buying suger from brazil yet suger hii is cheaper than from his home land kilombero?

lakini, how is the man credible to our socity? ammy huyu wa tanzania one? huyu ammy wa capital mining? no no no, hapana kabisa.
Hapa hata Mimi nilishangaa sana, japo na support utetezi wake kwasababu ya facts za Mpina, lakini kwenye watanzania hapana, hakutenda haki
 
Mpina hawezi kumalizika kirahisi hivyo.

Spika Tulia ameamua kulinda ufisadi
Spika Tulia anatoka chama gani?

Mpina anatoka chama gani??

Wabunge waliopo bungeni 99.9% ni chama gani??

Nani ali-engineer bunge kibogoyo la namna hii?

Kwenye hii angle najua utaruka ila mkitaka asifiwe pia mkubali kuna mahali pia amelifikisha taifa hivyo mtulie tu.

Samia ni mrithi wa huyo shujaa wenu na karithi 100% ya watu wake.

Nyumba inawaka moto wakati mlimuona mtu kaingia na sigara iliyowaka ndani halafu kaiangusha kwenye sponge halafu mseme hamjui moto ulianzia wapi?

Who is fooling who??
 
Kwann mnamwonea bashe?tulikuwa hatuwasikii mawaziri wa kilimo ni km hyo wizara haipo,leo iko kwa bashe mnatupia mawe. why? huyu jamaa ni mchapakaz napia ni hodari.bashe piga kazi wache wapige kelele watanyamaza
Kuchapa kazi ndio wajibu wake na analipwa kwa hilo. Hivyo hilo halimhalalishii kujingiza kwenye ufisadi
 
Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

“Kulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

“Sisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

“Tulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

“Tumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

“Gharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; “Ningekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
Nitakuwa mtu wa ajabu kuamini Ame Mpunga wa Iilovo na Seif A Seif wa Kagera/,Mtibwa ni watu Safi hawatafuti super profits na wana huruma kubwa na wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nitakuwa mtu wa ajabu kuamini Ame Mpunga wa Iilovo na Seif A Seif wa Kagera/,Mtibwa ni watu Safi hawatafuti super profits na wana huruma kubwa na wananchi.
Wanatafuta kwenye kuzalisha na siyo kuagiza sukari
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Bashe alitaka kuwaangishia jumba bovu Watengeneza sukari naona wamekataa
 

kuna wakati namwelewa mpina, na kuna wakati namwelewa msomali. wafanyabiashara wa sukari kila mwaka wamekuwa wakihodhi ili bei ipande, walimonopolize sana soko, na kwa wenzetu waislam, kila mfungo ukija huwa wanajiandaa kupanda sukari kwasababu wafanyabiashara wanajua tu lazima watu watakunywa sukari, uji au kuweka sukari kwenye vitafunwa au tambi n.k wanapandisha sukari, masikini wanateseka mno. hivi wewe kama ni waziri, kwanini usiagize sukari hata kwa kuvunja vifungu ili kukomoa wafanyabiashara?

nikurudi kwa mpina,anapotoa tuhuma kwamba inawezekana kuna kina abdul wameongeza kabei ambako kanaenda mfukoni mwao, hapo naogopa naona tena bora wafanyabiashara. hili jambo liwekwe wazi. tuna maslahi nao wananchi.
 
Mpina yuko sahihi 100%

Huyu nsomali afukuzwe aende anakokujua!
 
Watoto wa 2000 hamumjui huyo Balozi msitaafu tunayemjua tunajua ni mtu wa namna gani.
 
Hapa sijapaelewa vizuri.ina maana huwa tunauza sukari nje ya nchi?
Hivi viwanda kiutaratibu kipindi cha low season hupewa vibali na serikali waagize sukari ije nchini kutoka nchi nyingine.

Lakini kwa wakati huo hawakupewa vibali kwa wakati. Bila shaka hili lilisababisha pia upotevu wa sukari sokoni. Ila wao kwa kutumia ukubwa wao, kuna meli ilikuwa inapeleka sukari nchi nyingine, hivyo wakajiongeza ilete hapa nchini wakati wakiendelea kufuatilia vibali.

