Habari za Mpungwe nilikuwa nazo siku nyingi sana wakati akiwa balozi South...
Nakumbuka vizuri ktk moja ya mageuzi yetu ya kiuchumi moja ya agenda kubwa ya chama CCM ilikuwa kuwatumia South Africa na hiyo SADC kuwa kiungo cha maendeleo ya nchi zetu kwa sababu wao walikuwa mbele na vitu vyote vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa kitechnologia.
Mpango huu ulianza wakati wa Mwinyi kama sikosei awamu yake ya pili na hata Mwalimu, Marehemu Nyerere aliupendekeza badala ya mazungumzo ya karibu na Mandela..
tatizo lilokuja ni kwamba badala ya kutumia SADC na kuunda benki ambayo ingeweza kusimama ktk mikopo ya miradi ya maendeleo na ujenzi wa infrastructure nchini kama walivyofanya wenzetu wa nchi za Asia kutokutegemea zaidi IMF na benki kuu ya Dunia, viongozi wetu walikuwa na agenda zao za binafsi.
Tatizo kama nilivyowahi kusema viongozi wetu ni watawala weusi sawa na wakoloni kimawazo na hutafuta mwanya wa kujitajirisha wao badala ya kufikiria maslahi ya nchi...
Hivyo, Makaburu wa kwanza kuingia nchini walijengwa na Ami Mpungwe ikiwa ni pamoja na kurudi kwa De Beers kule Mwadui. tatizo lililojitokeza ni kwamba hawa wote walikuwa opportunist na kila kampuni iliyoingia nchini walikuja kuchuma kutokana na udhaifu wa mikataba yetu ambayo kama kawaida viongozi wetu walitaka kukatiwa chao.. Mikataba mibovu iliingiwa ktk kipindi kifupi sana na hawa makaburu hadi likazuka sakata la Tanzanite yetu kule Marerani na wanunuzi wakubwa kama Zales kutokana na mbinu ya Wasouth kutaka kuchukua umilikaji wa migodi hiyo..Nadhani mtakumbuka jinsi report ya uuzaji wa Tanzanite ilivyotofautiana na ile report ya taifa ktk mauzo ya Tanzanite toka hapo tukaanza kuona vitu vingine vikiibuka toka NBC,TBL, TANESCO na kadhalika...
Kundi hilo walianza kugeukana yakazuka makundi kufikia wakati wa Mkapa kwa sababu SADC haikujengwa na kuimarishwa badala yake ilibomolewa na viongozi wa nchi zote zilizohusika kwa sababu wote hawa walikuwa na mipango nje ya jumuiya hiyo - Kujitajirisha wakati ndio huu.
Kwa hiyo, kama alivyosema FMES, viongozi wetu wote walikuwa na malengo yao na wakamtumia sana Ami Mpungwe kufunga ma -deal huko South..Ikifika wakati muafaka huyu jamaa anaweza kuwa dhamana kubwa ya serikali kiushahidi dhidi ya Mafisadi kwa wakati huo kabla viongozi wetu hawajajitanua zaidi kufikia nchi za Ulaya, US na Canada..