Sisi kuuza nje sio rahisi, maana nchi jiran kwanza wanasukari bei nafuu.
 
Hivi viwanda kiutaratibu kipindi cha low season hupewa vibali na serikali waagize sukari ije nchini kutoka nchi nyingine.

Lakini kwa wakati huo hawakupewa vibali kwa wakati. Bila shaka hili lilisababisha pia upotevu wa sukari sokoni. Ila wao kwa kutumia ukubwa wao, kuna meli ilikuwa inapeleka sukari nchi nyingine, hivyo wakajiongeza ilete hapa nchini wakati wakiendelea kufuatilia vibali.

Sisi kuuza nje sio rahisi, maana nchi jiran kwanza wanasukari bei nafuu.
hivi mkuu haya maelezo yanakuingia akilini? yaani uagize meli ya sukari huyui inaenda wapi? vipi wangenyimwa vibali ingekuwaje?

kwanini ahusishe biashara ya vocha na bishara ya sukari hizi ni bidhaa mbili tofauti na sio substitute, kwanza upuuzi wa kukagua wamama kwa kutumia mbwa kule tanzania one hatujasahau, kuwavua nguo vijana wetu na kuwamulika kwa ct scan kuona kama wamemeza zanzanite hatujasahau, halafu anatupiga kwenye mshono, no way
 
Mkuu, usiongee bora umeongea tu, bila shaka umesikiliza video mpaka mwisho ingawa imechakachuliwa.

Kwanza Mzee Mpungwe ni "distinguished figure" kwenye nchi hii, hivyo ukimwongelea uangalie kila kona ya kazi zake katika nchi hii kabla hajaingia katika biashara miaka ya 90s.

Huko nyuma viwanda vilikuwa vikimilikiwa na serikali hivyo baadae vikabinafsishwa.

2015 sukari ilikuwa tani 200,000 kwa mwaka.

Tani 400,000 mwaka 2023 na sasa hivi mahitaji ya sukari yanaweza kutoshelezwa kwa asilimia 93.

Mwaka huu kuelekea mwishoni kutakuwa na Tani 528,000 kuanzia 2025/2025 yategemewa kuwepo na uzalishaji wa tani 660,000 na hata kuuza sukari hiyo nje ya nchi.

Kilombero Sugar wenyewe watarajiwa kuongeza uzalishaji sukari kutoka tani 130,000 kuwa tani 230,000 na pia wakulima wazungukao eneo la kiwanda nao watarajiwa kuongeza uzalishaji wa miwa 150,000 hadoi tani 300,000.

Tani 30,000 ni Gap sugar au nakisi na hii ni sukari ambayo ndo yagombewa na wauza vouchers.

Usisahau pia wakulima wa sasa wengi ni vijana ambao ni wasomi, hivyo wakopa kwenye mabenki ili walime mashamba ya miwa na wafanya hivyo wakichukulia kuwa kilimo hicho ndo njia bora ya kujiajiri badala ya kuzurura mijini.

Pia miwa ikiishatumika kupata sukari mabaki yake huweza kutumia kutengeneza nishati ya umeme ambao waweza kupelekwa kwenye NG.

Sasa angalia viwanda vyetu na ikiwa vyote vitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa taka za miwa wategemea kuwepo na tatizo la umeme kweli?

Ujinga huja pale mtu na akili zake anapokuwa akisema kwamba wakulima wa sukari washawishiwe kuacha kilimo cha miwa ili walime mazao mengine, what is this nonsense?

Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema ujinga una "levels" na ukifika kiwango cha juu ndo twaona yanoendelea saa hii huko bungeni, ni vituko.

Mtu mwingine akisema sie waafrika tuna matatizo na huwa twajiroga wenyewe na kisha akakupa facts tupu utambishia kivipi?
sijaelewa, kwenye maelezo yako unaelezea ishue za ujinga, upi? nani unaona ni mjinga mie au nani?
 
Back
Top Bottom